Dalili za kimbunga ukiwa baharini, mvuvi asimulia yaliyomkuta

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 3 май 2024
  • Dalili za kimbunga ukiwa baharini, mvuvi asimulia yaliyomkuta
    Mikoa ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi kwa saa 24 sasa, ipo kwenye kufuatilia kuhusu mwenendo wa Kimbunga Hidaya.
    Mwananchi imezungumza na mvuvi Ali Ramadhani (70) mkazi wa Tanga ambaye anaeleza amefanya shughuli za uvuvi tangu akiwa na miaka minane na baba yake mzazi mpaka leo hii.
    Anaeleza kuwa alishawahi kukutana na kimbunga akiwa baharini kwenye shughuli za uvuvi na wenzake watatu, kabla hakijawakuta na kusomba mtumbwi wao,kuna dalili waliziona na baadae dhoruba kutokea.
    Mfanyabiashara wa mkaa, Idd Omary aliyekuwa anafanyabiashara kutoka Bagamoyo kwenda Zanzibar, amesema alikutana na dhoruba na walikuwa wawili wakielekea Pemba na magunia ya mkaa majira ya asubuhi.
    Mwenyekiti wa Mazingira Soko la Deep Sea jijini Tanga Hamisi Said amesema wavuvi wachache wameingia baharini, lakini walioingia wapo kwenye tahadhari zote ikiwamo kuwa na makoti maalumu ya kuvaa endapo itatokea dhoruba yoyote wakati wakiwa kazini kwenye uvuvi.
    Mfanyabiashara Soko la Samaki Deep Sea, Salehe Jumanne amesema mpaka sasa upatikanaji samaki umeshuka kutokana na wavuvi wengi kuogopa kwenda baharini,hali ambayo imefanya hata bei ya samaki kupanda.

Комментарии • 3

  • @user-od2mc4mj4e
    @user-od2mc4mj4e 21 день назад

    Du n hatari

  • @andrewemanuel2213
    @andrewemanuel2213 20 дней назад

    Mi najua mxoke ni hatali niliwai kuona ulianguka kwenye maji ni hatali ila wavuvi wanajua kuvitegua

  • @musamwapinga361
    @musamwapinga361 21 день назад

    HUKU KWETU KUNA KIMBUNGA MASUMBUKO😂