Ambwene Mwasongwe - Nimeachilia (Official Music Video)

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 9 ноя 2024

Комментарии • 1,6 тыс.

  • @saraphinajohn9112
    @saraphinajohn9112 Год назад +16

    Tuliopona kupitia wimbo huu gonga like hapa mungu akubaliki ambwene🙏

  • @rachaelyusuph8492
    @rachaelyusuph8492 Год назад +25

    Wimbo unaponya maumivu yotee mtu aliyo nayo Moyoni.Mungu akubariki sana Una sehemu yako peke Yako peponi.Hunaga wimbo usio na maana kwenye maisha ya watu umezaliwa kwa Makusudi Libarikiwe Tumbo La mama yako aliyekuzaa🙏🙏🙏🙏

  • @matthewjames3380
    @matthewjames3380 6 месяцев назад +18

    Huu wimbo ulitia moyo Sana wakati nimeachwa kwa mara ya kwanza nauskiliza niliurudia rudi sana kwasababu sku naachwa ndio siku ya kwanza nauskia nikajiuliza kwani huu wimbo nimetungiwa Mimi au!!! nilihakikisha napata namba ya Huyu Muimbaji nikampigia akanitia moyo nikapona Mungu Akuinue Sana Baba yangu @AmbweneMwasongwe

  • @FurahiniSanga-i4h
    @FurahiniSanga-i4h 2 месяца назад +9

    Nimeachiria kabisa kutoka mume nilie mpenda sana kanitelekezea watoto3na mimba ya4 na kutokujali familia yake kabisa na sasa nimesikia wimbo huu nimeinuka tena nimesamee nimeachiria ee Mungu nisaidie nilee watoto wangu

  • @beatricekalisti3372
    @beatricekalisti3372 Год назад +49

    Yani nimeusikiliza huu wimbo hadi nimeamua kubadili maisha nimemrudia mungu nilikua sifai kabisa ameen ubarikiwe kaka ambwene🙏

  • @jacksonmrema4737
    @jacksonmrema4737 Год назад +13

    Mungu naomba unisamehe na unisaidie pale mm nilipokuwa sababu ya yeyote kuimba wimbo huu aachilie awe na amani, naomba Umpe nguvu na usimame naye awe imara kama Tai...Na mm nimeachilia kwa Machozi moyo wangu usahau, Mungu naomba Unipe Nguvu. 08 August 2023

  • @mercynnko3416
    @mercynnko3416 Год назад +256

    Nimepitia mazito for the past three months I lost my son after three day of delivery mwanaume alinitesa sana nilikua nimesema siwezi pona kutoka kwenye ile experience but Thank God nipo sawa nimepata amani ya moyo baada ya kuachilia kila kitu Mungu Akubariki Ambwene Nice Song

  • @jacksonygodiwe7417
    @jacksonygodiwe7417 Год назад +8

    huu wimbo Like umeniimbia mimi, Ahsante sana Mtumish wa Mungu, Yesu akutunze sana

