HII NI AIBU KUBWA/WAZIRI BASHUNGWA AKUTANA NA MAUZA UZA HAYA MAZITO/MOTO WAMUWAKIA MKANDARASI HUYU

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 24 янв 2024
  • Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameagiza kuondolewa kwa Mhandisi Mshauri LEA Associaties anayesimamia ujenzi wa barabara ya Kitai - Lituhi sehemu ya Amani Makoro-Ruanda (km 35) kwa kiwango cha lami na kuutaka Wakala wa Barabara (TANROADS) kuendelea kusimamia ujenzi huo ili uweze kukamilika.
    Pia, ameagiza Mkandarasi anayejenga barabara hiyo China Railway Seventh Group kutopewa miradi mipya mpaka hapo atakapokamilisha miradi aliyopewa katika mkoa wa Mara, Katavi ambayo nayo inaonekana kusuasua.
    Bashungwa ametoa agizo hilo leo tarehe 25 Januari 2024 wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma wakati akikagua ujenzi wa barabara hiyo ambapo hajaridhishwa na utekelezaji wake ambao umechelewa kwa asilimia 75 na kusisitiza hatua za kimkataba zichukuliwe dhidi ya Mhandisi Mshauri huyo.
    “Nimuagize Katibu Mkuu kuangalia hatua za kimkataba mnazotakiwa kumchukulia haraka Mhandisi Mshauri kwasababu ameshindwa kumsimamia Mkandarasi kukamilisha mradi huu kwa wakati”,amesisitiza Waziri Bashungwa.
    Bashungwa amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alishatoa Bilioni 6.9 ambayo imekamilisha kipande cha kwanza cha kilometa 5 kutoka Kitai hadi Amani Makoro na Bilioni 60 kwa ajili ya muendelezo wa barabara hiyo sehemu ya Amani Makoro - Ruanda.
    “Kiasi cha Shilingi Bilioni 155 zimetengwa ajili ya mradi mzima wa ujenzi wa barabara kuanzia Kitai - Lihuli - Bandari ya Ndumbi”, amefafanua Bashungwa.
    Bashungwa ameagiza TANROADS kutoendelea kulimbikiza miradi kwa Wakandarasi kwani ndiyo inafanya miradi mingi kuchelewa na mingine ikiwa ya kimkakati na kiuchumi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
    Akitoa taarifa ya mradi, Kaimu Mkurugenzi wa Miradi kutoka TANROADS, Mhandisi Jephason Nko, amesema kuwa maendeleo ya mradi huo mpaka sasa umefikia asilimia 25 ikilinganishwa na asilimia 100 ambapo mradi huo ulitakiwa kukamilika Disemba, 2023.
    Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma , Kanali Labani Thomas, amesema kuwa Mchuchuma na Liganga wanaitegemea barabara hii kwani ndio barabara muhimu na ni kiunganishi cha kutoka Mkoa wa Ruvuma kupitia Nyasa kwenda mkoani Njombe kupitia Ludewa.
    Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Ruvuma, Komred Oddo Mwisho, amesema kuwa barabara hiyo ni kiungo muhimu kati ya Wilaya ya Nyasa-Mbinga kwani ndipo uchimbaji mkubwa wa makaa ya mawe yanapofanyika na kwa siku takribani magari 400 hadi 500 yanapita katika barabara hiyo kuyasafirisha kuelekea maeneo mbalimbali.
    Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini, Mhe. Benaya kapinga, amesema kuwa kilio kikubwa cha Wananchi wa Amani - makoro hadi Ruanda ni kupata barabara kwa kiwango cha lami ili kuchochea maendeleo ya wananchi.
    Waziri Bashungwa yupo mkoani Ruvuma katika ziara yake ya kikazi ambapo atakagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara na madaraja.

