Wafanyabiashara wa Maduka Jijini Mbeya Wagoma Kupinga Manyanyaso ya TRA

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 22 май 2024
  • Baadhi ya Wafanyabiashara wa Maduka Mwanjelwa Kata Ruanda na Kabwe Kata ya Iyela Jijini Mbeya wamefunga maduka yao kwa kile walichodai kunyanyaswa na watumishi wa Mamlaka ya Mapato(TRA)Mkoa wa Mbeya.
    Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wafanyabiashara na wanunuzi nje ya maduka wamesema hupata usumbufu kutoka kwa wafanyakazi wa TRA.
    Kwa upande wake Musibu Shaban Meneja Mamlaka ya Mapato(TRA)Mkoa wa Mbeya amesema wao kama Mamlaka wanatekeleza majukumu yao zaidi wakidai baadhi ya wafanyabiashara hutoa stakabadhi kinyume na malipo.
    Hivi karibuni akiwa Mbeya Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji amepokea malalamiko na kuagiza malalamiko hayo yafanyiwe kazi.
    Mgomo huo wa wafanyabiashara umeleta usumbufu mkubwa kwa wateja wanaotoka nje ya Mkoa na nje ya nchi ambao wengi wao hupata mahitaji yao maduka ya Mwanjelwa na Kabwe.

Комментарии • 17