"Nilifuatiliwa Na Magari Mawili Mpaka Nyumbani | Walinishambulia Na SMG"

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 2 фев 2023
  • "Septemba 7, nimeondoka nyumbani nilikuwa Dodoma, kuna eneo linaitwa area D, kuna maghorofa mengi ndio wanakaa viongozi wa Serikali na yanalindwa muda wote nimeishi pale toka 2010. Nilifika Bungeni tukajadili na nilikuwa mtu wa mwisho kuzungumza katika ile session ya asubuhi.Nikatoka nje, nikampigia dereva wangu simu aje anichukue twende nyumbani tukale chakula cha mchana. Mimi siku zote nakula nyumbani.
    Ukiwa bungeni miaka ile njia rahisi ilikuwa inapita katikati ya uwanja wa ndege sasa ilikuwa njia imefungwa sababu palikuwa panafanyiwa matengenezo Kwahiyo ili uende area D inabidi uende mjini hivyo tukaelekea mjini. Tumepita round about ya Singida, tukapita round about ya barabara ya Arusha ambayo inapakana na uwanja wa ndege tulivyopita dereva akaniambia kuna magari mawili yanatufata nyuma kwenye akili yangu nikamuulizaDereva hawa polisi wanatufuatia nini? Maana mimi huwa nasumbuliwa na polisi.
    Tukafika area C tuko nao gari mbili land cruiser nyeupe na Mitsubishi tukaenda mpaka area D tumekaribia getini kama kuna mtu anafahamu iliko Club84 tulipopita pale Land cruiser nyeupe ikapaki pembeni Mitsubishi ikaja tukaingia nayo getini. Lile geti huwa linafungwa muda wote na huwa kuna walinzi wawili au watatu wanasilaha muda wote siku hii geti liko wazi na hakuna mlinzi tukapita tukaenda block E ninapoishi. Tukaingia parking bahati nzuri siku hiyo magari yalikuwa mengi na nafasi za parking zimechukuliwa imebaki moja kwa sababu niko mbele nikaingia kwenye hiyo parking.
    Wakaingia upande wa kushoto wanatafuta eneo la kupaki kuna magari, kulia kuna magari wakageuza gari kuelekea walipotokea dereva akaniambia nisishuke, wakasubiri na wao. Mmoja akatoka siti ya nyuma akaamia mbele upande wa abiria wakazungumza akarudi ndani akafunga mlango ghafla akafungua yeye, akafungua mwingine wanamashine hapo wakaachia" - Tundu Lissu
    #LiveOnClouds360

Комментарии • 536

  • @Maintenancetv971
    @Maintenancetv971 Год назад +38

    WANAOAMINI MUNGU YUPO WAGONGE LIKE HAPA ZA KUTOSHA TUMSHUKURU MUNGU PAMOJA.

  • @justinmazimba8335
    @justinmazimba8335 Год назад +32

    Like kwa lisu

  • @flavianimrod1017
    @flavianimrod1017 Год назад +20

    Huu ni muujiza unaoishi😭 Ila huyu Mungu jamani..wacha aitwe Mungu

  • @erastojackson9397
    @erastojackson9397 Год назад +2

    Nimependa watu wanavyo comment kumbe kunawatu wanahofu ya Mungu duniani endeleeni kumuombea maisha marefu Lisu, wale Akina Kangi ligola ambawo walikua Mambo ya ndani alikua akijibu maswali kwa kejeli wakati ule Mungu bado anashung'ulika nao Sasa aibu imewajaa walifikiri atakufa, naamini hawata sikia kifo Cha Lisu, Lisu ndiyo atashuhudia vifo vyao.

  • @EmmanuelKishiwa
    @EmmanuelKishiwa 3 месяца назад +3

    Daaah pole ndugu anguuu ujumbe wako apa umeniacha njia panda expressive feelings uloitoa hakika yake BWANA atalipia kisasi wala usiwe na shaka brother people's power we are together NCHI hii ya kwetu sote na tuijenge sote kwa amani

  • @hayeshimpeziy
    @hayeshimpeziy Год назад +40

    For the first time namsikiliza Mh. Lissu kwa makini, indeed kilichompata hakifai kumpata mtu yeyote yule na ninakilaani kitendo kile kwa roho yangu yote..Na mungu atakulipa kwa kadiri ya unyama uliotendewa. Pole sana Mh. Lissu.

