Tamko la JWTZ Juu ya Wanajeshi 14 Waliouawa Congo DR
HTML-код
- Опубликовано: 9 фев 2025
- Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania limesema kikundi chake cha ulinzi na usalama kilichopo DRC kwaajili ya kutekeleza jukumu la ulinzi na amani kilivamiwa na Waasi waliojilikana kuwa ni ADF na kusababisha mauaji kwa wanajeshi 14.
Amesema kwamba tukio hilo lilitokea katika eneo la kambi iliyopo daraja kwenye mto Simulike barabara ya kutokea Oicha kwenda Kamango mpakani mwa nchi ya Uganda Kaskazini Mashariki ya wilaya ya Beni Jimbo la Kivu Kaskazini.
Akithibitisha mauaji hayo muwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania (CDF) Luteni Jenerali James Mwakibolwa amesema shambulio hilo lakuvamiwa lilizusha mapigano baina ya kikundi hicho na kile cha waasi na yalidumu kwa takribani masaa kumi na tatu (13) na kusababisha vifo vya askari wa Tanzania 14 na wengine 44 kujeruhiwa na askari wawili bado hawajulikani walipo ambapo jitihada zaidi za kuwatafuta zinaendelea.
Amesema shambulizi la tarehe 7 kuamkia tarehe 8 Desemba lilikua baya zaidi kuwahi kuitokea tangu vikosi hivyo vianze kushiriki ulinzi wa amani nchini DRC mwaka 2011 kwakua limeleta madhara makubwa, hata hivyo kikundi hicho ambacho bado kipo huko kinauwezo mkubwa wa kutekeleza majukumu husika kwa uhodari wa hali ya juu ,ushupavu, weledi mkubwa na umahiri stahiki.
Kwa niaba ya mkuu wa majeshi Luteni Jenerali Mwakibolwa amewathibitishia watanzania kuwa tukio hilo halitawavunja moyo na kamwe Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania halitatetereka kupeperusha bendera yake ndani na nje ya nchi kwani tukio hilo limewaongezea nguvu, ari ,ushupavu na uhodari zaidi katika kutekeleza majukumu yake.
Aidha amesema nchi pia iko salama na itaendelea kuwa salama na yeyote ambaye anataka kuwajaribu atashughulikiwa ipasavyo kwani historia ya jeshi inadhihirisha uwezo thabiti.
Kuhusu taratibu za kusafirisha miili ya marehemu kuirejesha nchini zinafanyika chini ya utaratibu wa Serikali na umoja wa mataifa na JWTZ na serikali wanaendelea kuchukua hatua stahiki kufuatia tukio hilo ikiwemo kufanya uchunguzi katika eneo husika sambamba na kuangalia taratibu za kuwajulisha familia za wafiwa zimekamilika na ndio maana hawakuweza kutoa taarifa hizo bila kuwaweka sawa familia za mashujaa hao.
Kwa umoja wa watanzania amewataka kuwaombea dua roho za mashujaa hao zipumzike mahali pema peponi kwa amani na majeruhi wote wapone haraka iwezekanavyo ili warejee kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa ulinzi wa taifa na dunia nzima.
Mwenyezi mungu awalaze pahala pema amiin mashujaa wetu
mapigano yalikuwa makali Sana.. Mungu awapokee na roho zao mahali pema Peponi.amina
Ndio mitihani bhana! Poleni sana.
mungu ibariki tanzania mungi libariki jeshi letu amina
Mashujaa wetu mungu awapokee na mungu awaponyeshe jeshi retu riko imara poreni wakuu
Mungu alito na Mungu ametwaa Jina la Bwana Libarikiwe Amen.
Mungu ibariki Tanzania pamoja na vyombo vya usalama
😊na marehemu wetu au nmeskia vby
Kukosea lazima kuongea maana wanajeshi walioko huko mipakan ndo tunao wategemea 💃Allah azipumzishe roho za marehem 😢👏
Mungu azilaze pema roho za marehemu amina
Awalaze Mahal pema pepon amen
Mungu aliye muumba wa vyote na mwamuz wayote kwa namna ya pekee naomba umtume roho wako Mt. Akawafariji wafiwa wote.
Innalilah Wainnalilah rajiun, Allah warehem waliotangulia Ameen👏
Jamani kwann tupoteze ndugu zetu waludi wote hatutaki kumalizwa namba hii sawa niuchujaa lakini hawafanyii kwawenyewe ni majonzi kwa inchi yetu mungu azilaze roho zamarehemu pema peponi
Mungu azipokee roho za makamanda wetu, Amen.
