DKT NCHEMBA AZINDUA MFUMO WA KIELETRONIKI WA FORODHA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 30 май 2024
  • Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amewaongoza Mawaziri wa Nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika uzinduzi wa Mfumo wa Kielektroniki (EAC e-Tariff Software), utakaorahisisha upatikanaji wa taarifa mbalimbali za kiforodha.
    Uzinduzi huo umefanyika wakati wa Mkutano wa 44 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, Jijini Arusha.
    Dkt. Nchemba alieleza kuwa kupitia Mfumo huo watumiaji watapata taarifa mbalimbali kuhusu viwango vya pamoja vya ushuru wa forodha kwa wadau wanaohusika na masuala ya kiforodha katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo.
    Aidha, alisema kuwa Mfumo huo umelenga kurahisisha uchakataji na ufuatiliaji wa maombi ya unafuu wa ushuru wa forodha (duty remission) hivyo kupunguza urasimu pamoja na muda wa kupata huduma hizo.

Комментарии • 1

  • @PaschalFrancis-ex5zr
    @PaschalFrancis-ex5zr Месяц назад

    Mungu mbariki wazir wa fedha wa Tz Dr mwiguru L Nchemba kwa uzalendo katika nchi yetu na Kaz kubwa anayoifanya