RAIS DKT. MAGUFULI ATOA MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSU BEI YA KOROSHO NCHINI 2018

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 10 фев 2025
  • Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 28 Oktoba, 2018 amekutana na wanunuzi wa zao la korosho na kutoa msimamo wa Serikali kuhusu bei ya zao la korosho kufuatia kuwepo kwa mvutano wa bei ya zao hilo kati ya wanunuzi na wakulima.
    Mhe. Rais Magufuli amekutana na wanunuzi hao katika mkutano wa majadiliano uliokuwa ukiendelea kati ya wanunuzi wa korosho na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
    Katika msimamo huo Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali inaungana na msimamo wa wakulima kukataa bei zilizotolewa na wanunuzi katika mnada uliofanyika hivi karibuni ambapo kampuni za ununuzi wa korosho zilitangaza kununua korosho kwa bei ya kati ya shilingi 2,717/= na shilingi 1,900/= kwa kilo ikiwa imeshuka kutoka zaidi ya shilingi 3,600 ya msimu uliopita.
    Mhe. Rais Magufuli amesema endapo wanunuzi hao hawatakuwa tayari kununua korosho kwa bei isiyopungua shilingi 3,000/= kwa kilo, Serikali ipo tayari kununua korosho kwa bei yenye maslahi kwa wakulima na kutafuta masoko yenye bei nzuri.
    “Kama hamtanunua korosho kwa bei yenye maslahi kwa wakulima, Serikali itanunua korosho kwa bei nzuri kwa wakulima na tutaihifadhi, nipo tayari hata kutumia majeshi yetu kununua korosho na tutatafuta masoko ya uhakika ili tuuze kwa bei nzuri” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
    Wakizungumza katika mkutano huo, wanunuzi wa korosho wamekubali kununua korosho kwa bei isiyopungua shilingi 3,000 kama ilivyoelekezwa na Serikali na wameomba baadhi ya tozo zinazosababisha kupungua kwa bei ya zoa hilo kwa mkulima ziondolewe pamoja na kuruhusiwa kusafirisha korosho kupitia bandari ya Dar es Salaam ambako wanaweza kupata meli zinazotoza gharama nafuu za usafirishaji wa korosho kwenda kwenye masoko ya nje ya nchi.
    Mhe. Rais Magufuli amekubali kuondolewa kwa utozaji ushuru wa mara ya pili wa ushuru wa halmashauri uliokuwa ukifanywa baada ya korosho kufikishwa Mtwara, kupunguza ushuru wa Bodi ya Korosho kutoka shilingi 17/- hadi shilingi 10/- kwa kilo na ameruhusu wafanyabiashara kununua magunia yao wenyewe kwa ajili ya korosho badala ya kuuziwa na vyama vya ushirika kwa bei kubwa.
    Kuhusu bandari ya kusafirishia korosho Mhe. Rais Magufuli amekubaliana na maombi ya wanunuzi kutaka kusafirisha korosho kwa kutumia bandari ya Dar es Salaam ambapo kilo moja inasafirishwa kwa shilingi 47/- kwa kutumia meli ambazo zimeleta mizigo mingine ikilinganishwa na bandari ya Mtwara ambako kilo moja inasafirishwa kwa shilingi 203/- kwa kutumia meli zinazokodiwa kwa ajili ya kubeba korosho tu.
    “Bandari ya Mtwara na bandari ya Dar es Salaam zote ni bandari za Serikali, mimi sina tatizo na kusafirisha korosho kupitia bandari ya Dar es Salaam lakini na nyinyi muwe tayari kutozidisha uzito kwenye magari mnaposafirisha kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, kutotorosha korosho na pia kutimiza masharti ya usafirishaji” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
    Ameagiza Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na vyombo vya dola kuweka utaratibu mzuri utakaowezesha usafirishaji wa korosho hizo kupitia bandari ya Dar es Salaam kama ambavyo wanunuzi hao wameomba.
    Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewataka wanunuzi hao kuwekeza viwanda vya kubangua korosho ama kuwahamisisha washirika wao kuja kuwekeza katika viwanda hivyo na kwamba Serikali itaunga mkono juhudi hizo ikiwa ni pamoja na kuweka vivutio vya kikodi.

