KIPINDI MAALUM CHA RAIS DKT.JOHN MAGUFULI ALIPOZUNGUMZA NA VIONGOZI WAKUU WASTAAFU

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 3 июл 2018
  • Hii ni mara ya kwanza kwa Mhe. Rais kukutana na viongozi hao wakuu wastaafu na kupokea ushauri na maoni yao juu ya uendeshaji wa Serikali na mustakabali wa Taifa.
    Katika mkutano huo viongozi hao wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuwaita kwa lengo la kusikiliza ushauri na maoni yao, na wamempongeza kwa kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi kifupi cha miaka miwili na nusu tangu ilipoingia madarakani.
    Viongozi hao wamemshauri Mhe. Rais Magufuli kuimarisha na kujenga taasisi zinazosimamia uendelevu wa kazi nzuri zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Tano zikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kama vile ujenzi wa reli, mapambano dhidi ya rushwa, kuimarisha nidhamu kazini, kutilia mkazo watu kuchapa kazi, kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali na utoaji wa huduma za jamii.
    Viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa kudumisha amani kwa kuhakikisha haki inatendeka, kutathmini matatizo ya wananchi na kubuni mbinu za kuyatatua, kusimamia kwa ukaribu shughuli za kilimo na ufugaji ambazo zinaajiri Watanzania wengi na ni muhimu kwa maendeleo ya viwanda na kuboresha kiwango cha elimu.
    Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amewashukuru viongozi hao kwa maoni na ushauri waliompa na amewahakikishia kuwa ataufanyia kazi.
    Mhe. Rais Magufuli amewaeleza viongozi hao juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali hivi sasa ikiwemo kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali ambao umeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 800 hadi kufikia Shilingi Trilioni 1.3 kwa mwezi, ujenzi wa reli ya kisasa kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma utakaogharimu Shilingi Trilioni 7.26, kujenga mradi wa umeme katika mto Rufiji (Stieglers’ Gorge) utakaozalisha Megawati 2,100 za umeme, kutoa elimu ya msingi na sekondari bila malipo na kuongeza mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.
    Mhe. Rais Magufuli amewahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea vizuri na kwamba itaendelea kutatua changamoto ambazo bado zipo kwa juhudi kubwa ili Tanzania iwe nchi nzuri kwa Watanzania wote.

Комментарии • 54

  • @peterlibota1052
    @peterlibota1052 6 лет назад +4

    Ni heshima kubwa sana aliyoitoa Rais JPJ Magufuli kwa kutambua uwepo wa hao waliomtangulia katika kuijenga Nchi hii.Mungu Ibariki Tanzania,Mungu wabariki Viongozi wetu wote kila mmoja na sehemu yake ya Utendaji.Amina.

  • @kilimanjaroICE
    @kilimanjaroICE 6 лет назад +5

    Wooooow!!! That was so deep and amazing at same time. Magufuli is probably the best President in the Continent right now and the history will prove that. Tanzania Kwanza.

  • @jameslikata1581
    @jameslikata1581 7 месяцев назад +1

    Mungu aiweke roho yake pema.

  • @nyanda427
    @nyanda427 6 лет назад +5

    Well done wazee wetu, Mungu awabariki sana

  • @Epicmark_Group
    @Epicmark_Group 6 лет назад +3

    Ninafurahi sana kwa hili mheshimiwa Rais. Hongera.
    Pia pongezi kwa wastaafu kukubali kutete na rais.

  • @mukhtaribura6159
    @mukhtaribura6159 3 месяца назад

    M,mungu awake roho yake peponi ameen

  • @alexfrance5486
    @alexfrance5486 6 лет назад +2

    I always appreciate my President for the great job

  • @dmstephano8643
    @dmstephano8643 6 лет назад +3

    Nimefurahi sana kuwaona viongozi wetu wakiwa pamoja 🙏🙏🙏god bless my Tanzania

  • @bonifacegamba495
    @bonifacegamba495 6 лет назад +1

    Mungu ibariki Tanzania Mungu mbariki Rais wetu

  • @edwardedward2520
    @edwardedward2520 6 лет назад

    Hongera sana Mh. Rais wetu mpendwa Mungu aendelee kukulinda kukupigania.... Si kazi nyepesi MTU lelemama asingeiweza.