    • @venancemwanya4212
      @venancemwanya4212 Год назад +3

      Aliefanya bila shaka atakuwa alishalipwa.

    • @kokombwana8625
      @kokombwana8625 Год назад +2

      @@venancemwanya4212 Hakika,huwezi ukafanya ubaya huu halafu poetic justice ikuache hivi hivi

    • @hayeshimpeziy
      @hayeshimpeziy Год назад +5

      @@venancemwanya4212 Mungu hawafanyi kazi yake kwa utashi wa kibinaadamu..kwetu wanaadamu mengi yamejificha sana, sisi hatupaswi kuhukumu lakini hukumu tumuachie yeye (Mungu)
      Aliefanya tukio hili inawezekana anasoma post hizi..Basi hakika mungu atakulipa kwa karidiri ya ubaya uliomtendea binaadamu huyu, kwani hakuna binaadamu anaepaswa kufanyiwa ubaya wa kiwango hiki bila ya hatia yoyote.

    • @samwelmtonyi8203
      @samwelmtonyi8203 Год назад

      Pole Mungu akupe maisha marefu

    • @zaherashamte1058
      @zaherashamte1058 Год назад

      @@kokombwana8625 jaman vimeanza tena

  • @ZeAniamalTV
    @ZeAniamalTV Год назад +3

    Hii nchi ilikua katika hali mbaya na kuongozwa na watu wasio na utu ila Mungu alijithibitisha ukuu wake hakika wote wanalipa sasa

  • @johnsinyinza7450
    @johnsinyinza7450 Год назад +3

    Mungu alijibu aliye watuma yuko wapi. Wamwogope mungu ipo siku watajulikana..usiuwe kwa upanga utakufa kwa upanga.

  • @paiwanjara3502
    @paiwanjara3502 Год назад +37

    Mungu ni wetu sote kama Mungu alipanga uwepo hakuna mwanadamu atakaye kuondoa katika maisha

  • @nsibwenekaswaga6267
    @nsibwenekaswaga6267 Год назад +6

    Bwana asipoulinda mji waulindao wakesha Bure! MUNGU ambariki sana Mh SAMIA SULUHU HASSAN kwa huruma zake.

  • @flova7022
    @flova7022 Год назад +12

    Aliyefanya unyama huu naamini Mungu ashamlipa kitaaaamboo xna

  • @lindambilinyi6253
    @lindambilinyi6253 Год назад +22

    Lisu umefanya nizid kukupenda wallah

  • @gadyjohn3815
    @gadyjohn3815 Год назад +33

    Ni mmojawapo kati ya watu waliokuombea sana na Mungu akatenda, Mungu ana kusudi na maisha yako, usirudi nyuma endelea kusimamia na kutetea haki.

    • @livinuskamugisha5296
      @livinuskamugisha5296 Год назад +1

      Haki ya ushoga ndo haki?

    • @gadyjohn3815
      @gadyjohn3815 Год назад

      @@livinuskamugisha5296 kwa hiyo ndiyo haki pekee uliyoona Lissu amewahi kutetea, huwa sipend kujibizana mitandaoni ila kuna muda inabid tu vijana wengi mnakurupuka muda mwingine inabid msaidiwe kueleimishwa, Lissu ameanza kufahamika kabla ya chadema kwa sababu ya misimamo yake na kutetea haki, amewatetea na kusaidia kushinda kesi nyingi sana za watu wanyonge wasio na uwezo ni hulka yake kutokukaa kimya haki isipotendeka, tatizo wengi wenu mmemjua baada ya chadema, tafuta kujua historia yake, mi sio chadema ila nakubali misimamo yake ndio maana nimemsihi aendelee kusimamia anachokiamini ni sahihi ambacho ni haki., akihama hapo sipo pamoja naye., mtizamo juu ya ushoga ni kitu kidogo sana hakitoshi kumjudge mtu., you think very low.

    • @thomastarimo
      @thomastarimo Год назад +1

      Mkono wa mungu ni mrefu sana

    • @musasabuu2808
      @musasabuu2808 9 месяцев назад

      ​@@livinuskamugisha5296punguza masiliko

  • @Oboss_billharvester
    @Oboss_billharvester Год назад +8

    Asante Mungu kwa kumlinda mtu huyu kwa ulinzi wako mtu huyu yupo hai, baba mwenye enzi simama nae na waliohusija na ugaidi huu wakaabike kwa matendo Yako makuu.