Комментарии • 124

  • @mohamedkassimu8789
    @mohamedkassimu8789 6 лет назад +10

    Mh.Rais,simamia maslahi ya wanyonge, hata mimi niliamini lazima utaliingilia Kati TU, wewe ni Rais wa mfano duniani sio tu Tanzania .mungu akulinde Sana na akupe maisha marefu.amin.

  • @mohammedjuma6736
    @mohammedjuma6736 6 лет назад +8

    Raisi wangu, Mungu akulinde na akupe umri mrefu utuongoze miaka mingi, aaaaamin, asante baba

  • @mazeramatimo1110
    @mazeramatimo1110 6 лет назад +4

    Nimeiona hasira yako Mh. Rais ukiona wananchi wako wanataka kuonewa Mungu akubariki. Nikutakie tu heri ya siku ya kuzaliwa Mungu akupe maisha, siku moja nitakuwa kiongozi na nitakuwa na nitaongoza kwa mfano wako na Nyerere,

  • @wasshaincmwanza4374
    @wasshaincmwanza4374 6 лет назад +11

    This man is a true and patriotic leader and above all he is absolutely genius

  • @rosenamilia4140
    @rosenamilia4140 6 лет назад +4

    Mh Rais wetu JPM wewe ndie Rais muwazi,mkweli mchapa kazi, mtetezi wa wanyonge na unaetoa mwelekeo sasa wananchi wako.Mungu akupe maisha marefu Mh JPM. HAPPY BIRTHDAY RAIS WETU.

    • @kingmayatz9999
      @kingmayatz9999 6 лет назад

      Nilikuwa mpinzani sana ila wewe ni rais unaejielewa sana nakupenda sana

  • @salumkseleman1470
    @salumkseleman1470 6 лет назад +2

    Baba umenifurahisha sana asante sana mzee baba😂😂😂wanakuletea ujanja hapa wakat zao hili lina kazi c ya kitoto..... Hao wahindi wanajifanya wajanja wakat wao wenyewe ni middlemen pumbavu zao
    Asante magu baba
    Korosho yetu itanunuliwa tu alhamdulilah 👏👏👏👏👏👏👏

  • @mwinukafundibombanjombe
    @mwinukafundibombanjombe 2 года назад +3

    😭Kwenye direcrion ya Mzee Ukilaza unaondoka.

  • @lameckbalekele2901
    @lameckbalekele2901 6 лет назад +24

    Rais 2020 usihangaike kuzunguka tena kupigakampeni tunakupakula mpaka washangae

  • @kingmayatz9999
    @kingmayatz9999 6 лет назад +13

    Sikukupigia kula ila hakika unanidai kula yangu 2020 nakpenda huna mpinzan

  • @yugakiyumbi9909
    @yugakiyumbi9909 6 лет назад +30

    Mungu atupe nini, this is the best president ever. Endelea kutawala hadi uchoke mwenyewe,hakuna shida,tunahitaji Maendeleo na wewe unatuletea maendeleo na pili ww n mtetezi wa WANYONGE. Nani kama Magufuli ,We love you our President, you're doing what every well minded Tanzanian needs. Rule even 40 years,we still need you.
    Chapa kazi ,HAPA KAZI TU.

    • @neemamasangula7404
      @neemamasangula7404 6 лет назад

      Enzi Za Mwl. JK. Nyerere tulisema UHURU NA KAZI sasa tunasema HAPA KAZI TU BIG UP MY PRESIDENT

    • @rtvmediare805
      @rtvmediare805 6 лет назад

      Ongela

  • @prospermakundi2787
    @prospermakundi2787 6 лет назад +2

    Raisi wangu umenifurahisha sana,hakika unafanya kazi ya kutetea wakulima tz.

  • @agneomasonda2462
    @agneomasonda2462 6 лет назад +3

    Mheshimiwa Rais nakuombea mema asante sana Mungu akupe maisha

  • @allymichael7310
    @allymichael7310 6 лет назад +2

    Sina cha kuongeza muheshimiwa Rais wangu..mwili unasisimka kila ninapokusikiliza , unayawakilisha mawazo yangu. Mungu akulinde na kila wabaya na aina ya ubaya! Pamoja tutaijenga Tanzania.

