Kijana ajirusha kwenye kivuko cha watembea kwa miguu, kisa wivu wa mapenzi

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 6 май 2024
  • Mkazi wa Kijiji cha Kemakolele Kata ya Nyarero Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara, Mwikwabe Range (20) amejaribu kujiua kwa kujitupa chini kutoka kutoka juu ya kivuko cha watembea kwa miguu, kilichopo Mabatini jijini Mwanza kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.
    Tukio hilo limetokea Mei 3, 2024 majira ya saa 11 jioni katika kivuko kinachosaidia waenda kwa miguu kuvuka Barabara ya Mwanza - Musoma eneo la Mabatini, chenye urefu wa mita 5.5.
    Hata hivyo kijana huyo aliokolewa na wananchi na kuwahishwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure ambapo amelazwa kwa ajili ya matibabu.
    Akizungumza kwa njia ya simu jana Mei 6, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema kijana huyo amechukua maamuzi hayo baada ya mpenzi wake ambaye anadai amemsomesha kumkuta akiwa na mtoto baada ya kuolewa na mwanaume mwingine.
    Mashuhuda wa tukio hilo wamedai kabla ya kujirusha kijana huyo alionekana kwenye daraja hilo akiandika kitu kwenye daftari na baadaye kusali mara tatu na daftari likiwekwa mfukoni.
    Kufuatia hatua hiyo, Mwanasaikolojia na Mshauri Nasaha katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi Shirikishi Bugando (Cuhas), Paul Masele amewasihi vijana kuacha tabia ya kusomesha wapenzi wao kwa kuwa hilo ni jukumu la wazazi wao.

Комментарии • 31

  • @danieldanielwangwe7274
    @danieldanielwangwe7274 Месяц назад +1

    Wanawake mhhhhh

  • @abbyjma7355
    @abbyjma7355 Месяц назад +3

    Wenzie wanajirusha kwenye halkopta kikomando yeye anajilrusha kisa mapenz

  • @martinchambala9399
    @martinchambala9399 Месяц назад +2

    Wanawake ni wakuogopa sana tuwaepuke kuwaamini kwa %100 hawa watakuja kutuua kizembe

  • @AminaLibisa
    @AminaLibisa Месяц назад +1

    Mimi mwanangu namwambia kila.siku usithubutu kumwendeleza mwanamke ukitaka muoe mjijenge tu maisha yaendelee maana unaweza kujiua so mapenzi ni gharama unaziwazia

  • @christainc.5217
    @christainc.5217 Месяц назад

    Mungu amuwekeye wepesi apone😢😢masikini

  • @psgospel3490
    @psgospel3490 Месяц назад

    Mbaya sana hii

  • @AmedeusMbanda-gh4rj
    @AmedeusMbanda-gh4rj Месяц назад

    Jamani,🙆🙆

  • @VailethManyanda
    @VailethManyanda Месяц назад

    Jamani,wabongo😂🤦‍♀️🧟‍♀️🙌🏿🤲😂

  • @sskondopoleani9616
    @sskondopoleani9616 Месяц назад +2

    Mtu kama hayo akipona mpeni sumu ya panya....

  • @yukundapeter8200
    @yukundapeter8200 Месяц назад +1

    Miaka 20 angetakiawa chuo.Akome

  • @MbatiaZakaria-ti5kt
    @MbatiaZakaria-ti5kt Месяц назад

    Alikosea kwenda kujirusha kwenye daraja angetumia sumu ya panya ata asinge wasumbua watu

  • @user-oo1vz3zi1t
    @user-oo1vz3zi1t Месяц назад +1

    Bado mudogo hvi siutampata tu mengine usirudie tena

  • @LizenMaker
    @LizenMaker Месяц назад

    Mwanamke Kama hakutaki tafuta mwingine wapo wengi acha ujinga dogo

  • @hollymore4904
    @hollymore4904 Месяц назад

    Alkua anataka ajivunje sio ajiue.. mitq 5?? 😃 Kwan Mwanza hakuna miti mirefu?

  • @omarybakunda2554
    @omarybakunda2554 Месяц назад

    Mleteni kwangu nimgonge ngumi za usoni.

  • @NeemaSamson-ti8pc
    @NeemaSamson-ti8pc Месяц назад

    Kumsomesha mwanamke au mwanaume ni ujinga alivyosomeshwa na wazazi wake inatosha

  • @naturelle1097
    @naturelle1097 Месяц назад

    Huyo mwanamkempuuzi

  • @marasimarasi6139
    @marasimarasi6139 Месяц назад

    baadhi ya wanawake ni mashetani

  • @NeemaSamson-ti8pc
    @NeemaSamson-ti8pc Месяц назад

    Upumbavu tu huo kujitia ulemavu bure

  • @nathanlusulo-po2lj
    @nathanlusulo-po2lj Месяц назад

    Angepanda ghorofa ya bugando akaruka hapo ni pafupi

  • @SaimoniCharles-qm5bz
    @SaimoniCharles-qm5bz Месяц назад

    Elewa mzungu akikwsmbia anakuonda anamanisha ila mbongo akikwambia anakupnda pita kushoto

    • @stanleybupambambogo3334
      @stanleybupambambogo3334 Месяц назад

      Eeh! Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa...? Ni nani alikwambia kuhusu hiyo dhana uliyo nayo kuhusu eti mzungu akisema anakupenda eti anamaanisha...???!!!

  • @FredMwamgogwa-td6ni
    @FredMwamgogwa-td6ni Месяц назад +1

    Mjinga huyo angekufa tuu

    • @eggysulle7988
      @eggysulle7988 Месяц назад

      Wala s mjinga kwa sababu s ww ,muombe Mungu akuepushe

  • @musampanda3643
    @musampanda3643 Месяц назад +1

    Sasa hapo krb hivi atakufaje

  • @user-wj6zj1ly4e
    @user-wj6zj1ly4e Месяц назад +3

    Kwanza kijana umri mdgo kweli miaka 20 alikuwa akipata wap pesa za kusomesha mchumba? Pili mtu akijinyonga au kunywa sumu akipona huwa anafunguliwa mashitaka ata huyu naomba akamatwe

    • @israelkisaila8401
      @israelkisaila8401 Месяц назад

      Wengine wanatoka familia za kishuwa ndugu,mbilioni kwao siyo tabu zao,wewe kama uko na 40yrs na huna pesa,pole, wenzio wamezaliwa kwa pesa na watakufa kwa pesa.😂😂😂

    • @bilid4128
      @bilid4128 Месяц назад +2

      Ukisikiliza hapo wanasema aliuza shamba ili akasomeshe mpenzi wake.

  • @ElishaSolomoni-kc4zk
    @ElishaSolomoni-kc4zk Месяц назад

    KUMEKUCHA XX