  • @allenangumbwikewillieson6178
    @allenangumbwikewillieson6178 Год назад +29

    Lyrics!!!
    Ulipanda mti mzuri ukategemea kuvuna matunda,
    Ila mti wenyewe umezaa miba na michingoma,
    Uliwekeza muda na mali ukamwagilia ukitarajia,
    Matarajio yamekuwa sio sasa umebaki na maumivu,
    Japokuwa uliiona miba ulijipa muda ukapogolea,
    Ulitarajia mabadiliko ladba kesho mti utazaa,
    Sasa imekuwa kinyume mti wako mwenyewe unakuchoma!
    Unaliaa aaaaaaahh!
    (Ukimbuka mbegu)
    Unaliaa aaaaaaahh!
    (Ukikumbuka maji uliyo mwagilia)
    Unaliaa aaaaaaahh!
    (Ukikumbuka kazi uliyo wekeza)
    Sio kila kinacho kuja kwako ni chako,
    na si kila kiondokacho kwako ni chako,
    Hata kama unavipenda sio vyako,
    Vingine Mungu huviondoa ili wewe ubaki salama,
    Iwe kazi, nafasi, mahusiano au cheo,
    Japo vyaondoka kwa maumivu,
    Ila jifunze kuviacha viende,
    Nafasi ya moyo wako mpe Mungu.
    Chochote kile kikuumizacho
    Kufikia hatua ya kukua,
    Jua ulikikalisha mahali Pa Mungu!
    Jifunze kukiacha kiende,
    Jifunze kusema bye bye,
    Maana sio vyote vyakwako!
    Walitoka kwetu hawakuwa wakwetu,
    Maana wangekuwa wetu wangelikaa nasi,
    Walitoka ili wafunuliwe sio wote wa kwetu!
    Walitoka kwetu hawakuwa wa kwetu,
    Wangekuwa kwetu wangelikaa nasi,
    Walifunuliwa ili tujue sio wote wa kwetu!
    Eeeeh! Eeeeh!
    (Nimeachiliaaaaa)
    Aaah! jifunze kuuambia moyo wako…
    (Nimeachiliaaaa)
    Hata kama inauma sana jifunze kusema…
    (Nimeachiliaaaa)
    Eeeh! nimesamehe Mungu anaona mimi,
    (Nimeachiliaaaa)
    Tafuta mahali pa pekeyako,
    Mahali hakuna akuonae,
    Mahali pa siri pa utulivu,
    Mahali hakuna akusikiae,
    Ukakumbuke machungu yako,
    Maumivu yako na machozi yako,
    Ukayakumbuke maneno yote,
    Yakuumizayo moyo wako,
    Ukakumbuke vitu ulivyo poteza,
    Kakumbuke muda na watu wa karibu,
    Kakumbuke hasara uliyo pata,
    Usiyasahau machungu yoyote,
    Lia usibakishe machozi,
    Lia usiyameze yoyote,
    Toa yanayo uthibu moyo,
    Toa yasibakie yoyote!
    (Aaaaah!!! Aaaaah! Aaaaah!)
    Toa usibaki na machungu,
    Hakikisha umetuliza moyo,
    Umesahau yote yaliyo pita,
    Achilia wote ulio shikilia,
    Waache waende si riziki yako,
    Hakikisha umekuwa mwepesi,
    Ji’editi moyo ubaki salama,
    Inuka sema kwa ujasiri,
    Nimeachilia ninaanza upya,
    Inuka jikung’ute mavumbi,
    Yakale yamepita sasa ni mapya!
    Nimeachiliaaa semaa,
    Nime achi lia!!
    Nimeesamehe yote,
    (Nimeeachilia)
    Nimejinyonyoa manyoya ya kale,
    Sasa ni mwepesi (Nimeeachiliiia) nimeota mapya,
    Aaaaah! Aaaaah! Aaaaah! Sasa niko huru,
    Nina luka luka na maisha mapya,
    Nimeeachilia
    (Nimeeachilia)
    Nimesamehe sasa ninayo amani,
    Ooh ooh Oooh
    Maumivu ya kale nimeyaacha nyuma.
    Nimeeachilia!!
    Yooow! Nimefunguliwa, nimewekwa huru, nina amani Bwana kaniwezesha!! Yooow! Yooow! Yooow! Sijinyongi tena, sijiui tena! Bwana Yeye ni Bwana wangu wa moyo wangu! Yooow!!

    • @yonasingooi7458
      @yonasingooi7458 Год назад +1

    • @enjoysabuni3635
      @enjoysabuni3635 Год назад

      🙏🙏🥰🥰🥰

    • @barakamwakajumba
      @barakamwakajumba Год назад

      Ambwene umebarikiwa Kwa wimbaji napenda wimbaji wako saana yaan tangu nimeanza kusikiliza nyimbo zako nabarikiwa sana nataman siku moja nijekua kama wewe, Mungu aendelee kukubaliki.

  • @mfariji
    @mfariji Год назад +1

    Nimelia sana nikiangalia wimbo huu. Hujapitia usaliti, huwezi kujua maumivu yake. Kuachilia ni muhimu lakini sio rahisi kabisa. Mungu atusaidie, tuachilie. Nahisi nahitaji kujifunza kuacha viende, nahisi nahitaji kupata mahali pa peke yangu, mahali pa siri, pa utulivu ambapo hakuta kuwa na anisikiaye, nilie tu, nisamehe yote, nikakumbuke machungu yote, nikayatoe yote, nikaachilie wote walionisibu moyo, nikayatoe machozi yote niweze kusema nimeachilia. MUNGU NISAIDIE.

