RC TABORA AAGIZA KUKAMATWA KWA WATUMISHI 3 NA MMILIKI WA ZAHANATI YA HOSSIANA KWA KULAZA WAGONJWA

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 9 фев 2025
  • #CgOnlineTv
    Mkuu wa mkoa wa Tabora, Paul Chacha ameagiza kukamatwa kwa watumishi watatu na mmiliki wa zahanati ya Hossiana Mission iliyopo Manispaa ya Tabora kwa kufanya upasuaji na kulaza wagonjwa kinyume cha taratibu na miongozo ya afya.
    Mkuu wa mkoa Chacha, amesema baada ya uchunguzi watakaobainika kuhusika na matukio hayo wafikishwe mahakamani huku akimuagiza mganga mkuu kufanya ukaguzi kwenye zahanati na vituo vyote vya afya mkoani humo na kuvifungia vituo vyote vitakavyobainika kukiuka kanuni za afya.
    Miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na kaimu mkurugenzi wa hospitali hiyo Sara Elias, mganga mfawidhi Ezra Masesu, mmiliki wa zahanati hiyo Dkt. Festo Jafari na daktari mmoja mstaafu ambaye hutumiwa kufanya upasuaji kituoni hapo.
    Awali mganga mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatinisibwa alimweleza mkuu wa mkoa kuwa timu ya afya ya mkoa ilibaini uwepo wa huduma za kulazwa wagonjwa katika zahanati hiyo kinyume cha taratibu na baada ya kufanya ukaguzi waliwakuta wagonjwa wawili waliopewa rufaa ya kwenda Bugando wakiwa wamelazwa na kuandaliwa kwa ajili ya upasuaji.
    Mganga mfawidhi wa kituo hicho Ezra Masesu amekiri kuwapokea wagonjwa hao akisema aliwapokea wagonjwa hao kwa maelekezo ya mmiliki wa kituo hicho ambaye ni daktari wa hospitali ya Rufaa mkoa wa Tabora Kitete aliyeko masomoni.
    Zahanati ya Hossiana Mission imefungiwa wakati huu ambao taratibu nyingine za kisheria zikiendelea kuchukuliwa.

Комментарии • 103