Poleni sana Jeshi la Wananchi la Tz, Mungu awapumzishe mahala pema mashujaa wetu, na awaponye majeruhi wote ili wawe na afya njema na warejee katika majukumu yao ya kudumisha amani. Ila Mnadhim mkuu hapo mwisho sijamuelewa, anasema na marehem wetu wapote haraka na weendelee na kazi. Marehem wanaweza kupona kweli?
Richard Nyamahanga na wewe umesema wapote ulimi hauna mfupa
From 🇧🇮 inalillah wa inalillah rajiun
sawa kaka mwakibolwa nimekuelewa naomba amani itawale kwani mdogo wangu yuko huko
single soldier attack under enemy fire ni noma sana poleni wapiganaji we2 mungu awatangulie
duu wanaume kazi poleni xana
kuzaliwa ni siku moja na kufa ni siku moja poleni sana familia Kwa kupoteza na taifa ila Pongezi Kwa jeshi kuthibitishia Uma kuwa jeshi ndo limeimalika zaidi
daa inasikitisha saaan polen wote mloondekewa na wapendwa wenu mungu ibariki Tz lakin watoen huko jaman
R. I. P, ndugu zangu. Mungu nakuomba uwapokee ndugu zangu kwa upendo wako na kwa aman yako ktk ridhaa yako. Inshaallah. TANZANIA NGUVU MOJA.
Mungu awape subra ndugu na jamaa waloondokewa na wapendwa wao.
Jameni laiti Nyerere angali Jua hayo ayatendayo Suluhu? Ange jutia sanaaaaa!
ni Leteni jenerali sio meja jenerali,. fuatilieni vizur alama Za vyeo,. Wana habari
Mwakibolwa.. tanzania
Ni Lt. Gen siyo Maj. Gen
majeruh bhana siyo marehem
Marehemu wetu wapone haraka iwezekanavyo, Hii imenda
Mungu fariji familia zao
Hhhh mtalia sana kwa hivi wamekufa mamia wameuliwa na m23
Poleni Sana wapi ganajiwetu
Aksanteni Tanzania kwa kujitolea kutulinda sisi wakongo tuna waheshimu
Jaman mbona nguvu kazi zetu wanajeshi wetu wanateketea uko congo? Nchi yenyew haitak aman leo wanaili kesho lile kama mashekwani tu 😭😭inauma sn iseee 😭😭😭😭😭😭
Acheni kutupigia kelele kwann msiwapige mpaka alie watuma kila siku wanajeshi wauwawa kila siku mpo tu tunataka wapigwe walio shiliki
Huyo Ni luteni generali sio meja jenerali
Jamani kamanda hakutuambia hayo mapigano wamekufa waasi wangapi ?
Saa 13 chuma zinalia tu daah sio poa
Kwanin waasi hawaoneshwi wanapokufa wao
jamani kaka zetu na dada zetu warudi nyumbani poleni familia za wanajeshi hawa
Askari wetu hawajazoea kukabiliana na waasi ila wamezoea kupambana na wananchi wanaoandamana tena wasio na silaha. Ni vema kuwaandaa askari vijana wetu kabla ya kuingia katika uwanja wa mapambano, vinginevyo watkwisha wote . Tutaambulia makaburi.
Ndiyo maana askari waliouawa ni Watanzania japo kulikuwa na askari toka nchi mbalimbali.
God bless Tanzania. Amen.
Usiongee ujinga uwo kijna una unacho kijuwa kakimya
waje home haraka
et naomba kuuliza. iv uko congo wanaofanya matukio ni wanajesh pia. maana nshawah kuona kuna kipind iv wanajesh wanauwa watu then wanawatupa kwenye uwo mto wa mamba
Rest Easy Fallen Heroes!
Poleni jeshi la wananchi wa Tanzania, Amiri jeshi mkuu na Watanzania Kwa ujumla. Lakini tuna maswali: hao waasi wanafadhiriwa nani? Nini malengo yao? Kijografia wanatokea wapi ktk DR Congo? Shughuli zao kiuchumi ni zipi? Wanapata wapi silaha na chakula? Mungu tusaidie kuifanya Africa kuwa sehemu salama ya kuishi na kupiga hatua kimaendeleo
Plse serikali watunzieni wazee na wake zao waliowaacha uhai wao wote na muwasomeshee watoto wao pia. Isie km baada ya kupewa kiunua mgongo baadae bac.
