SIKU 1000 ZA WATOTO 3 IRINGA /MAFANIKIO

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 19 сен 2024
  • SIKU 1000 ZA SOPHIA, VIVAN NA JOYCE- KATA UKWEGA/MAFANIKIO MIEZI 6
    Leo katika makala yetu inahusu siku 1000 za watoto 3 katika Kata ya Ukwega Wilaya ya Kilolo.
    Safari ya siku 1000 za watoto hawa zilianza mwezi Oktoba 2023 katika jengo la mama wanaosubiria
    kujifungua Kliniki ya Ipalamwa, Wlaya ya Kilolo.
    Lengo letu kurudi ni kufanya ufuatiliaji. afisa muuguzi Mkunga anasema wakinamama wote
    walijifungua salama, safari kuelekea kitongoji cha Iwanda na kijiji cha makungu katika kata hiI ya
    Ukwega, na hawa ndio watoto waliozaliwa na sasa wametimiza miezi 8.
    Wataalamu wanasema kudumaa humkosesha mtoto fursa ya kukua akiwa na afya bora, kukosa
    uwezo wa kujifunza kikamilifu na hata kupunguza nafasi ya kupata ajira akifikia umri wa
    kuajiriwa, kubadili hali hii kunahitajika uwekezaji katika siku 1000 za uhai wa mtoto.
    Wadau hawa Global Volunteers kupitia wafanyakazi na watoa huduma waliopatiwa mafunzo
    stahiki, wanafanya kazi kubwa vijijini kwa kutoa mafunzo kwa wazazi juu ya malezi bora katika
    hizi siku elfu moja
    Maendeleo ya nchi yanategemea watu wenye uwezo kiakili, na inawezekana. Tanzania, kama
    nchi, kuwa na mamilioni ya watu wenye uwezo wa kiakili inawzekana. Serikali na wadau
    inatekeleza Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto,
    Mtazamaji sisi makutano TV tunaahidi kuendelea kufuatilia safari ya siku 1000 za watoto hawa
    Sophia, Vivan, na Joyce hadi watakapotimiza siku 1000, kumbuka kuwa ukuaji vema wa
    ubongo unahitaji lishe bora, huduma bora ya afya, mawasiliano chanya, na mazingira salama.
    mimi ni Tukuswiga Mwaisumbe

Комментарии • 4

  • @temmymahondo4387
    @temmymahondo4387 2 месяца назад +1

    Safi kazi nzuri

  • @sophiampunga6016
    @sophiampunga6016 2 месяца назад +1

    Hongera sana madam CEO hakika utalipwa usipozimia moyo. Kazi nzuri sana kongole MAKUTANO TV TEAM

  • @martinhipolitichuwa366
    @martinhipolitichuwa366 2 месяца назад +1

    Mtoto anapendeza sana. Hongereni sana Team tuendelee kuchapa kazi hii njema ya Mungu hadi tupate watoto bora watakaoweza kufikiri vyema na kubadili kabisa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya taifa hili.

  • @MwanaidiBrown
    @MwanaidiBrown 2 месяца назад +1

    RCP Program at Global volunteer inafanya kazi kubwa, Kudos kwao. Hongera kwa team Nzima ya MAKUTANO TV nyinyi ni wadau wa muhimu sana kwa Mkoa wa Iringa na Tanzania kiujumla.