KAMPENI MAALUM IRINGA

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 19 сен 2024
  • KAMPENI MAALUM IRINGA
    Mtazamaji wa Makutano TV karibu, hii ni ripoti maaalum kuangazia UTATUZI WA MFUPA MGUMU TATIZO LA UDUMAVU MKOA WA IRINGA.
    Mnamo tarehe 20 mwezi Machi mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Peter Joseph Serukamba, alitoa rai kwa viongozi na watendaji kujipanga kutatua KERO za wananchi huku akieleza wazi kukerwa na mfupa wa KERO ya Iringa kuongoza kwa UDUMAVU kwa watoto chini ya miaka 5.
    Mhe Serukamba ameanza kutekeleza adhima yake yenye dhamira ya uwazi wa uwajibikaji wa kutatua KERO hii kwa vitendo, tarehe 10, Julai ametangaza kuanza kwa siku 4 za KAMPENI MAALUM YA KUTATHIMINI HALI YA LISHE KATIKA MKOA WA IRINGA yenye kauli mbiu “ mtoto kwanza udumavu unazuilika”
    Hii ni moja ya kaya Mkoani hapa, yenye changamoto ya mtoto mwenye utapiamlo mkali, kwa kipindi kirefu makutano TV kwa kushirikiana na serikali ya mtaa na mtoa huduma ngazi ya jamii, tumefanya ufuatiliaji wa mara kwa mara wa maendeleo ya mtoto huyu, changamoto ya mahudhurio duni ya kliniki, unyonyesheji usioridhisha na lishe kwa mama isiyoridhisha, mtoto kutonyonya ipasavyo yamkuwa matatizo ya kujirudia kwa mtoto huyu, na leo tumefika hapa tena, kuona je kampani hii maalum imeifikia katika kaya hii?
    Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa wa Iringa, mkoa una watoto zaidi ya laki 2, na hii ndiyo idadi ya watoto wanaotarajiwa kufikiwa katika kila halmashauri.
    Hapa ni ofisi ya kata ya Mwangata, kata ambayo inaongoza kwa ukubwa katika Manispaa ya Iringa
    Nimefika pia mitaa ya ipogolo hiki ni kituo kimojawapo katika kata ya Ruaha hapa pia wazazi wamehamasika wakiwemo pia kina baba
    Septemba 2022 Rais Samia Suluhu Hassan aliagiza kufanyiwa mapitio kwa Sera ya Lishe ya Mwaka 1992, si hivyo tu bali pia aliweka saini Mkataba wa Usimamiaji wa Shughuli za Lishe na mkataba huo huo wakuu wa mikoa walisaini na wakuu wa wilaya na kushusha kwenye ngazi ya Halmashauri, hapa Iringa Mkuu wa Mkoa uliwasainisha wakuu wa wilaya tarehe 24 Oktoba 2022. Ungana nasi katika ripoti inayofuata ili kujua matokeo ya kampeni hii.

Комментарии •