  • @jaccquelinemakungu1777
    @jaccquelinemakungu1777 3 месяца назад +8

    Huu wimbo naona nimetungiwa Mimi maana nilikuwa naishi kwenye maumivu nashindwa kutoka siku natoka ndio naona wimbo unapigwa duuh si mchezo ku move on na watoto 3. Nimeachilia Sasa I'm so happy nime edit moyo kwa kweli

  • @emmymwanjala2788
    @emmymwanjala2788 10 месяцев назад +5

    Huu wimbo nimeuona live ktk maisha yangu mwaka 2023. Namshkuru Mungu alinivusha salqma ktk kipindi cha msongo wa mawazo. Amina.. nimesamehe Mungu anaona

  • @sharonlivingstone9415
    @sharonlivingstone9415 6 месяцев назад +12

    I remember I had pregnant,,lakini jamaa alikata kiukweli nilipata maumivu makali maana ckuwai waza kwamba hili jaribu lingenipata,,after some time due to stress while I was pregnant nilipata shida kiafya nikazaa wakati ambao sio na mtoto hakueweza kusurvive for long,,japo nilikimbiwa huh wimbo utanipa ujasiri wa kusame na kusau na kupata mwanzo mpya,,ubarikiwe sana

  • @cleveraziz1673
    @cleveraziz1673 Год назад +1

    Uuuuu wimbo visa vinafanana na vyangu nimeachiliaa nafasii imebakii kwakoo mungu , gospel upande juuu ihubiriwe injilii

  • @tumainielmaruwa3148
    @tumainielmaruwa3148 10 месяцев назад +6

    Huu wimbo umenikumbusha mbali sana alikuja kama mti wa matunda mazuri ila wanadam wakasimama hata wale walikuwa karibu pia wakawa wanafiki kumbe wanalao jambo. Kweli sio Kinachokuja kwako ni chako maana Mungu aweza kuwa na njia zake. Nikweli ukiona jambo lakuuma ujuwe umelikalisha mahali pa Mungu. Yusuf ktk nyumba ya Potifa alipotezwa kwa kumkatalia Boss Mungu akampa muujiza wa Uwaziri Mkuu akitokea gerezani😭😭😭🙏🙏🙏

  • @MariaWaYesu
    @MariaWaYesu 5 месяцев назад +10

    Ninapitia Wakati Mgumu Sana ambao Sijawahi pitia katika Maisha yangu tongue nizaliwe, YESU nishike Mkono Usiniache, Ukiniacha Ndo mwisho wangu BABA 🙏🙏😭😭😭😭

  • @JoyceChristopher-d9x
    @JoyceChristopher-d9x Месяц назад +5

    Nimeachilia na naanza mwanzo mpya machungu yame nifanya niwe karibu na mungu

  • @babygwede4982
    @babygwede4982 Месяц назад +3

    NIMEACHILIA ❤ ASANTE MUNGU KWA UPONYAJI NA KUNIINUA KATIKA MAISHA YANGU NILIHISI NDY MWISHO WANGU, KUMBE MUNGU ULIKUWA NDY UMEANZA KUSHUGULIKA NA MAISHA YANGU VYEMA❤ ASANTE MUNGU WANGU NAKUPENDA ❤ KILA ASOMAE MUNGU AKUPIGANIE AKUTUNZE AKUPE KILA HITAJI WAKO. WEWE NI WA THAMANI SANA MBELE YA MUNGU USIJICHUKULIE POA KABISA

  • @ivvansiwiti9085
    @ivvansiwiti9085 Год назад +29

    AMBWENE WEWE MUIMBAJI WA MFANO NIMEJIFUNZA KUJUA HII 🙏🙏

  • @kashindiseti4493
    @kashindiseti4493 Год назад +2

    Therapy❤️🙏.
    Nimeachilia; Jehovah wewe wajuwa❤️🧎‍♀️🙏

  • @amosizebedayo9190
    @amosizebedayo9190 Год назад +85

    Hakika wote walio niumiza nimeachilia 🙏😌 ubarikiwe Mtumishi Ambwene

    • @faustinammilla757
      @faustinammilla757 Год назад

      Uwiiii nimemuumiza mtu but still nampenda

    • @farajahalenko924
      @farajahalenko924 Год назад

      Amina mtumishi wa bwana,barikiwa sana🙏🙏kwa wimbo mzuri hakika nimebarikiwa sana pia nimejifunza kupitia wimbo huu kuachilia napitia mambo mengi ila mungu akanifunge mkanda kupitia wimbo huu.

