BARAZA LA WATOTO IRINGA DC

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 19 сен 2024
  • Kuelekea siku ya Mtoto wa Afrika, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imezindua BARAZA LA WATOTO kutoka kata 28 kwenye Halmashauri hiyo.
    Mkuu wa Idara ya ustawi wa jamii Bi Saumu Kweka anaeleza lengo la mabaraza haya
    Mwakilishi wa Baraza la Watoto aliyemaliza muda wake Schola Mwakilisa ameeleza changamoto walizokutana nazo wakati wa uongozi wao kuwa ni pamoja na kukosekana kwa utayari na ushirikiano katika ngazi ya familia
    Chimbuko la siku ya mtoto wa Afrika ni azimio lililopitishw mwaka 1990 kuwakumbuka watoto wa Kitongoji cha Soweto Afrika kusini waliouawa 1976 kutokana na ubaguzi wa rangi, watoto hao waliuawa wakidai haki za kibinadamu ikiwemo haki ya elimu bora, katika kikao cha uzinduzi wa baraza hili inaibuliwa hoja ya adhabu ya viboko na ukatili kwa watoto.
    Maadhimisho haya ni fursa ya kutathimini utekelezaji wa Sera za Taifa zinazohusu maendleo ya watoto kwa kuwapatia huduma stahiki.
    #mtotokwanza
    #pjtmmmam
    #sikuyamtotowaafrika2024
    Endelea kufuatialia Kampeni hii kupitia kurasa zetu hapa
    MAKUTANO TV.

Комментарии •