Dakika 25 za Mwigulu bungeni akiomba matumizi ya Sh18.17 trilioni 2024/25 yaidhinishwe

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 3 июн 2024
  • Serikali imewataka wananchi kuwasilisha malalamiko ya kodi kupitia namba ya bure, pia imeeleza changamoto wanazopata kukusanya kodi kwa kutumia mashine za kielektroniki za EFD.
    Mbali na hayo, Kamati ya Bunge ya Bajeti imezungumzia tatizo la malalamiko ya kodi, pia imesema masharti ya kumlinda mteja kwenye Sheria ya Sekta ndogo ya Fedha ndiyo suluhisho la mikopo kausha damu.
    Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amewasilisha bungeni mapendekezo ya mpango na bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2024/2025.
    Leo Jumanne Juni 6, 2024, wizara hiyo imeliomba Bunge kuidhinishiwa matumizi ya Sh18.17 trilioni kwa mwaka wa fedha 2024/25. Mwaka 2023/24, wizara hiyo iliidhinishiwa na Bunge Sh15.87 trilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo.
    Mwigulu ameliambia Bunge kuwa Bodi ya Rufani za Kodi imeanzisha mfumo wa kupokea malalamiko kwa njia ya simu (call center) ambapo mlalamikaji au mtoa taarifa anaweza kuwasilisha malalamiko kwa kupiga simu ya bure namba 0800111022.

Комментарии •