Ripoti Maalumu|| Vivuko Kigamboni, Bomu linalosubiri kuingiza nchi kwenye maafa

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 25 май 2024
  • Usalama wa zaidi ya watu 60,000 wanaotumia huduma ya vivuko kuvuka Kigamboni na Magogoni kila siku upo katika mashaka.
    Mashaka ya usalama wa watu hao, yanatokana na ubovu wa vivuko hivyo, unaosababishwa na kutofanyiwa matengenezo makubwa kwa mujibu wa sheria, ratiba na matakwa ya kitaalamu.
    Hali hiyo inazua hofu ya kuharibika kwa vivuko hivyo vikiwa safarini, kama ilivyowahi kutokea mara kadhaa vyombo hivyo vya usafiri wa majini vilipozima vikiwa na abiria katikati ya maji.
    Kwa mujibu wa taarifa ya Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), kwa siku ni zaidi ya abiria 60,000 wanaohudumiwa katika vivuko vya Magogoni-Kigamboni.
    Uchunguzi wa Gazeti la Mwananchi, umebaini vivuko hivyo aghalabu hupitiliza muda wa matengenezo makubwa, ambayo ndiyo msingi wa uhai na ufanisi wake.
    Soma kwa undani kupitia www.mwananchi.co.tz

Комментарии • 9