  • @emmanuelisarria6321
    @emmanuelisarria6321 Год назад +23

    Mungu ni mwem usiogope

  • @sanaanimaisha4072
    @sanaanimaisha4072 Год назад +22

    Pole sana kaka Lissu. Ule ni unyama na lazima kukemewa na kila mmoja wetu. Ubinadamu kwanza jamani

  • @deokibona2835
    @deokibona2835 Год назад +14

    Hili tukio liliniumiza sana sana. Yaani sitaki hata kulikumbuka. Pole sana Lissu.

    • @nayerabudebu5974
      @nayerabudebu5974 Год назад

      Yet mnasifu Magufuli alikuwa mwema

    • @deokibona2835
      @deokibona2835 Год назад

      @@nayerabudebu5974 sijawahi kumsifu Magufuli mie. Kilichonifanya nimpinge tangu mwanzo ni ukandamizaji aliokuwa anaufanya na kudhibiti vyombo vya Habari. Hakuna kiongozi mwema anayeweza kuvinyamazisha vyombo vya habari, ni fisadi peke yake ndio anaweza kifanya hivyo.

  • @marthasiliro6386
    @marthasiliro6386 Год назад +5

    Long live baba,Taifa hili linakuhitaji,MUNGU ana makusudi take juu Yako,na gumbo hili lina maana kubwa sana kwako.....!

  • @williamjames8190
    @williamjames8190 Год назад +8

    Mungu Ni Mwema Mh:Lissu Kama Ameweza Kukupitisha Katika Hili Basi Hakuna Wakukuteteresha Katika Hii Dunia

  • @baloziubalozini5074
    @baloziubalozini5074 Год назад +4

    Kwa Lissu it was a life changing moment,kwa mama as for now ni LIFE OPPORTUNITY ktk uwanja wa kisiasa

  • @ms_teeonly
    @ms_teeonly Год назад +6

    Pole sana Mungu ni mwema

    • @bellasi349
      @bellasi349 Год назад

      Pumbavu zako iki kijamaa kinatetea ushoga sibora ungekufa hizo hadisi zako zimepitwa n'a wakati n'a uo mwandishi jinga lingine izo habari nani hazijui kwani mpaka muweke iyo kipindi nyumbu wakubwa

    • @the_white_43.
      @the_white_43. Год назад

      @@bellasi349 wewe ni mkundu kama mikundu mingine,....Lissu hajawahi kutetea ushoga hizo siasa za maji taka peleka matakoni ...mkundu wewe ...
      mmekazana ushoga ushoga ushoga unatombwa nini /....

    • @the_white_43.
      @the_white_43. Год назад

      @@bellasi349 wewe ni kamkundu tu.

  • @malindimalindimerinyo1632
    @malindimalindimerinyo1632 Год назад +4

    Pole sana nafikiri waliotenda unyama huo nafikiri wanajutia Mungu ni mkubwa na waelewe hivo dunia hii si mali yetu ina mwenyewe udhalimu hautadumu na wanao shabikia udhalimu watajuta

  • @christopherobinya9874
    @christopherobinya9874 Год назад +14

    Watesi wako wapo mikononi Mwa Mungu yeye atalipa Kwa hayo mabaya. Na kamwe hawataishi maisha marefu watapita na wewe utabaki. Mungu ni mwema sana.

    • @thomastarimo
      @thomastarimo Год назад

      Kaka pole sana ila mungu ni mwema

  • @josephgregory9843
    @josephgregory9843 Год назад +33

    Mungu yu pamoja nawe mwamba utaishi sana

  • @christiannyamamba9089
    @christiannyamamba9089 Год назад +13

    Siasa yetu ilifika pabaya sana Mungu asimamie hili tuepukane na haya mambo

    • @daimavlog
      @daimavlog Год назад

      Mungu alisimamia mpendwa, akatufungia udikteta mapema

  • @robertzingu9889
    @robertzingu9889 Месяц назад

    Hakika Tundu Lissu ni mwanadamu wa pekee. Na wewe ni mwanaume. Pamoja na tukio hili baya kabisa kukutokea, lakini uko vilevile, huna ubaya na mtu. Tundu you're really very special person. God loves you very much. Mpe utukufu na heshima yeye peke yake

  • @jujajony905
    @jujajony905 Год назад +7

    Ni ngum ata kusikiliza, very emotion.