    • @innocensiamwabena3787
      @innocensiamwabena3787 Год назад

      Nimebarikiwa mno

    • @agathasungura5047
      @agathasungura5047 Год назад

      Hii nyimbo sichoki kuisikilizaa

    • @amosizebedayo9190
      @amosizebedayo9190 Год назад

      @@agathasungura5047 hakika

  • @preshTzpreshTz553
    @preshTzpreshTz553 Год назад +7

    Nenda Joachim sitaki tena nikufikilie maisha yangu yote hata kama nipo kwenye mji wenu hata nikikuon uwe wa kawaida sana naachalia kila kitu

  • @chimsmulumbi8937
    @chimsmulumbi8937 Год назад +6

    Ni kama Roho wa Mungu aliniongoza nipate wimbo huu... Two days ago nilifiata hubiri kuhusu Kusamehe, I told to God that I want but sina nguvu ya kuachiliya... Ndipo wimbo huu nikaupata. Kwa hakika nnimehudumiwa n'a Roho wa Mungu kupitiya wimbo huu...

  • @mdoefernandes5442
    @mdoefernandes5442 Год назад +1

    Im Muslim but hii nyimbo haitaji ITIKADI KALI saana kusikilizaa ujumbe mzuri saaana

  • @janethmabwa1012
    @janethmabwa1012 Год назад +44

    ubarikiwa sana mtumishi ,nimepita kipindi kigumu sana nusura ya kupoteza uhai wangu ,wimbo huu ni kama Mungu amekutumia uutoe wakati huu kwaajili yangu mtumishi ...Amen nimebarikiwa na nimejifunza kua kumbe sio vyote ni vya kwetu na vinavyoondoka kwetu sio vyetu na nafasi ya moyo wangu nimpe Yesu🙏

    • @wistonbigera989
      @wistonbigera989 Год назад

      Pole Sana, trust in God

    • @afcambassador4566
      @afcambassador4566 Год назад

      Pole sana

    • @anusiatamichael1957
      @anusiatamichael1957 Год назад +1

      Umesema kweli..

    • @jamesfanuel4595
      @jamesfanuel4595 Год назад +3

      1 Yohana 2:19 Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.

    • @janethmabwa1012
      @janethmabwa1012 Год назад

      @@wistonbigera989 ahsante amina

  • @sophiakyalo1
    @sophiakyalo1 2 месяца назад +7

    Amen🙏🙏🙏🙏 After suffering for months finally my heart is at peace 🙏🙏🙏🙏🙏 si rahisi but let them go , achilia everything that is hurting you and tormenting you , may we all fine peace

  • @Susy0610
    @Susy0610 Год назад +75

    This is what we call Ministry, barikiwa Mtumishi
    Kwa kweli nimeachilia 🙏🙏

    • @jiskakablack3402
      @jiskakablack3402 Год назад +1

      Ambwene, kweli vita Yako ni kubwa anayekupambania ni mkubwa Sana. Huu wimbo umepambana ndgu .sijui ilikuwaje ila naamini ubora huu wimbo ni ukubwa wa vita na mzigo ndani Moyo

    • @deborajoseph5270
      @deborajoseph5270 Год назад +1

      Nimeachilia hata Kama kinauma😭, barikiwe mtumishi

    • @Susy0610
      @Susy0610 Год назад +1

      Ingawa ni uchungu na inauma, itabidi tuachilie ndio Yesu Kristo akaweza kuponya mioyo yetu. Let go and let God
      Shalom

    • @jp.productionpasho6893
      @jp.productionpasho6893 Год назад

      How How 7th is 0

  • @mercykasyoka4007
    @mercykasyoka4007 Год назад +6

    Mpenzi wangu ndiye amenitumia wimbo huu na anadhani mimi smpendi sasa ameenda naomba mungu amrudishe kwangu kwa utukufu wa Mungu 😢😢😢😢

