"Jella Mtagwa ameteseka sana nilikuwa naishi nae, sitaki kuogea nitalia" Tino, Tenga wafunguka

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 17 май 2024
  • Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars , Pan Africa na Majimaji ya Songea Peter Tino amehudhuria mazishi ya Nguli Jella Mtagwa ambaye amezikwa mkoani Morogoro Mei 18, 2024.
    Tino amesema kutokana na Mambo mengi aliyoyafanya Mtagwa enzi za uhai wake alitakiwa kuzikwa na bendera ya taifa lakini haikuwa hivyi. Amesisitiza kuwa Heshima aliyoiletea nchi hii mwaka 1974 hali iliyomfanya awekwe kwenye stempu ambapo alifahamika dunia nzima alipaswa kuzikwa kwa heshima zote.
    Hata hivyo Tino amesema enzi za uhai wa rafiki yake Jella Mtagwa waliwahi kuishi nyumba moja jijini Dar es salaam na walikaa chumba kimoja hivyo kwake huu ni msiba mzito.
    Nae, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo hapa nchini (BMT) na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ni miongoni mwa waliohudhuria mazishi ya Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa Jella Mtagwa aliyefariki jijini Dar ea aalaam.
    Tenga amesema msiba huo kwake ni pigo kubwa kwaku amecheza nae katika timu ya taifa hata timu ya Yanga pia wamecheza pamoja.

Комментарии • 14

  • @saidramadhan71
    @saidramadhan71 23 дня назад

    Poleni Sana ndugu zetu mwenyezi mungu awape wepesi

  • @rehemamahendeka-rm2ek
    @rehemamahendeka-rm2ek 23 дня назад +1

    "Ukiwa huna kitu,kinyama cha mwitu",nimekuckia kk Peter Tino umeongea kwa machungu ya marehem kk Jella Mtagwa,lkn yote kwa yote tumshkr Allah kk amesitirika,yalobakia bac tuyapokee,Rabbi awafariji familia/ndg/jamaa wote pia wa tz WALIOGUSWA.

  • @sumayasumaya6455
    @sumayasumaya6455 23 дня назад

    Nchi ngumu saana hii.., Allah amstiri jella. Amfutie dhambi zote.. AMIN

    • @FahadAbubakari
      @FahadAbubakari 23 дня назад

      Nchi imejaa upuuzi na haipendi watu wake

  • @songombingo108
    @songombingo108 23 дня назад

    Suala la Stamp ya Jella Mtagwa lilikuwa mwaka 1982 wakati wa Kombe la Dunia zilizofanyika Hispania. Haikuwa mwaka 1974.

  • @rehemamahendeka-rm2ek
    @rehemamahendeka-rm2ek 23 дня назад +1

    Sawa sawa stamp ilikuwa ni 1982,pia mchezaji mwingine aliewahi kuwekwa ktk stamp kama kumbukumbu zng zipo sahihi ni MOHD CHUMA wa Mtwara(cjui kama yu hai au alishatangulia),hapo kk Peter kapitiwa kiduchu,wajua tena yote sbb ya MACHUNGU/CMANZI na MAYONZI kwa kjn mwenzie wa hey days.

  • @LiisaMaisha-is1hi
    @LiisaMaisha-is1hi 22 дня назад

    R.I.P nahodha nimelia nakumbuka enzi zake.umeongea ukweli.tino Alistahili heshima ya kitaifa.

    • @athumanfuko199
      @athumanfuko199 17 дней назад

      Hakika kila nafsi itaonja umauti,enzi za utoto nilikuwa namsikia sana. yani bongo mpaka uwe chawa unakumbukwa

  • @abdulrahmansalim9773
    @abdulrahmansalim9773 23 дня назад

    TANGANYIKA VIONGOZI IMANI NA HURUMA HAKUNA😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢

  • @saidimwishehekienda933
    @saidimwishehekienda933 23 дня назад

    INASIKITISHA KUONA HAYA YANATOKEA.

  • @Esterkomba-ef7eb
    @Esterkomba-ef7eb 23 дня назад

    Tenga ww ndiyo taperi mkubwa

  • @songombingo108
    @songombingo108 23 дня назад

    Leodger Tenga huwezi kukwepa lawama kuhusu kutomjali Rafiki yako Jella Mtagwa. Ulipaswa kutoa misaada ya kumhudumia na kumkatia Bima ya afya rafiki yako. Hukufanya hivyo. Sina hakika pia kama ulishawahi kumtembelea kwake wakati akiugua. Wewe Tenga na wenzio wenye nafasi nzuri kimaisha mlimtupa rafiki yenu.

    • @Mkonkotolyo
      @Mkonkotolyo 23 дня назад +2

      Wakati akiwa kiongozi wa TFF alitakiwa atengeneze utaratibu wa kuwaenzi hawa wenzake lakini hakujali na hata walipokua wanamfuata kumuomba msaada alikua anawakimbia.