Kunambi :Tanzania ndio nchi pekee duniani wakurugenzi wanateuliwa, wanatakiwa kuomba nafasi....

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 21 апр 2024
  • Mbunge wa Mlimba (CCM), Godwin Kunambi ameshauri nafasi za uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri wasiteuliwe wanasiasa na badala yake watu wafanye usaili ili mamlaka ya uteuzi ipelekewe majina ya watu watatu ambao wanatokana na utumishi ili mmoja wao awe mkurugenzi.
    Kunambi ameyasema hayo leo Jumatatu, Aprili 22, 2024, wakati akichangia maoni yake kwenye makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kwa mwaka 2024/25 ambapo amesema kwa kufanya hivyo nchi itakuwa na watu waliopo kwenye fani hivyo kuleta maendeleo.
    Kunambi amesema Tanzania pekeyake ndio nchi inayoteua Wakurugenzi wa Halmashauri huku akisema nchi nyingine Duniani hazifanyi hivyo na kutaka kuwa wakurugenzi wasiteuliwe kutokana na historia zao za nyuma kwenye siasa.
    Godwin Kunambi alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kabla ya kwenda kugombea ubunge kwenye Jimbo la Mlimba, kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM na kuibuka kidedea kwenye uchaguzi uliopita wa mwaka 2020.

Комментарии • 16

  • @ALESIACHIJOKA
    @ALESIACHIJOKA Месяц назад +1

    Uko vizuri hongera kwa muongozo wako na kuwapa maarifa mawaziri na kazi zao UBARIKIWE SANA .. NAKISIFU PIA UNA SAUTI YA UTENDAJI .. .

  • @pastorgodwinchengula7848
    @pastorgodwinchengula7848 Месяц назад +1

    Hapo hawapigi makofi kwenye point nzito kiasi hicho! Kuna shida kubwa Sana ktk siasa yetu bado!

  • @abushirikwani5
    @abushirikwani5 Месяц назад

    Mungu aku aukupe maisha marefu sana maana ulitupambania sana Wana ndachi ila ss wamebaki vidabwa vidabwa tu

  • @BarakerZeonlist
    @BarakerZeonlist Месяц назад

    you deserve to save the country

  • @patrickKitambo
    @patrickKitambo Месяц назад

    Hua mnapoteza muda mwingi kwenye shukrani ambazo hazina kichwa wala miguu

  • @omaryalhaj3139
    @omaryalhaj3139 Месяц назад +1

    wambie viongozi wetu huwezi kuweka mkurugebz kuwa mwanasiasaaa

  • @RubenMtuwaMungu-bz8ee
    @RubenMtuwaMungu-bz8ee Месяц назад

    Tukiendelea na mtindo wa kuteua watendaji wa serikali nchi yetu itaendelea kuwa kichaka cha wizi.

  • @karolikisaka8991
    @karolikisaka8991 Месяц назад +1

    Ccm wanajitoa ufahamu hapa ni katiba tuu

  • @PhilipoMwasha
    @PhilipoMwasha Месяц назад

    Kunambi ni madini matupu safiii tunataka wabunge kama hawa

  • @HassanMohamed-fn8ue
    @HassanMohamed-fn8ue Месяц назад

    Kaka Bado huja iva

  • @solomoneglesias9752
    @solomoneglesias9752 Месяц назад +1

    C useme tuuu kuwa katiba mpya ni sasa au unaogopa kuitwa na kuhojiwa kuwa au umetumwa na Mbowe🤣🤣🤣🤣

    • @sonnyr1899
      @sonnyr1899 Месяц назад

      Katiba waka ku vyote ni bure kama hakuna utashi wa uzalendo.
      Kenya wanakatiba mpya OG ila kila uchaguzi ukikaribiya wanakufa watu na uchaguzi ukimaliza katiba unarudi kuheshimiwa tena.
      Kikubwa ni uzalendo wa kujenga nchi kuliko ubinafsi wa kujifaidisha mifuko na familiya zao.

  • @petersilas4234
    @petersilas4234 Месяц назад

    Katika jambo la kurekebishwa haraka bila kusubiria katiba ni kuondoa huo uteuzi wa watendaji wa ngazi za watendaji kuteuliwa na rais.

  • @charlesmarco248
    @charlesmarco248 Месяц назад

    hawawezi ndg mjomba atapeleka jina kwa mhusika atapea

  • @EliauMtishbi-os5ky
    @EliauMtishbi-os5ky Месяц назад

    Tukipata KATIBA mpya itaondoa cheni ya teuzi ambazo hzina mshiko.

  • @georgemahenge
    @georgemahenge Месяц назад

    Hiyo imepenya