Wanaomaliza mafunzo JKT waomba serikali kuwatafutia ajira

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 3 май 2024
  • Vijana waliohitimu mafunzo ya kijeshi kutoka kikosi cha 835 Mgambo JKT cha wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga,wameuomba uongozi wa jeshi kwa kushirikiana na serikali,kuangalia uwezekano wa kuwapatia ajira wanapohitimu mafunzo yao.
    Ombi hilo wamelitoa kwenye sherehe za mahafali yao ya kuhitimu mafunzo ya miezi minne,katika kikosi cha 835 JKT Mgambo iliyofanyika na kusema kuwa wengi wao,wanapohitimu mafunzo wanakuwa wamekamilika kimafunzo,hivyo uongozi wa jeshi kwa kushirikiana na serikali waangalie ni jinsi gani wataweza kupatia ajira.
    Akifikisha ujumbe huo kwa njia ya mashairi,mhitimu wa mafunzo Abdul Kareem amesema moja ya kilio cha wahitimu wengi wanaopata mafunzo ya JKT ni kupata ajira,ili kuweza kuendeleza walichojifunza,kwani wengine wakirudi nyumbani hakuna kinachoendelea.
    Brigedia Jenerali Abubakar Charo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania,(JWTZ) amesema wanafahamu kuhusu uwepo wa kilio cha wahitimu hao kuomba ajira,ila amewatoa wasi wasi kuwa serikali inaangalia jinsi ya kuwatumia.
    Akifunga mafunzo hayo mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Handeni Albert Msando amewataka viongozi wa halmashauri na ofisi nyingine za serikali,kuwatumia vijana hao kwenye shughuli mbalimbali kwani ni weledi,na wanaweza kufanyakazi bila kusukumwa kutokana na mafunzo waliopata.
    Awali mkuu wa kambi ya Mgambo JKT Raymond Mwanri amesema vijana hao wamefundishwa uaminifu,utii na uhodari wa kuweza kutimiza majukumu yao,ikiwa suala la uzalendo kwa taifa lao na wamefaulu vizuri mafunzo yao.
    (Imeandikwa na Rajabu Athumani)

Комментарии • 2

  • @topfreelancer5151
    @topfreelancer5151 22 дня назад

    Wanajeshi kutoa ujumbe kwa namna hio (shairi) si ni ishara ya kuwa dhaifu? 😂

    • @NicolausMufuruki
      @NicolausMufuruki 22 дня назад

      Jeshini kuna masomo ya utamaduni kwa hiyo uwasilishaji wa changamoto zao kwa njia hiyo si shida kiongozi