ALIYEKAA NA UVIMBE KILO TANO TUMBONI MIAKA 10 ASIMULIA MAZITO, WATAALAMU WAFUNGUKA....

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 2 май 2024
  • Nimezaa watoto 11 lakini mtoto wangu wa mwisho niliyemzaa mwaka 2010 nilikuwa nipoteze maisha, maana nilitokwa na damu nyingi sana, nikazimia mara tatu na wakati wote wa mimba damu ilikuwa inavuja, sikujua tatizo.”
    Haya ni maneno ya Eveline Paulo, mkazi wa Biharamulo mkoani Kagera aliyetolewa uvimbe wenye uzito wa kilo tano tumboni.
    Uvimbe huo alioishi nao kwa miaka 10 bila matibabu, ulikuwa umekaa nje ya kizazi.
    Akizungumza na Mwananchi, akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Geita baada ya kufanyiwa upasuaji, Eveline amesema tumbo lake lilikuwa limejaa na alihangaika kwenda hospitali mbalimbali lakini hakupata huduma kutokana na kusumbuliwa na shinikizo la damu.
    “Nimehangaika kwenda hospitali huko Biharamulo na Mwanza, lakini kila wakitaka kunihudumia presha inapanda, narudishwa nyumbani, mwisho nikaamua kuishi na hali hiyo hadi nikaona kawaida, lakini nilikuwa nateseka sana,” amesema mama huyo.
    Hata hivyo, amesema hivi karibuni alienda kumtembelea mwanawe aishie Geita na akamsimulia tatizo lake na mwanawe akaamua kumpeleka hospitali kwa matibabu zaidi na baada ya vipimo kuonyesha uvimbe alikokuwa nao tumboni ni mkubwa, madaktari wakaelekeza afanyiwe upasuaji kuuondoa.
    Akizungumzia upasuaji huo uliochukua saa mbili na nusu, Dk Isaack Ajee, bingwa wa magonjwa ya wanawake ameasema uvimbe aliokuwa nao Paulo ulikuwa wa sentimita 38 na kama ingekuwa ni mimba, ni sawa na ya miezi tisa.
    Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi
    (Imeandikwa na Rehema Matowo)

Комментарии •