  • @yohanaagastinymasumbuko8181
    @yohanaagastinymasumbuko8181 Год назад +356

    Jamn ambao tumesubilia kwa ham gonga like bas

    • @yohanaagastinymasumbuko8181
      @yohanaagastinymasumbuko8181 Год назад +2

      Namshukul mungu man Badi namtegemea ataniinua na mm mana naipenda hii kaz

    • @dynesssanga1948
      @dynesssanga1948 Год назад +2

      Haleluja nimejifunza kusema byebye

    • @wilsonemanuel9915
      @wilsonemanuel9915 Год назад

      Ulipenda mti mzuri ila siyo chako, Napenda sana kaka nyimbo zako

    • @wilsonemanuel9915
      @wilsonemanuel9915 Год назад

      Na mm nimeachilia

    • @estamichoromichoro5634
      @estamichoromichoro5634 Год назад

      Hata nami naachilia kwa jina la YESU. Naamini kwa neema ya Mungu nitapata mme ambaye yuko sahihi kwangu naomba na kuamini AMINA 🙏

  • @pascallyaruu
    @pascallyaruu Год назад +2

    Kwa huu wimbo kuna jambo inabd niachilie maisha yasonge, siyo kwa Maisha haya aisee,ahsantee Ambwene mwasonge umenifar sanaaaaa sanaaa.Amina mtumishi.

  • @gotafostv7305
    @gotafostv7305 Год назад +35

    Mtumishi Ambwene nimekuelewa sana baba ,nakujua kuwa ni mtu wa point(hoja) nzito sana zenye fikra na tafakari za rohoni sana ,mimi huwa nasikiliza nyimbo zako kwa umakini mkubwa,neno hata neno ,kwa mfano kwenye huu wimbo nimenukuu neno zito sana ulilosema (NIACHILIE KWAKUWA HAWA WALIOONDOKA WALICHUKUA NAFASI YA MUNGU) ,Kumbe hiyo nafasi ilikuwa akae Mungu ,lakini cha ajabu nilimkaisha huyo mtu,nimeelewa kwakuwa mimi ni moja ya vijana niliyesaidia sana watu wengi sana kumjua Mungu na kuwagharamikia sana,kiasi cha mimi kuishi maisha magumu sana,lakini waliniacha na kuondoka ,aiseeh nimebarikiwa na kuelewa sana ujumbe huu

  • @mbalilax162
    @mbalilax162 Год назад +83

    It's not just a song, it's a therapy📌

  • @surendereka5982
    @surendereka5982 Год назад +5

    Huu wimbo Mungu ameuleta ili useme nami, NIMEACHILIA NA NIMESAMEHE, ninaimani YESU atalejesha yote maradufu🙏🙏🙏🙏🙏

  • @invocavitmbise5296
    @invocavitmbise5296 Год назад +1

    MUNGU huviondoa ili ubaki salama.....!!!🎤

  • @lilianokomba1607
    @lilianokomba1607 Год назад +7

    Nimeurudia huu wimbo almost 100 times. Si shibi kuusikiza. Thank you for using your talent to bless us. Beautifully done.

  • @rosemuhandoofficial5676
    @rosemuhandoofficial5676 Год назад +1

    Kakangu ubarikiwe kazi nzuriungu akutunze sana

  • @UweraPeruth-tw2hz
    @UweraPeruth-tw2hz Год назад +7

    huu wimbo ulinigusa moja kwa moja nilipo pitia mambo magumu yakumpoteza my first born wangu 😭😭😭

  • @anethturinge2472
    @anethturinge2472 11 месяцев назад +5

    Nilikua na mwanaume nampenda sanaa lakn aliniumiza sanaa nilikua nafikilia adi kujiuwa lakn kupitia hu wimbo nimejifunza kuachilia sio kilakinacho kuja kwako ni chako balikiwa🙏🏼mtumishi🙏🏼 wa mungu kwakweli nimeachilia sijiuwi tena🙏🏼

  • @liannsambu7264
    @liannsambu7264 7 месяцев назад +5

    Ila kwenye hii Dunia jamani , hapana hapo ndipo unaona Bora kuwa pekeyako na YESU TU , Maana people mmmmm hapana jamani