  • @mossesmuhanuzi5154
    @mossesmuhanuzi5154 Год назад +6

    Mungu atuepushe na mipango ya wanadamu

  • @faustaarobogast8978
    @faustaarobogast8978 Год назад +7

    Pole Sana baba lisu mungu Ni mwema

  • @amosmichael8986
    @amosmichael8986 Год назад +8

    Mungu atupe mwisho mwema

  • @shedracklyamuya9670
    @shedracklyamuya9670 Год назад +8

    Mungu anakupenda ❤️❤️

  • @stateofart1089
    @stateofart1089 Год назад +7

    Magufuli kafa Lissu mzima, Lowasa mzima acheni Mungu aitwe Mungu. Watanzania tuache upumbavu nchi yetu ni ya amani tuache uoga wapinzani wapo kwa ajili ya maendeleo ya nchi kama CCM wote ni wanasiasa na ni watanzania.Tujifunze kwa wamarekani leo upinzani kesho chama tawala wanabadilishana

    • @alfredmarti3131
      @alfredmarti3131 Год назад +2

      Sijui kama watakuelewa. Ni fact.

    • @stateofart1089
      @stateofart1089 Год назад +1

      @@alfredmarti3131 Bro wabongo Mungu aturehemu tu hakika nadhani bora kupaza mawazo yetu tu, ni wachache tunaelewana tuwaombee na wengine wengi wafungue macho yao na tuendelee kuipenda nchi yetu.

  • @joshuaswai8203
    @joshuaswai8203 Год назад +6

    Pole sana mzalendo Mungu ni juu ya yote Asante Yesu Mwokozi

  • @deusdedithjoseph7588
    @deusdedithjoseph7588 Год назад +9

    Mungu yupo pamoja na wewe mwamba

  • @KUBANDA53
    @KUBANDA53 Год назад +7

    Inasikitisha Sana, inaumiza Sana na inaudhunisha Sanaaaaa@Tundu lisu mungu akusimamie zaidiiiii wewe Ni super katika uongoz wako,,,, nakwenda singida kukupokea kaka

  • @abellabv
    @abellabv Год назад +11

    Mungu ni mwema sana. Wabarikiwe sana wote waliokusaidia.

  • @benedictomahendeka7156
    @benedictomahendeka7156 Год назад +3

    hakika Ukuu wa Mungu Ni wa ajabu sana GOD hatuna cha kukulipa ila tunasema asante sana kwa kuendelea kutuonyesha ukuu wako
    yaliyotabiriwa kwenye biblia hakika ndo yanayotokea
    eeeeeeh mwenyezi mungu nifundishe kunyamaza umetufundisha mengi sana kupiti LISSU

  • @mathewyoung2159
    @mathewyoung2159 Год назад +9

    Mungu ni mwema

  • @husseinkonz5192
    @husseinkonz5192 Год назад +10

    Hii inaitwa mungu mkubwa mshukuru mungu Mara zote tena

  • @princeriwa4000
    @princeriwa4000 Год назад +9

    Pole sana kamanda
    Malaika walinzi wakulinde na kukupa maisha matefu hapa duniani

  • @davidsilwamba2465
    @davidsilwamba2465 Год назад +7

    Pole Sana honourable lisu hakika mungu nimwenye rehema

  • @emmanicko1535
    @emmanicko1535 Год назад +10

    Inauma sana 😭😭 ila Mungu mwema kwakweli

  • @josephmakutano7067
    @josephmakutano7067 Год назад +3

    Unyama wabinadamu niwakipumbavu, kwasababu yakujisahau, maisha yabinadam nibahati tu kutoka kwamwenyezimungu, eemungu tusaidiye utuepushe napepo wabaya wanchihii

  • @dorisfabian4776
    @dorisfabian4776 Год назад +24

    Huyu baba ana maisha marefu sana..