  • @mwamengele
    @mwamengele 6 лет назад +2

    Nimejialika,..! Hehee umetisha mzazi

  • @acrestv3377
    @acrestv3377 6 лет назад +3

    Asante rais wetu kwa kuwapigania wakulima ..... Mwenyezi Mungu azidi kukuongoza

    • @talenterick4209
      @talenterick4209 6 лет назад

      Siku zote haki ikisimama malaghai wengi huumia sana wakati mwingi wanatafuta sehem wakosoe na si kutoa ushirikiano kwa yanayotendeka mh jpm pambana zid ya wanyonge usiwasikilize watakao kukatisha tamaa pambana zaid ya hapa ulipo yupo atakaye kulipa nayeye ni mwenyez mungu si mwanadam Mungu akujalie miaka mingi ili uitetee tanzania na fahari zake

  • @samiahazali2027
    @samiahazali2027 6 лет назад +1

    Mweshimiwa rais alipo xema tuzae alikuwa anamanisha angalia nchi zote zilioendelea zina watu wengi xana angalia apo wahindi wengi na angalia kwetu kira sehemu kuna duka la muyindi mweshimiwa anaona mbali xana mungu amuongoze katika majukumu yake 👍👍👍👍

  • @josephsospeter8304
    @josephsospeter8304 6 лет назад +14

    Hiki kichwa nihatari kinajua mambo mengi sana

  • @Kamikaze2910
    @Kamikaze2910 6 лет назад +4

    Daah! Mheshimiwa Rais sina cha kuongezea, Mungu akubariki sana

  • @acrestv3377
    @acrestv3377 6 лет назад +5

    Asante sana kwa yote unayoifanyia nchi yetu ..... Kipekee kabisa napenda nkushukuru kwa ujenzi wa barabara ya Mpemba kwenda Ileje unaoendelea .... Asante sana mh rais

    • @derickgambi8627
      @derickgambi8627 6 лет назад

      Hakika MUNGU alikuleta kwa kusudi maalum ubarikiwe sana

  • @iamjoseph795
    @iamjoseph795 Год назад +1

    I miss you Mangufuli. Rest in peace ✌️ byou are my hero up to now from Kenya 🇰🇪

  • @samwelmalwa9814
    @samwelmalwa9814 6 лет назад +3

    Wanaompinga Mh, JPM watapata tabu sana maana utendaji kazi wake umetukuka sana. Hongera sana JPM, juhudi zako tunaziona,tunakuunga mkono na tunakuombea Mungu akubaliki.

  • @kaizamulinda633
    @kaizamulinda633 6 лет назад +4

    Ila kumbe kuwa Rais si masihara. Nikisikiliza namna JPM anavyoongea kwa details na uelewa mkubwa wa mambo, najiuliza haya alijifunza lini. Anaongea vitu very technical kwa kweli.

  • @melickzedeckmunuo190
    @melickzedeckmunuo190 6 лет назад +1

    Mungu akubariki kwa kuwa mzalendo wa Taifa letu tunakuombea sana wana nchi wamenyonywa sana

  • @angelanather9640
    @angelanather9640 6 лет назад +2

    Yaani nikimsikia Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli natokwa na machozi kwa furaha. Kweli ni zawadi toka kwa Mungu.

  • @furahamwajeka3708
    @furahamwajeka3708 6 лет назад

    nakuelewa sana baba magu thanx maana kuongoza ni kazi sana baba piga kaziiii

  • @shukurumwangosi1537
    @shukurumwangosi1537 6 лет назад +10

    Rais wangu nchi yangu.
    Haya tunayoyaandika tunatamani uwe unasoma mwenyewe ha ha ha
    Kiukweli Raisi wangu unawapigania wakulima wanyonge kwa kiwango kikubwa sana
    Tatizo watu wako (watendaji)wanakuangusha.
    Haya mambo sasa ulitakiwa baada ya wewe kulipigia kelele mwaka Jana ilitakiwa sasa upumzike .wanakutesa sana sana.
    Lakin tutafika tuu.
    Good job JPM

  • @mswadikubushumbilo7170
    @mswadikubushumbilo7170 6 лет назад

    mzee umenifurahisha speech yako yale,

  • @paulshamba1746
    @paulshamba1746 6 лет назад +2

    Mungu akulinde maana wewe ni mtetezi wa kweli

  • @قاسممحمد-ص5ت
    @قاسممحمد-ص5ت 6 лет назад +2

    The best leader in Africa

  • @japhetmombia
    @japhetmombia 6 лет назад +1

    Mungu akulinde Mh.Rais

  • @paulchugu9198
    @paulchugu9198 6 лет назад +3

    Nyerere II in the house.