Комментарии • 46

  • @onesmomhagama7519
    @onesmomhagama7519 2 месяца назад

    Wapi hapo

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  2 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @hassanmwallimu5767
    @hassanmwallimu5767 3 месяца назад +1

    Hakuna chochote hapo watu wameshachukua percent zao

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  3 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @mohamoudhussein4570
    @mohamoudhussein4570 4 месяца назад +1

    Munawapa Wachina Kazi baada ya Kuwezesha Wakandarasi wa Kwetu sisi wenyeww

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  4 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @saynabmohammed6263
    @saynabmohammed6263 Месяц назад

    Wanini kuwaendeleza wawanyang,abye wapewe wengine hiyo walojenga wafanye hesabu wakatiane

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  Месяц назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @mohamoudhussein4570
    @mohamoudhussein4570 4 месяца назад +1

    Mnaishia Maigizo tu

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  4 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @salummpango5250
    @salummpango5250 2 месяца назад

    Kama utamsaidia rais hivyo! Hiyo wizara inakufaa mheshimiwa waziri!! Ongera!!

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  2 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @emmanuelmlowe-ew7gx
    @emmanuelmlowe-ew7gx 3 месяца назад

    Makonda hoyeeee anaamsha watendaji sasa tunawaona wanafanya kazi

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  3 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @felicianndunguru5353
    @felicianndunguru5353 4 месяца назад

    Alishatoka ulinzi yupo ujenzi na hii itakuwa ya leo maana kaingia Songea jana

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  4 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @saynabmohammed6263
    @saynabmohammed6263 Месяц назад

    Mtoe wapen wengine

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  Месяц назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @saynabmohammed6263
    @saynabmohammed6263 Месяц назад

    Mbona barsbara hazina mitaro kuzuia mmomonyoko
    Na maji chafu

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  Месяц назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @mohamoudhussein4570
    @mohamoudhussein4570 4 месяца назад

    Hakuna Nchi iliendelea kwa kutegemea Wakandarasi kutoka Nje

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  4 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @estheroscar6520
    @estheroscar6520 4 месяца назад

    Ila mimi nawapongeza wachina kwa madaraja tu wapo vzr

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  4 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @user-dk5kk4rf3v
    @user-dk5kk4rf3v 3 месяца назад

    Kingereza cha kufikiria aibu mno..

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  3 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @emmanuelmlowe-ew7gx
    @emmanuelmlowe-ew7gx 3 месяца назад

    Sasa naona nguvu ya magufuli inakuja.

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  3 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @hassanmwallimu5767
    @hassanmwallimu5767 3 месяца назад

    Kuna watu watanzania nyuma yake

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  3 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @user-dk5kk4rf3v
    @user-dk5kk4rf3v 3 месяца назад

    Nyie ni kuiba na kumtaja mama

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  3 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @fahadfaraj6474
    @fahadfaraj6474 4 месяца назад

    Hii ni ya lini ? Maana huyu ni waziri wa ulinzi sasa sa hayo mambo ya barabara vp

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  4 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia Ila Kwa Sasa Huyu Ni Waziri Wa Ujenzi

  • @omarybakunda2554
    @omarybakunda2554 4 месяца назад

    Wachina ni wachapa kazi waje wengi.

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  4 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @hassanmwallimu5767
    @hassanmwallimu5767 3 месяца назад

    Rushwa imejaa na watu wenu mnaowapa kazi je mmewachukulia hatua gani hao watendaji wenu? Lakini ingekua mtu kashikwa na nyama ya porini mngemfunga miaka 100

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  3 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @zobakazizi7637
    @zobakazizi7637 4 месяца назад

    Shida ni watu wetuuu

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  4 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @user-fk4st8qj2k
    @user-fk4st8qj2k 4 месяца назад

    Bashungwa wewe ni jembe, isaidie nchi ktk wizara hiyo uliyopewa.

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  4 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @user-fk4st8qj2k
    @user-fk4st8qj2k 4 месяца назад

    Bashungwa wewe jembe.Isaidie nchi tupare maendeleo.

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  4 месяца назад

      Asante Kwa Kutufuatilia

  • @kisumouongo2paul123
    @kisumouongo2paul123 Месяц назад

    Kati ya mawaziri 4 ninao wakubali wewe nimmoja wao

    • @ICONTVTZ
      @ICONTVTZ  Месяц назад

      Asante Kwa Kutufuatilia