SAKATA LA SUKARI, WAZALISHAJI WAVUNJA UKIMYA KUTOTENDEWA HAKI

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 1 июл 2024
  • Umoja wa Wazalishaji wa sukari nchini (TSPA) umekanusha madai ya kuficha sukari ili kuongeza bei kwa faida yao binafsi.
    Wamesema hawana nia ya kuwa waagizaji kwa sababu lengo lao ni kuzalisha zaidi, huku wakilalamika kwamba wametuhumiwa na kuhukumiwa bila kupewa nafasi ya kusikilizwa.
    Wamesema wao hawana nia ya kuwa waagizaji wa sukari, kwa sababu lengo la biashara yao ni kuzalisha zaidi.
    Akizungumza kwa niaba ya wazalishaji wa sukari jana Jumatatu, Julai 1, 2024, mbele ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wazalishaji wa Sukari nchini, Ammi Mpungwe, amesema tangu utabiri wa hali ya hewa ulipotangazwa na kuonesha kwamba kutakuwa na mvua za El Nino, wazalishaji waliwasiliana na mamlaka za Serikali kuzitaarifu kwamba Desemba mwaka jana kungekuwa na tatizo.

Комментарии • 11

  • @isaachayes9783
    @isaachayes9783 19 дней назад +3

    Curtaiĺ ipo na ninyi mnafanya 'silent curtail' msitudanganye, ujanja huu mshaufanya mara nyingi ndio maana hakuna stability kwenye bei ya sukari.

  • @godfreybigeyo4356
    @godfreybigeyo4356 19 дней назад +1

    Ukipitia comment unaona watanzania ni mazombi , hii ingekuwa inahusu mambo ya Mpira ungeona comment kama elf 20

  • @geofreymranda9743
    @geofreymranda9743 19 дней назад

    Tafsuri ya haraka, huu ni ujumbe kwa bashe kuwa hawamtaki na hawataki kushilikina nae katika sekta ya kilimo kwa wakulima wa miiwa na wazaliahaji wa sukali🤔

  • @godfreybigeyo4356
    @godfreybigeyo4356 19 дней назад

    Serikali ya vibaka hii

  • @tibbsminja2575
    @tibbsminja2575 19 дней назад

    Acheni kutuona mazuzu! Badala ya kuja na majibu ya hatima ya tatizo hili kwa wananchi mmeendeleza uchawa! GEN Z wapo wanaangalia.

  • @andreap.assenga8480
    @andreap.assenga8480 19 дней назад

    Tatizo kwa nini kila mwaka linajirudia?
    Mimi binafsi naona waache uhuru wa kuagiza ili kuleta unafuu kwa mlaji suala kubwa walipe kodi au waongeze viwanda vya sukari.
    Hujuma za kila mwaka na kupanda bei tulisha zoe sbb zipo zipo kila mara.

  • @senixdanethox
    @senixdanethox 19 дней назад

    Kuna shida hadi kwenye kamati za bunge kuna kauli mzee kaongea mpina anajambo lake

  • @abdulikilala5902
    @abdulikilala5902 19 дней назад +1

    Kiko wapi wabunge mliokuwa mnamtetea Hussein Bashe mlaaniwe ninyi wakina msukuma na gengeni lenu la kupinga wabunge wazalindo mlaaniwe

    • @isaachayes9783
      @isaachayes9783 19 дней назад

      We ndio ulaaniwe maana ni mbumbumbu, unaamini maneno yao hawa bila kujiridhisha wayasemayo ni kweli au la, je kuna curtail au la,

  • @godfreybigeyo4356
    @godfreybigeyo4356 19 дней назад

    Tanzania ya vibaka hii