Hospitali ya Bugando kukusanya Sh1 bilioni za matibabu ya saratani kwa watoto

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 3 май 2024
  • Mwanza. Hospitali ya Rufaa Kanda ya Bugando (BMC) inatarajia kukusanya zaidi ya Sh1 bilioni kwa ajili ya kuwezesha matibabu ya saratani kwa watoto 500.
    Akizungumza leo Mei 4, 2024 wakati wa uzinduzi wa mbio za Bugando Health Marathon 2024 zinazolenga kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwezesha matibabu hayo, Daktari bingwa mbobezi wa magonjwa ya saratani ya watoto, Heronima Kashaigili amesema mbali na kupata msaada wa fedha za matibabu kutoka serikalini na kwa wadau, hazitoshi kutokana na idadi kubwa ya watoto wenye saratani.
    "Mwaka 2009 tulianza kuona watoto 50 na ufanisi wake kutibu ulikuwa chini ya asilimia 20 ina maana karibu asilimia 35 ya watoto walikuwa wanakufa lakini hadi kufikia mwaka 2023 tunaweza kuona watoto 300 na tumefikia zaidi ya asilimia 50 ya kuweza kutibu watoto hao," amesem

Комментарии •