  • @greensky9607
    @greensky9607 6 лет назад +1

    Hongera sana Mh. Rais wangu kwa uamuzi wako wa kuwakutanisha wastaafu wa ngazi za juu kabisa katika nchi yetu na kuchota baraka zao.
    Ninakuamini katika kusikiliza na kutenda, kwa jitihada zako Tanzania ya mfano inakuja kwa kasi ya ajabu, ni lazima sasa kila mtu atambue ama afahamu kuwa kuna SERIKALI, na ni lazima iheshimiwe.
    Umeweza kwa muda mfupi kulirudisha Taifa la uchapa kazi, japo bado wachache hawajaweza kukuelewa, WATAKUELEWA TU.
    TANZANIA TUTAIJENGA WENYEWE, AMANI, UPENDO NA UTULIVU TULIONAO TUTALINDA KWA GHARAMA ZOZOTE ZILE.
    VIVA JPM,
    ASANTE MAWASILIANO IKULU.

  • @abeidmayanga809
    @abeidmayanga809 6 лет назад +1

    our greatest president in Africa ubarikiwe

  • @amabilis-mariesangu9500
    @amabilis-mariesangu9500 6 лет назад

    This is absolutely beautiful to see. Precedence is the way to go..Mungu Ibariki Afrika Mungu Tubariki watanzania

  • @deusgabri
    @deusgabri 6 лет назад +4

    Mhe. Benjamini kaongea mstari mnyoofu.......

  • @agneomasonda2462
    @agneomasonda2462 6 лет назад +1

    Hongera sana Mheshimiwa Rais Magufuli

  • @sk-wj9or
    @sk-wj9or 6 лет назад +1

    Umeshinda Magufuli good way ahead. Well done.

  • @yusuphshabani7285
    @yusuphshabani7285 6 лет назад

    mungu akujaalie maisha marefu kiongozi wetu kwasbbu yeye ndie aliekuchagua mtetezi wawanyonge.

  • @prospermakundi2787
    @prospermakundi2787 6 лет назад +1

    Safi sana raisi wetu Mungu azidi kukuongoza

  • @shukuruexperius5035
    @shukuruexperius5035 3 года назад

    Mzalendo wa kweli hongera sana Jpm haijawahi kutokea wewe ndio wa kwanza

  • @ambelecheyo5667
    @ambelecheyo5667 6 лет назад +1

    Nakupenda buree rais wangu.

  • @ValEmaChannel
    @ValEmaChannel 6 лет назад +1

    And that's all God bless the retired and Our currently President and God bless Tanzania.
    Fulfill #GreatTanzanianDreams

  • @NyakiMollel
    @NyakiMollel 3 месяца назад +1

    Kuna mzee kaongea kitu cha ajabu cjui alitawalaje hii nchi

  • @athumanomary1438
    @athumanomary1438 6 лет назад +5

    Mwenyez MUNGU tunazidi kukuomba enderea kumuongoz raisi wetu

  • @dickaugustino2214
    @dickaugustino2214 6 лет назад +3

    Better be so, its bitter but sweet!?

  • @khamismallya7588
    @khamismallya7588 6 лет назад +3

    Ziundwe taasisi zitakazosimamia serikali ili tusije rudi nyuma tena ushauri si wakuacha huu

  • @yusufurahabiamu6052
    @yusufurahabiamu6052 6 лет назад

    Mungu akuongezee hekima na busara zaidi amen

  • @yahayaseif5175
    @yahayaseif5175 6 лет назад +6

    Tunaiomba ikulu ikitoa habari wakalimani wawepo kutafsiri kwa lugha ya alama.
    Viziwi wa tanzania nao pia wanadai haki yao kupata habari bila kubanwa uhuru wao wa kupata habari.
    Yahya al sawafi.
    DEAF PERSON.
    chake chake
    Pemba

  • @omaryyusuph3251
    @omaryyusuph3251 6 лет назад

    Ahsante warioba na malecela

  • @emmanuellyatuu4103
    @emmanuellyatuu4103 5 лет назад

    Great indeed Mr President...nimekuelewa sana

  • @hassansamata3666
    @hassansamata3666 6 лет назад

    Mzee mwinnyi umeongea vizuri

  • @dickaugustino2214
    @dickaugustino2214 6 лет назад +1

    Good Mr president j.p.m, sisi wanyonge tupo na tunakutazama, tukisubiri useme kitu ktk hizi taasisi za mifuko ya bima,pesa kutoka isiwe mpaka MTU afikishe miaka amsini na za zaidi,bora kuwe na utaratibu kwamba MTU akichukua pesa zake, aende akafanye masuara ya msingi.kuepusha utegemezi baadae.

