MATATIZO WANAYOPITIA WAFANYAKAZI WA MAJUMBANI
HTML-код
- Опубликовано: 12 янв 2025
- kunyanyaswa kingono Kunyimwa Mikataba na Misharaka pamoja na kukosa Huduma rafiki za Uzazi wa Mpango ni miongoni mwa Matatizo sugu yanayowakumba wafanyakazi wa Majumbani ambao wameiomba serikali iingilie kati ili wapate haki zao za Msingi kwa Mujibu wa Sheria za Nchi na Miongozi ya Shirika la Kazi Duniani ILO
Taarifa na Nelson Munema
Wakizungumza Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani wakati wa Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo katika Majukumu yao yaliyoandaliwa na Shirika la CVM wafanyakzi wa Majumbani wameitaka Jamiii iache kuwapuuza na Kuwanyima haki zao stahiki kwani wao ni wafanyakazi Kama wafanyakazi Wengine
Naye Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Bagamoyo Bakari Ally amesema serikali inatambua Mchango wa kila mmoja kwa Maendelo ya Jamii na Uchumi kwani Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Ibara ya 22 inamtaka kila Mtu kufanya kazi kwa Usawa