  • @raphaelpaschal7892
    @raphaelpaschal7892 6 лет назад +3

    mzee hongera sana jitahidi ufike maswa wananchi tunatahabika maji ayatoki wilaya nzima wiki ya tatu sasa fatilia mzee maji ni uhai

    • @petercosmas4376
      @petercosmas4376 6 лет назад

      Ni kweli kabisa nmetka juzi huko tabu tupu

  • @milimomashini9432
    @milimomashini9432 6 лет назад +4

    Nakupata vzur MH.Rais kutoka masharik ya kati kimsing hao wengi madalali huwa wanataka supernormal profit hayo matatzo mengi yako hata kwenye zao la ufuta na mazao mengine ya biashara

  • @salumkseleman1470
    @salumkseleman1470 6 лет назад +2

    Asante baba jkt na majesh yetu yote hata kwa mdomo👏👏👏👏😂😂😂😂

  • @siwonikewilliam8832
    @siwonikewilliam8832 6 лет назад +5

    Happy birthday Mr.President

  • @jenyyusuph4973
    @jenyyusuph4973 6 лет назад +2

    Kwaajili ya maendeleo yanchi yetu huyu baba alizaliwa mungu ulitupa Bure zawad ya jpm mlinde muongezee muda waungozi siku kwasikuamina

  • @davidandrew9575
    @davidandrew9575 6 лет назад +5

    Mnaenda kununua au hamuendi

  • @oscarmisiru9725
    @oscarmisiru9725 2 года назад

    This is the Man of Yes and No, no mbambamba

  • @makumbele
    @makumbele 6 лет назад +3

    Ukisikia Raisi basi ndio huyu.

  • @tajinehemia3961
    @tajinehemia3961 6 лет назад

    Mungu Akuzidishie Hekima Na Maarifa Raisi Wetu

  • @mswadikubushumbilo7170
    @mswadikubushumbilo7170 6 лет назад +1

    mzee tunakukubali,we ni Rais wa wanyonge,asiekubali akafie mbali,

  • @yusuphluwali5514
    @yusuphluwali5514 6 лет назад +7

    Huyu ndie aliekapaswa akabidhiwe nchi km alivyokabidhiwa rais wa China mpk afe

  • @susangibai2691
    @susangibai2691 6 лет назад +5

    Hahahaaaaaa, jkt. Mtabangua korosho kwa mdomo Kweli, chezea jembe we! Hakika Mh. Rais. Unakonga mioyo ya wakulima Mungu akuongoze baba.

  • @jerichoseth4188
    @jerichoseth4188 6 лет назад +2

    haki ya Mungu ingekuwa ni amri yangu huyu Rais angeendelea angalu hata miaka ishirini maana kumpata kama huyu tena ni mtihani japo nina amini wapo ila kumpata ni shughuli kubwa.

  • @isackjuma7973
    @isackjuma7973 6 лет назад +4

    VIVA magufuli VIVA

  • @Antibeberu
    @Antibeberu 6 лет назад +3

    Bravo JPM

  • @jacksonrwebangira9446
    @jacksonrwebangira9446 6 лет назад +2

    What a great president!

  • @sabatojoshwa6684
    @sabatojoshwa6684 6 лет назад +1

    Hadi Bodyguard ametabasamu!!! Heshima yako mzee Magufuli

  • @samwelhechei8537
    @samwelhechei8537 6 лет назад +1

    Hongera sana mkuu,

  • @ezekielnjau8830
    @ezekielnjau8830 6 лет назад +1

    Huyo ndio mh. JPM, my favourite president

  • @hilalihashimu5693
    @hilalihashimu5693 6 лет назад +1

    Mr Prisedent anglia uwezekano wa shirika la Tanganyika perkas yale maeneo ni muhimu sana kwani yamesahaulika kwa muda mrefu sana

  • @hyeragerald4442
    @hyeragerald4442 6 лет назад +3

    Nawaza cha kufanya ili kukuongezea muda wa uongozi. Hakuna namna

  • @edwinmalale1513
    @edwinmalale1513 6 лет назад +3

    ohooo hii ya kubangua kwa mdomo tusiende kichwakichwa asije akaangiza watanzania wote wabangue kwa mdomo

  • @musamakuka8319
    @musamakuka8319 6 лет назад +1

    Ibadilishwe tu katiba ya Tanzania uwendelee mbaka kuzeeka kwako ayupo mwingine wa kuvaa viatu vyako

  • @khadijaabdalla1011
    @khadijaabdalla1011 6 лет назад +3

    This is my president. ..