  • @juliekahambu7474
    @juliekahambu7474 Месяц назад +4

    Mungu wezeshe kuachiliya kwani maumivu yamenjaa moyo

  • @berthabraison7979
    @berthabraison7979 11 месяцев назад +6

    Umenibariki sana mtumishi nilifiwa na mchumba wangu 😢 sijakaa vzr Mama yangu mzazi sina Baba hatasikuwahi kumuona leo Mama nae Ameniacha nililia nilipousikia Wimbo nililia sikubakiza machozi namshukuru Mungu

    • @selinagwandu8183
      @selinagwandu8183 11 месяцев назад

      Pole dear

    • @JosephatBalikulije
      @JosephatBalikulije 10 месяцев назад

      Mungu ni mwanifu nilifiwa na baba na namiaka 13 na baada ya miaka 6 mama kututoka na nyuma yangu watt wa 5 Mimi nilibaki baba na mama wa wadogo zangu niliumia kupita kawada,wimbo huu wanipa faraja tunashukuru Mungu tuna ishi vyemaa ko wimbo huu uwe faraja kwa wote

    • @lisserbrown9304
      @lisserbrown9304 2 месяца назад

      Hugs 🫂 dear Mungu akupe faraja kuu

  • @majormanaseh5668
    @majormanaseh5668 Год назад +32

    "Sio kila kinachokuja kwako ni chako" this part went deep down in me🤲🥹🥹

  • @siscoministry8400
    @siscoministry8400 Год назад +42

    Mtumishi wa Mungu .... I declare you are the best song writer in Tz....this is healing song...🔥🔥🔥...no one expected ....huu wimbo ni Balaa... Umechana( Rap) 😂🙌🏿🙌🏿🙌🏿..... Walitoka kwetu ,hawakua wa kwetu..wangekua wa kwetu wangelikaa kwetu ..walifunuliwa ili tujue sio wetu 🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿,
    Umebarikiwa Sana Daddy Ambwene Mwasongwe.🤴🏾

    • @JoyceAmlima-mg4hl
      @JoyceAmlima-mg4hl Год назад

      Hiyo Rap from 1 Yohana 2:19
      & Ambwene yupo vizuri abarikiwe

  • @gaspersafari3816
    @gaspersafari3816 2 месяца назад +9

    Huu wimbo unaponya moyo

  • @neykidoti102
    @neykidoti102 Год назад +4

    Message nzuri sana ubarikiwe mtumishi wa Mungu Ambwene

  • @carlowilly1600
    @carlowilly1600 Год назад +2

    nimeachilia ee bwana kama ni mahusiano n ndoa vtkuja kwa wakat wake

  • @tukuyufm
    @tukuyufm Год назад +7

    wimbo huu umeshirikisha kila tarajio la fikra zetu, na ndiyo maisha ya kila mmoja, "mtumishi anaimba universal lessons - mafunzo yanayolenga kila mtu duniani. katika umbo la ndani Napendelea sana maudhui ya mguso wa roho unayoifanya ( fikra + utashi wa kuamua mema). Hakika mungu amekupa mbio za akili kwa urefu na upana wa kuzikatiza fikra za jamii kwa nyimbo za FARAJA ZINAZOTIBU MATUMAINI kwa ukubwa nyimbo ulizoimba tunaishi nazo kilasiku zinaachilia bado mienendo mizuri. Mungu akubariki sana namwomba mungu aibariki familia ya mwamlenga kwa kazi njema ya mungu unayoitumikia hapa duniani.

    • @emmanueljacobo-iy5sf
      @emmanueljacobo-iy5sf Год назад +1

      Hakika

    • @tukuyufm
      @tukuyufm Год назад +1

      @@emmanueljacobo-iy5sf mfumo wa muziki wa injili unatupa faraja na MATUMAINI yenye uhakika. Tupo hapa duniani tumezingirwa na hali zinazojiri katika miguso ya huzuni, masononeko, chuki, na kujikatia hamu ya kuendelea kuishi. Pamoja na miguso ya furaha, amani na upendo ambapo ndio mahali sahihi pa kuishi kwa macho ya elimu ya nje.

