HATIMAYE SERIKALI, WAFANYABIASHARA WAFIKIA MAKUBALIANO

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 26 июн 2024
  • DODOMA: SERIKALI imefikia makubaliano na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara baada ya siku nne za majadiliano kwa ngazi mbalimbali kuzaa matunda.
    Sasa wafanyabiashara wataendelea kufanya biashara zao kama kawaida chini ya maazimio 15 ambayo ndani yake pia kuna maagizo ya Serikali yanayoleta unafuu kwa wafanyabiashara hao kufanya biashara zao katika mazingira ya kuridhisha.
    Mazungumzo hayo yalikuja baada ya wafanyabiashara hao kuja na hoja takribani 41 walizoziwasilisha serikalini kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara zao.
    Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mkoani Dodoma leo kuhusu matokeo ya majadiliano baina ya pande hizo mbili.
    Majadiliano hayo ambayo kwa upande wa Serikali yalikuwa yanawakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yalihusisha Mawaziri wa Sekta husika ambaye alitumia falsafa ya Maridhiano miongoni mwa R4 za Rais Samia Suluhu Hassan ambayo ilileta matokeo chanya kwa siku nne za majadiliano yaliyohitimishwa mkoani Dodoma.
    Follow us on:
    FACEBOOK;
    SpotiLeo: / spotileo-176. .
    HabariLeo: / habarileo
    DailyNews: / dailynewstz
    INSTAGRAM;
    HabariLeo: habarileo_tz?ig...
    SpotiLeo: spotileo?igshid...
    TWITTER;
    Twitter HabariLeo: HabariLeo?s=09
  • РазвлеченияРазвлечения

Комментарии •