  • @athumanomary1438
    @athumanomary1438 6 лет назад

    Mwenyez MUNGU yupo pamoja nawe raisi wetu

  • @kareembesta1057
    @kareembesta1057 6 лет назад +1

    Good Mr president"

  • @BennyChristian
    @BennyChristian 6 лет назад +2

    Kweli kabisa wakilaza = kilaza, fukuza tu, hata hii bodi jipu tu, watu wanunue tu hata wauza dagaa wanaweza jalibisha biashara ikiwashinda watavulia samaki

  • @jumaulamba25
    @jumaulamba25 6 лет назад

    Hongera mtetezi wa wanyonge

  • @geraldlazaro4523
    @geraldlazaro4523 Год назад

    Yessssssssssssssss assessed tanzaniaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

  • @pascalgwandu1657
    @pascalgwandu1657 6 лет назад

    mungu akulinde siku zote!

  • @salimamri9488
    @salimamri9488 6 лет назад +2

    🔥🔥🔥🔥

  • @mwalamimtupa4728
    @mwalamimtupa4728 6 лет назад +1

    Jpm ever domination...we love u mo

  • @alvangidion9366
    @alvangidion9366 6 лет назад +3

    Mr president anaijua korosho

  • @allyabbas4793
    @allyabbas4793 6 лет назад +7

    Rais wa wanyonge

  • @tajinehemia3961
    @tajinehemia3961 6 лет назад

    Nakuelewa Sana Kiongozi

  • @jamesngundateresia2600
    @jamesngundateresia2600 6 лет назад +3

    BABA DUNIA ZIMA INAKUTAMANI UJUE UNA MADINI YASIYOISHA ALIKUZAAA ANASTAILI SIFA ZOTE
    DUU HATUWEZI PATA TENA MTU HUYU MIMI NASEMA
    HATA AKIPATIKANA ATAFIA TUU JANGWANI MAANA NCHI WATU KARIBIA WOTE NI WATUMWA WA WA WATU WEUPE TUU

  • @alvangidion9366
    @alvangidion9366 6 лет назад +1

    My President big up

  • @mussambilu229
    @mussambilu229 6 лет назад +1

    safisana

  • @mbwanaomary7537
    @mbwanaomary7537 6 лет назад

    Raisi bora wa muda wote

  • @michaelmrosso2106
    @michaelmrosso2106 6 лет назад +2

    😂😂 hata kwa meno jesh litabenguaa korosho..

  • @newtonmunenekaibiria6623
    @newtonmunenekaibiria6623 6 лет назад +12

    Hakika huyu ni mtetezi Wa wanyonge. Kongole Rais.

  • @suleimanbakar1271
    @suleimanbakar1271 6 лет назад

    baada yale kuongelea issue anazunguka kross

  • @Michael-dl1lu
    @Michael-dl1lu 8 месяцев назад

    ❤❤❤❤❤❤❤❤❤🎉🎉🎉🎉🎉

  • @shifumponda666
    @shifumponda666 2 года назад

    Kweli ulisema tutakukumbuka kweli nakukumbuka sasa

  • @athumanomary1438
    @athumanomary1438 6 лет назад +1

    Ewe mwenyez MUNGU tunazidi kukuomba enderea kuyapa nguvu majeshi yetu yote ewe mwenyez MUNGU mkuu

  • @yakoboisack9054
    @yakoboisack9054 6 лет назад

    jamani acheni siasa tunataka ela hadi mwezi wa kumi na mbili hatujapata ela kama hela haipo wapeni wahindi wanunue

  • @jilugalamarco9308
    @jilugalamarco9308 6 лет назад +3

    good president

  • @fbr5113
    @fbr5113 6 лет назад +1

    Nawapongeza sana Ikuilu mawasiliano pia kwa kuanzisha vyombo vyenu vya habaria na kwenda na wakati kama hivi mana hao waandishi wa TZ wengi tumeshawashtukia washanunuliwa na magaidi wa mabepari, wanakimbilia kutangaza habari za kuvuruga nchi zaidi kuliko habari za kuikomboa nchi. Watu wa hivyo wote wachunguzwe na wanyang'anywe uraia, tunataka watanzania wanaoitetea nchii kama Rr. Magufuli sio kuteketeza nchi na Wananchi.