    • @moodyzanzibar4336
      @moodyzanzibar4336 Год назад

      anaejua siri ya maisha marefu ya mjawake ni Mungu / Kuna watu wamepigwa mabomu hasa kenye vita ya kagera na pia wako hai sio yeye tuu

    • @moodyzanzibar4336
      @moodyzanzibar4336 Год назад

      NAHAKUNA MAISHA MAREFU KWA MJA NABII SULEIMAN AMEISHI ZAIDI YA MIAKA MIA NANE LAKINI ALIKUFA MUDA ULIPOFIKA SASA WEWE USITABIRI YA MUNGU

    • @dorisfabian4776
      @dorisfabian4776 Год назад

      @@moodyzanzibar4336 kwa kupigwa kule,kuvuja damu kule kumenifanya niamnini ataishi sana....

    • @dorisfabian4776
      @dorisfabian4776 Год назад +1

      @@moodyzanzibar4336 Na atakufa kwa wakati wa Mungu sio binadamu.

    • @mussakasela1937
      @mussakasela1937 Год назад

      Halafu hato kufo milele

  • @TheRonoTV2024
    @TheRonoTV2024 6 месяцев назад

    Kosa kubwa sana;Ukihisi au kuona inafuatwa na watu wasio julikana usielekee nyumbani au kokote unakoeenda maana unajiingiza mtegoni wanakokutaka maadui.
    Badilisha mkondo na uelekee kwa kasi kati nafasi yoyote ya umma
    mfano hospitali,duka kuu,kituo cha polisi etc.hapo utawanyima maadui nafasi ya kukushambulia faraghani.

  • @lindambilinyi6253
    @lindambilinyi6253 Год назад +7

    Dah story hii imeniumiza sanaa😭😭😭😭kwel Mungu akiamua kukupigania anakupigania kwel kwel,,kwel vita ya Mwanadamu mwachie Mungu,,Lisu Mungu amekuacha kwa sababu kubwa sanaa,,,aliyetaka ufe yy katangulia,sijui leo anajibu nn hko?Acha Mungu aitwe Mungu

  • @laurenceekway9451
    @laurenceekway9451 Год назад +3

    Pole mteule wa mungu Gina la mungu liimidiwe amemi

  • @abelianraphili5150
    @abelianraphili5150 Год назад +3

    Kazi ya Magufuli hiyo... Huyo Mshikaji wa kisukuma alikuwa mpumbavu sana

    • @dorisfabian4776
      @dorisfabian4776 Год назад +2

      Alikua na roho mbaya sana

    • @becare2300
      @becare2300 Год назад +2

      Nikweli magufuli alikuwa Ana mambo ya ajabuuu san

  • @mashauriobedi6290
    @mashauriobedi6290 Год назад +2

    Mungu Ndio mpangaji ila Si binadamu, Pole Sana Lissu kwa madhira hayo uliyopitia kwa kuwasemea wa Tanzania wanaojita machawa.

  • @drsumatz7539
    @drsumatz7539 Год назад +1

    Mh Lisu zidisha imani kwa Mungu na Hakika kupitia miujiza juu yabtukio hili tumejifunza Sana kuwa kumbe haya mambo sio historia tuuza kale ila tumeona miujiza na baadh wakalipwa ubaya huo na Mungu moja kwa moja

  • @pendaelimkumbo
    @pendaelimkumbo Год назад +6

    pole sana ila malipo ni hapa hapa duniani ..... mwache mungu aitwe mungu

  • @renatuswilson1577
    @renatuswilson1577 Год назад +7

    Polesana. Binadamu tunaunyama sana

  • @josephkulija293
    @josephkulija293 Год назад +2

    Acha Mungu aitwe Mungu. Jina la Mungu lihimidiwe.

  • @jonathanmnyone4003
    @jonathanmnyone4003 Год назад +1

    Kuna kazi bado hujaifanya hapa duniani -Tanzania Mungu anataka uifanye. Vinginevyo angeruhusu uondoke. Msikilize Mungu atakueleza cha kuifanyia hii nchi.

  • @asnathmasegenya9890
    @asnathmasegenya9890 Год назад +4

    Pole sana storyimeniumiza mno

  • @festohaule9716
    @festohaule9716 Год назад +1

    Amini usiamini Mungu yupo..pole lisu pole chadema.. pole Demokrasia!!!!!?

