TIMU YA WATUMISHI CHUNYA YAENDELEA KUJIMARISHA TAYARI KUSHIRIKI SHIMISEMITA 2024

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 5 июл 2024
  • Timu ya mpira wa miguu ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya imeshika nafasi ya pili kwenye bonanza la michezo lilofanyika uwanja wa Sokoine ambapo katika michezo mitatu iliyochezwa Chunya imeshinda mchezo mmoja, imedroo mchezo mmoja na imefungwa mchezo mmoja hivyo kuwa na jumla ya pointi nne n imeshika nafasi ya pili ikitanguliwa na RAS yenye pointi saba
    Bonanza hili limeshirikisha timu nne ambazo ni RAS, Mbeya DC, Chunya DC na Timu kutoka shule za ST Marry’s. Jambo la Kufurahisha ni kwamba Chunya ilitoa suluhu ya Moja kwa moja na timu iliyoongoza yaani RAS.
    Kiongozi wa timu ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ridhiwan Mshigati amesema bado michezo hii ni maandalizi tu hivyo wataendelea kufanya mazoezi ili kujiimarisha tayari kwa michezo ya SHIMISEMITA baadaye mwezi Agosti huko Mwanza.
    Afisa Michezo wa Mkoa wa Mbeya ambaye pia ndiye mratibu wa Bonanza hilo Robert Mfugale ameshukuru timu zote zilizoitikia wito wa kushiriki Bonanza hilo huku akisema kabla ya mashindano ya SHIMISEMITA inawezakana kuandaliwa Bonanza lingine kubwa hivyo wachezaji kutoka Halmashauri ya wilaya zote saba wajiandae kushiriki bonanza hili

Комментарии •