Kimbunga Hidaya chakata mawasiliano mikoa ya kusini-Dar

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 4 май 2024
  • Zaidi ya madaraja manne wilayani Kilwa, mkoani Lindi katika barabara iendayo Dar es Salaam yamesombwa na maji, hivyo kukata mawasiliano kwenye mikoa ya kusini.
    Hali hiyo inatokana na madhara ya kimbunga Hidaya kilichosababisha mvua kubwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
    Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mohamed Nyundo amesema takwimu za juzi Mei 3, na jana Mei 4, 2024 zinaonyesha kuwapo mvua kubwa zilizotokana na kimbunga Hidaya.
    Amesema mvua zimesababisha zaidi ya madaraja manne kukatika yakiwamo ya Somanga, Mikereng’ende, na la Mto Matandu, huku baadhi ya vijiji vikiwa vimezingirwa maji.
    Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Lindi, Emil Zengo amesema Somanga Mtama tuta la barabara limesombwa na maji, ikiwa ni athari za kimbunga Hidaya.
    “Baada ya mvua kunyesha kwa wingi katika ukanda wa Lindi maji yakawa mengi zaidi na kusababisha barabara eneo la Somanga Mtama kusombwa na maji.”
    Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi

Комментарии • 8

  • @abelyhokororo8622
    @abelyhokororo8622 12 дней назад

    Mwananchi mmezingua hii ndio habari gani

  • @J.C.MMwambaOG
    @J.C.MMwambaOG 13 дней назад

    Pole

  • @kendramartin3707
    @kendramartin3707 13 дней назад +1

    Niko nashangaa video kipisi ajabu hiii

  • @user-fu2xl6wp1e
    @user-fu2xl6wp1e 13 дней назад

    Hamna mpiga ppicha bora jamani saa hichi nini?

  • @JohnMhapa-cg4gu
    @JohnMhapa-cg4gu 13 дней назад

    Imenikuta leo 😅😅😅😅

  • @rofinkitali3765
    @rofinkitali3765 13 дней назад +1

    Picha bila melezo sio habari iliyokamilika.
    Sasa huyo mpiga picha aeleze ni wapi hapo na nini kimeadhirika.
    Anyway. Ni waandishi wa Tz.

  • @esthereliufoo
    @esthereliufoo 13 дней назад

    Hapo ni Somanga jmn.. Gari hazitoki kusini wala hazingii kutoka Daresalam.. Wananchi tunapata tabu.. Imagine watu walitoka Masasi tangu jana hawajafika wanakokwenda, wanaishije, mfano leo watu walikua wanakuja mikoa ya kuisini imebidi waishie hapo warudi tena Dar