  • @danielmatya373
    @danielmatya373 Год назад +1

    Mungu Mkali Kafa yeye kamuacha mwamba bdo anahema Glory to God

  • @RosemaryNjiku
    @RosemaryNjiku 7 дней назад

    Mhe. Tundu lissu mungu atakulipia Kwa yote waliokufanyia

  • @farajasallah2338
    @farajasallah2338 Год назад +6

    Pole Sana jamani, niliumia mnoo, karibu Tz kazi iendelee

  • @kassim1262
    @kassim1262 Год назад +1

    Ukiona mtu anapingana na tundu lissu kwanza huyo nimiongoni mwawatu wasiojuilikana wauwaji ambao hawana utu wapo tayari kuua kwakisingizio chamaendeleo kibaya zaidi hata mipango yamungu hawaiyamini manaake wanajua tundu lissu kapigwa risasi nyengi tu lakin kwamipango tu yamungu bado anaishi lakin watu wasiojuilikana bado wanapinga mipango yamungu wanaanza kujuilikna mitandaoni watu hatari sana kwataifa

  • @glorysungura3180
    @glorysungura3180 Год назад

    Pole sana, jina la BWANA LIBARIKIWE. MUNGU NI MWEMA SANA. Kama siku za kuondoka duniani bado zipo, utapona tu hata iweje. Dah, moyo umeniuma sana. Nasikia maumivu makali moyoni mwangu. Jipe moyo mpendwa, KISASI NI CHA BWANA. MWACHIE MUNGU HAKIMU WA HAKI, YEYE HAPOKEI RUSHWA. ATAHUKUMU TU IPO SIKU.

  • @remmyalfred6736
    @remmyalfred6736 Год назад

    Pole sana. Mungu azidi kukutetea Mungu amewaokoa na akampa hekima dereva kufanya alichofanya. Utukufu Kwa Mungu,

  • @danielmushi5755
    @danielmushi5755 Год назад +12

    Pole sana Lissu,Mungu ni mwema wakati wote.🙏🙏

  • @ngowestanley2535
    @ngowestanley2535 Год назад +5

    Mungu mwema cku zote

  • @khadijaomary9324
    @khadijaomary9324 Год назад

    Kiongozi hongera hakika unapamba juu ya chama na mungu akuongezee baraka tele wanyooshe unajuwa serikali hii imejaa mafisadi weng Sana rushwa Kama zote adi tulishaachoka

  • @meggygitau4079
    @meggygitau4079 Год назад +11

    Mungu ni Mungu na maajabu yake jamani 🙏

  • @yahyashaib5116
    @yahyashaib5116 Год назад +2

    Allah nimwema sn pole sana

  • @edmundrutahiwa
    @edmundrutahiwa Год назад

    Different days months and years but same story...kupigwaa risasi kupigwaa risasi mzee tushajuaa tushakuombea na thanks umerudi bongo salama...weka sera mezani sasa na acha kutafuta huruma...kura hupati kwa kuonewaa huruma kura unapata kwa nn utafanyaa au nn umefanya

  • @aishaswalehe6848
    @aishaswalehe6848 Год назад +1

    Mungu yupo kamanda tunazidi kukuombea 🙏🏾🙏🏾

  • @KUBANDA53
    @KUBANDA53 Год назад +2

    Pole Sana kaka machoz yamenitoka walai,

  • @renatusdeogratias2108
    @renatusdeogratias2108 Год назад +6

    Lissu pole sana machozi yananitoka

  • @erastomadary2891
    @erastomadary2891 Год назад +5

    Mungu mkubwa hiyo siku hata chakula kilikuwa haliki

  • @mahmoudukusso4488
    @mahmoudukusso4488 Год назад +2

    Pole sana Comrade

  • @nelsonsape2809
    @nelsonsape2809 Год назад +2

    Pole sana...

  • @ludatoke2451
    @ludatoke2451 Год назад +1

    Pole sana kamanda tuvushe lisu CCM wameshachoka

  • @lucaskuseroi119
    @lucaskuseroi119 Год назад +1

    Kweli mshukuru mungu alikulinda Kwa bidii Mrs

  • @danielntengwi7699
    @danielntengwi7699 Год назад +2

    Pole sana Tundu .

