Mbowe atoa tamko kuhusu sakata la yeye na Lissu asema 'watu wanasema' ...

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 16 июн 2024
  • Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe, amesema hawezi kugombana na makamu mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu kama baadhi ya watu wanavyodai.
    Amesema ili kudhihirisha hilo, katika operesheni GF ya majimbo 30 atakayoifanya wilayani Karatu, Juni 22, 2024 kwa kutumia chopa, ataongozana na Lissu.
    Aidha amesema wanaosubiri Chadema ipasuke, watasubiri sana na kuwa wanaofikiri hivyo wanapoteza muda wao, labda kinaweza kufa akifa yeye.
    Mbowe amesema hayo jana Juni 16, 2024, wakati akiongoza kikao cha mashauriano ya mkoa ya chama hicho.
    Amesema kuna baadhi ya watu wanasema anagombana na Lissu, jambo alolikanusha kwa kusema hawezi kugombana naye wala kuwa na chuki za milele na yeyote yule ndani ya chama hicho.
    “Unajua kuna watu wanasema ooh Mbowe na Lisu wanagombana, niwaambie mimi na Lisu yule ni makamu wangu mimi ni mwenyekiti, siwezi kugombana na makamu wangu kama nilivyosema siwezi kugombana na kuwa na chuki za milele na yoyote ndani ya chama hiki," amesema.

Комментарии • 3