  • @charlesmakuri792
    @charlesmakuri792 6 лет назад +1

    Wale wanao jiita wapinza huwa hawakosi kukosoa watatia ujuaji wao et wao ndio wanajua ,upinzani huu ni chuki matusi na lawama ,zito atakosoa tu

  • @singinowelnel4656
    @singinowelnel4656 6 лет назад

    Pongezi ziende kwa John

  • @maxmilliankibura1047
    @maxmilliankibura1047 6 лет назад

    Mbele itabaki kuwa mbele tu speed hainashida nakuunga mkono raisi wangu hata kama tunaspeed ndogo naamini mbele tutafika tu HAPA KAZI TU

  • @fraviansweetberty8819
    @fraviansweetberty8819 3 года назад

    Leo ih atupo nawewe Jpm pumzika kwa Amani

  • @stephenshio588
    @stephenshio588 6 лет назад +1

    Hongera President hili ndo tulikuwa tunalitaka kwa wananchi fukara

  • @elymollel
    @elymollel 6 лет назад

    Kina "Kemcho" hapo wanachanganyikiwa 😃😃thumb up jembe!

  • @ramadhanimgaya8287
    @ramadhanimgaya8287 6 лет назад

    Piga kazi Mr President, Watanzania tupo pamoja nawe

  • @isayaupson7712
    @isayaupson7712 6 лет назад +1

    Mheshimiwa tunaomba tuangalie upande wa mbaazi hali ni mbaya kilo mia mbili 200 mkoa wa manyara

  • @mochings8012
    @mochings8012 6 лет назад +2

    43:50 😅😅

  • @danielmmbaga976
    @danielmmbaga976 6 лет назад +1

    Hakika huyu ni raisi mtetezi wa wanyonge mungu azidi kukulinda mkuu.

  • @mongliclassic5642
    @mongliclassic5642 6 лет назад

    Ndomaana 2nakunda Rais. Jpm

  • @petercosmas4376
    @petercosmas4376 6 лет назад +4

    Nmeona mzee mmja kama haelewi kabisa,hahaaaa

  • @athumanomary1438
    @athumanomary1438 6 лет назад +1

    Ewe mwenyez MUNGU tunazidi kukuomba enderea kumuongoz kumsimamia kumrindi na kuzidi kuimalisha afya yake raisi wetu ewe mwenyez MUNGU pia enderea kuwaongoza vyema viyongoz wete wanaomsaidia raisi wetu turiongoza taifa retu

  • @fbr5113
    @fbr5113 6 лет назад +1

    Tawala miaka yote Magufuli, hadi hao majambazi wa mabepari wakimbie nchi, kwanza wote wale sio Watanzani wanatumwa kuivuruga nchi. Kwa mwendo huu uwezo wa kuiendesha nchi unao hata bila msaada wa wanyonyaji wa nje, sisi hata njaa tutalala mradi ututoe utumwani, kunyonywa Tanzania ibaki kuwa historia, unaonesha njia ambayo wengi walishindwa kwasababu walikwamishwa na kuwaogopa hao wahalifu wa mabepari. Magufuli oyeee

  • @nyakytito4954
    @nyakytito4954 6 лет назад +1

    nitaasisi maandamano ya kupinga kuondoka madaraka kwa anco magu bado tunakuhitaj

  • @japhetmwamlenga7078
    @japhetmwamlenga7078 6 лет назад +1

    ndo uzuri wa
    kuchagua rais msomi huwezi kumdanganya.

  • @avax5717
    @avax5717 6 лет назад

    Natamani nione jinsi jeshi linavyobangua korosho kwa meno.. Lol

  • @najimcompanyltd2096
    @najimcompanyltd2096 6 лет назад

    kama nikijana alafu huumpend magufuli inabidi ukapimwe akilii

  • @salumkseleman1470
    @salumkseleman1470 6 лет назад +1

    👏👏👏👏😂😂😂😂😂👏👏👏👏

  • @suleimanbakar1271
    @suleimanbakar1271 6 лет назад

    kigeugeu

  • @EmanuelAmosi-r4p
    @EmanuelAmosi-r4p 3 месяца назад

    chuma hiyo