  • @esterpius7423
    @esterpius7423 Год назад +2

    Mungu atukuzwe na aendelee kukutunza. Waliofanya hicho kitendo Mungu ahusike nao

  • @FaustinaWarioba-zq2tx
    @FaustinaWarioba-zq2tx 9 месяцев назад

    Mbeee! Mungu anajua kuhuisha uhai wake....

  • @obedwilliam5906
    @obedwilliam5906 Год назад +1

    Vibaraka wa ccm hao ila mungu ni mwema malipo ni hapa hapa dunian pole sana Mr lisu

  • @mwl.frankmadembo7472
    @mwl.frankmadembo7472 Год назад +14

    Mungu amekusaidia tafsiri yake Kuna mask mbele. Jipange lakini tengeneza mahusiano Yako na Mungu

    • @margarethpolepole7438
      @margarethpolepole7438 Год назад +1

      Huyo hana mahusiano na mungu katawaliwa na matusi na kumkashifu mwendazake magufuli na marais wengine hauwezekani kila Rais mbaya yeye nani anatumiwa huyo

    • @rogathesarwatt
      @rogathesarwatt Год назад

      We imekuaje kuwa hana mahusiano na Mungu

    • @ezekieljacob5795
      @ezekieljacob5795 Год назад +1

      Huyu ni mteule tayari..na nchi tutajiuliza wakati wake ukifika,atafanya mambo mengi ya kuishangaza dunia .God I hope it will be soon.niliomba sana upone,sasa naomba tena

  • @geoffreykilawe3953
    @geoffreykilawe3953 Год назад

    Mungu anakupenda sana Tundulisu, azidi kukutunza. Tunatamani urudi bungeni mwaka 2025.

  • @Filexwawa
    @Filexwawa Год назад +3

    Pole sana

  • @opiyowilson3640
    @opiyowilson3640 Год назад +7

    God is OMNIPRESENT.

  • @josephmkinga9509
    @josephmkinga9509 Год назад +6

    LISSU hilo tukio lilikua baya sana hua anaongea kwa uchungu mpaka wengne wanalia MUNGU akusimamie akupe nguvu akulinde Sana kama alivokupingania kwenye uhai wako

  • @mumbesophia-jd3lt
    @mumbesophia-jd3lt Год назад

    Daa pole sana mungu yupo nawe

  • @samsonsakwa-sg4du
    @samsonsakwa-sg4du 7 месяцев назад

    Pole sana umenitoa machoz umepita magumu sana

  • @eliasthomas1547
    @eliasthomas1547 4 месяца назад

    Mungu nimwema.

  • @vicentsalum4884
    @vicentsalum4884 Год назад +2

    Mungu azidi kukutia nguvu Mh. Tundu Lissu

  • @maxcharles5436
    @maxcharles5436 Год назад +3

    mungu mkubwa sasa aliye fanya ivo yy yupo wap

  • @mussaandrew2083
    @mussaandrew2083 Год назад

    Pole sana kiongozi

  • @marthamtalo4348
    @marthamtalo4348 4 месяца назад

    Mungu anajua ndie mwamuzi

  • @faustinebahenobi3412
    @faustinebahenobi3412 Год назад

    Duhuuuuu akia mungu mwendazake attopokelewa mbinguni kamwe muuaji yule

  • @user-qi8ct9zk2h
    @user-qi8ct9zk2h 28 дней назад

    Napenda lisu mno❤🎉

  • @ramadhanimtambo6755
    @ramadhanimtambo6755 Год назад

    Hapa tutayasikia mengi huyu mh nadhani mungu alimuweka makusudi Ili tujue maovu yaliyofanywa .

  • @BONGOINMOTION
    @BONGOINMOTION Год назад

    Pole sana mr

  • @davidelisha4455
    @davidelisha4455 Год назад +2

    Pole Sana baba Mungu yupo pamja nawe

    • @ngasarichard1443
      @ngasarichard1443 Год назад

      Mungu akusaidia walio panga kukuua mungu atakuja kuwafanyia kibaya nawao zaidi yahicho walicho kufanyia mwamba

  • @wilfredjohn4829
    @wilfredjohn4829 Год назад +4

    Kuna muda nasema MUNGU YUPO NAWE HAKIKA..

  • @eddiemohamed9003
    @eddiemohamed9003 Год назад

    GOD BLESS YOU

  • @ibrahimmwanza6162
    @ibrahimmwanza6162 Год назад +1

    Mungu yupo