  • @edwardedward2520
    @edwardedward2520 6 лет назад

    Indeed it is very clear..

  • @greensky9607
    @greensky9607 6 лет назад +1

    The Making of Tanzania to be Great Again

  • @abellabv
    @abellabv 6 лет назад

    Mstarini: (Wimbo wa Taifa - kwa sauti Kuu) "...Heekima, Umooojaaa, na Amaaaniiii: hiiiziii ni ngao zeetuuu,..."
    Darasani: (Salaam - kwa sauti Kuu) "Ili tuendelee twahitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi, na Uongozi Bora. SHIKAAAMOOO MWAAALIM."

  • @ahmed59122
    @ahmed59122 6 лет назад

    IS GOOD MAN

  • @athumanomary1438
    @athumanomary1438 6 лет назад +3

    Ewe mwenyez MUNGU ewe mwenyez MUNGU ewe mwenyez MUNGU tunazidi kukuomba enderea kumuongoza kumsimamia kumrinda kumuipushia kira yario mabaya na zidi kuimarisha afya yake raisi wetu ewe mwenyez MUNGU mkuu

    • @ValEmaChannel
      @ValEmaChannel 6 лет назад

      Athuman Omary Amen.
      Mungu asikie kuomba kwetu

    • @abellabv
      @abellabv 6 лет назад +1

      Isaac Valema. AMEN, AMEN, AMEN.

  • @kalundemedia242
    @kalundemedia242 6 лет назад +6

    Ninafikiri sana namna ya kuwashawishi watanzania wote wakubaliane nami kuuondoa utaratibu wa "Periodic Election" kwa kiti cha Urais, ili Rais DKT JOHN POMBE MAGUGULI ubaki madarakani mpaka utakapoona kuwa kuna haja ya kustaafu mwenyewe; maana ktk Afrika na duniani kote sjaona Rais Mzalendo kama wewe. Tanzania ilikokuwa imefikishwa ni kubaya hakuna mfano, lakini leo ni miaka miwili na nusu tu ya utawala wako mambo yamegeuka na kuwa mazuri kiasi hiki. Nakuombea kwa Mungu akujalie Afya njema, ili utufikishe salama ulipopalenga.

  • @sumaiyaturky7023
    @sumaiyaturky7023 6 лет назад +1

    Fantastic speech. Kweli ni mtu wa Mungu. Hats off for my President.

  • @mosesmkopi4786
    @mosesmkopi4786 3 года назад

    Nimerud kusikiliza hekima za Muheshimiwa Dr Benjamin william mkapa may his soul rest in peace

  • @allyfutto8763
    @allyfutto8763 6 лет назад

    Hakika ni Faraja kubwa sana kuwaona wazazi Viongozi waliotutowa huko tulikotoka mpaka hapa tulipo wapo salama na wanayo Amani mimi binafsi hili ni tukio kubwa sanakabisa maana Dunia ya sasa hakuna Nchi ya mfano huu ulimwengumzima. watanzania wamefarijika sana na mtindo huu Bora, Tanzania JUU!!! Juu!!! Juu!!! JuuZaidi!!!!!!!

  • @HakunaMatata_2024
    @HakunaMatata_2024 6 лет назад

    safi

  • @seifhabibu9890
    @seifhabibu9890 6 лет назад

    Sasa naino tanzania inavuka maana imepata mtu wa kuivusha, miaka 15 ijayo wakenya watakua nyuma yetu

  • @ibraobed8273
    @ibraobed8273 5 лет назад

    Kikwete vp mbona ajatimba hapo.

  • @japhetdaud3889
    @japhetdaud3889 6 лет назад

    Ama kweli MUNGU awafungue macho watu yawezakuwa hawaoni yale anayotenda mh. Magufuli hajawahi tokea Rais kama huyu :Labda kama msemo usemao watakuwa ma macho hawataona ,masikio wanayo hawasikii, akili wanayo hawaitumii - hivyo Mungu awasaidie watanzania wanaobeza

  • @agrikolaleo677
    @agrikolaleo677 6 лет назад +2

    JAMAA HAJAACHATU ZIARA?