Nmesikia roho za marehem zipone haraka
Pole Sana 😭😭R.I.P
tutafika tu kwenye lengo
inauma jamani bora waliobaki warudi
Ni luteni general siyo meja muwe making mnapoandika
sasa hapo mkuu marehe,u wanaponaje tena
Idf siyo mchezo rudisheni wanajeshi wataishia huko waasi wa congo🇨🇩 wameshindikana umoja wa mataifa wameshindwa. lengo la kupeleka jeshi ni nn au ni kutafuta sifa UN
Bado mna waachatuu huko.mungu ibarikiTanzania.
Hapana Amani gani unaenda kulinda inchi ya jirani wenyewe awana Amani kwenye Inchi yao warudisheni Ndgu zetu hari yanini Ndgu zetu kila cku wanahuliwa inje ya inch i inauma sana hata kama warudi walide Amani hapa nyumbani
Kiukweli inasikitisha sana aisee daaah bora ndugu yangu hakurudishwa tena huko, sasa na huyo mkuu anasema marehem wapone duuh ni kuchanganyikiwa ama kama yeye kapagawa hivi sasa walioko kule wako katika hali gani
Kassim Ramadhani amen
Aisee inauma
😭😭😭😭😭
Daaah Ndiyo maana niligoma kwenda jeshi
hata km usipokuwa mwanajeshi siku yako ikifika utakufa tu.
kwani wanaokufa ni wanajeshi tu..??
kauze maandazi wache wanaume wapeperushe bendera
Ramadhani Athumani acha woga
Kwenda jeshini siyo kufa wewe,kifo hutokea sehemu yoyote.
Mnatafuta dhahabu , alimasi, Uranium lakini jueni kwamba mtavilipa Kwa damu ya watanzania!!! Je mbona munahivyo vyote kwenu? Simurudie kwenu!
r.i..p solder
Muwafate wote watoke huko si kwao.
marehem wetu waponee haraka 😂😂😂😂😂😀😀
Usicheke kachanganyikiwa..inaumiza sana
Meja kachapia😂😂😂😂
Huyu si ndio Yule jamaa alisema marehem wapone haraka si ndio Huyu au vipi?
Damu ya mtanzania haipotei bure
ETI MAREHEMU WETU WAPONE HARAKA IWEZEKANAVYO ..haupo serious kamanda
RIP 😭😭😭😭😭😭😭😭
dah
uchunguzi ufanyike na kujua uwezo wa silaha za waasi na wanajeshi wetu
ikitokea pana uzembe uwajibikaji uchukue nafasi yake kwa pande yeyote
ndo jeshi hiyo,poleni ndugu zangu
mi naona Tanzania ni nchi yenye aman kwa nn tunajipendekeza kwenye mataifa ambayo wao wenyewe wameshindwa kulinda amani yao
Kwa kweli
Meja kavulugwa
Wapigeni tu hao waasi mnawalea wa nini piga
mkuu marehemu haponi maana ameshakufa
Yeyote atakayetaka kutujaribu atashughulikiwa ipasavyo
R.I.P MAKAMANDA WETU
rudisheni majeshi yetu wate kila nchi ibebe msalaba wake
rip mungu awabrk família YA marehemu wawe na Subra ktk kipind hik kigumu?
RIP Makamanda wetu.
R I p makomando
Eti Na marehemu wetu wapone Kwa haraka iwezekanavyo khaaa😂😂😂
Hassani Sadiki haaa haaaa haaa marehemu wetu!
Hata mimi niliskia hivyo kasema na mimi nikasema kama ulivyozungumza wewe
Kakosea hapo ulimi uliteleza,itakua majeruhi kakusudia huyo
Hassani Sadiki kavulugwa meja
Hassani Sadiki hahahaaa
Hahahah eti marehemu wetu wapone haraka iwezekanvyooo!!!!!!
Hussein Muhammad usimcheke msiba kubwa huo hawezi kuwa sahihi katika kuongea.
wewe husen Mungu anakuona kwani wewe hua hukosea ktk kutamka
R.I.P makamanda
R I P
askari wa f
RIP
Mbona mkuu huna ht kielezo ktk mwili wako kwa Taifa lina msiba mzito ?!!!!. Mfano kitamba cheusi au vazi jeusi. Au huko sio smdestuli yenu ?
R.I.P
r.i.p infactia
Mnabebana kwenda huko
siri majini
Pole Sana 😭😭R.I.P
R.I.P
siri majini