Zitto amjulia hali Sativa, 'asema tuhakikishe matukio haya' ...ataka uchunguzi

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 13 сен 2024
  • Kiongozi mstaafu wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe ameitaka Serikali kufanya uchunguzi huru na wa kina kuhusu vitendo vya utekaji vinavyojitokeza mara kwa mara nchini Tanzania, ili wanaohusika wafikishwe katika vyombo vya sheria.
    Amesema vitendo vya utekaji vilishaanza kusahaulika nchini, lakini hivi sasa vimeanza kurejea upya na kuzua hofu kwa Watanzania, hasa katika familia ambazo ndugu zao wanakumbwa na hali hiyo.
    Zitto ametoa ushauri huo siku chache tangu kuripotiwa tukio la mkazi wa Mbezi, Dar es Salaam, Edgar Mwakabela maarufu kama 'Sativa' anayedaiwa kutoweka Juni 23, 2024 na kupatikana Juni 27, 2024 katika pori la Hifadhi ya Katavi akiwa na majeraha.
    Sativa ambaye amepata majeraha, ikiwemo mpasuko wa taya zilizosagika huku baadhi ya mifupa ikionekana na mipasuko midogo, hivi sasa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.
    Zitto ameeleza hayo leo Jumanne Julai 2, 2024 alipozungumza na wanahabari muda mfupi baada ya kwenda kumjulia hali Sativa aliyelazwa Aga Khan.
    "Uchunguzi huru ufanyike, ili kukomesha matukio haya yaliyoanza kushamiri katika siku za hivi karibuni. Matukio haya yanaharibu taswira ya nchi yetu, yanaturudisha katika zama ambazo wengine tuliamini tumeshatoka.
    "Njia pekee ya kukomesha haya ni kufanyika uchunguzi huru na wa kina, ili hatua stahiki zichukuliwe kwa watu watakaohusika na matukio haya," amesema Zitto.

Комментарии • 2

  • @SmilingCityMap-xb9md
    @SmilingCityMap-xb9md 2 месяца назад

    Tuache unafki jamani unafki utatumaliza

  • @ZawadyKaoneka
    @ZawadyKaoneka Месяц назад

    😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂cc yetu macho cc mazezeta ipo cku tutafika