    • @tukuyufm
      @tukuyufm Год назад

      ndugu @@emmanueljacobo-iy5sf tunahitaji sana elimu ya ndani (elimuyaroho) kuzistahimili hali pasipo kujali utegemezi tuliouwekeza awali .

  • @MariamHassan-j4g
    @MariamHassan-j4g 22 дня назад +2

    Mungu akubaliki mtumishi maana maumivu ya kumbeba mtu moyoni yamenitesa sana 😢😢😢

  • @mathewmassawe5982
    @mathewmassawe5982 Год назад +5

    Ameeen!! Nimeachilia,! huyu ndo AMBWENE MWASONGWE! MUNGU akubariki sana kwa ujumbe huu mzuri, MUNGU aendelee kukutunza kwenye huu utumishi wa kumuimbia, uendelee kumuimbia kwa uzuri na utakatifu.

  • @sarahmmbando2467
    @sarahmmbando2467 Год назад +1

    Ni Mungu tu anajua 😢nimeachilia imeniponya 🙏🏻😭Utukufu kwake aliyeweka huduma hii ndani yako

  • @mwajumabinwa604
    @mwajumabinwa604 Год назад +4

    nime barikiwa sana na mwibo huu mpaka naurudia kusikia kila nikiweka nyimbo ata nikiwa nafanya kazi nasikia moyowaku unaimba mwibo uhu bila kutarajia 🙏🙏💯💯 Mungu akubariki mtumishi amen.

  • @TynaRichard
    @TynaRichard 7 месяцев назад +2

    Nakupenda Sana huu wimbo unanigusa

  • @BenedictoMahilane
    @BenedictoMahilane Год назад +5

    Naenda kuachilia kusamehe kutoka moyoni stalia tena nimekusamehe mme wangu nilikubeba moyoni nenda uweda mm sio fungu lako

  • @roseasimwe827
    @roseasimwe827 Год назад +4

    Walitoka kwetu hawakuwa wetu wangekuwa wetu wangekaa kwetu amen, ubarikiwe mtumishi

  • @mikenickson6585
    @mikenickson6585 Год назад +7

    Imenichukua takribani miaka 2 lakini baada ya kuskiliza hii nyimbo nimepata mwanzo mpya ......Nimeachilia mimi nimesamehe 😭😭😭ijapokuwa ilikuwa ni ngumu maumivu makali sana lakini leo nimepona

  • @witymazubu2977
    @witymazubu2977 Год назад +6

    2023 huu nilianza vyema lakin katikati ya mwaka nilipitia magumu ambayo nilisema mungu hichi kikombe kwangu kikubwa sana kupoteza nyumba ,kazi ,mume , biashara kuanza moja siyo jambo rahisi tena kwa mara moja ila siku nasikia hi nyimbo nilijipiga kifuwa nikasema nahitaji kuachilia na kushukuru paka leo November 3 nasema mungu asante sana niliachilia ukanipa mwanzo mpya

  • @dashconceptz
    @dashconceptz Год назад +29

    100% Ministry When you know the assignment and the One who has called you for His purpose you do not worry about views but you just worry about fulfilling His will. May God remember you man of God

  • @MirryKirungi-u2p
    @MirryKirungi-u2p 9 месяцев назад +3

    Duh ni mara ya kwanza leo nausikiliza huu wimbo nimefiwa na Bibi yangu kipenzi nilikuwa na maumivu makali coz nilimpenda sana Bibi yangu alikuwa zaidi ya rafiki iliniuma sana nimeachilia Asante Kaka ambwene kwa nyimbo hi imenifariji

  • @yustomwaisomania2587
    @yustomwaisomania2587 Год назад +3

    Kuna waombaji Alaf Kuna Ambwene mwasongwe/Mwamlenga🙏🙏🙏 our gifted gospel singer

  • @jovinmwesige8520
    @jovinmwesige8520 Год назад +5

    Ambwene Bwana akutunze,nawe uutunze moyo wako usije ukamwacha Bwana kwa namna yeyote.kama waimbaji wenzako wanavyozidi kumwacha kila siku,ili uendelee kuimba nyimbo zenye Roho wa Mungu ndani yake.Hakika zinatubariki sana.

    • @frida-oi6kw
      @frida-oi6kw 2 месяца назад

      Umewaona wanavyomuacha Mungu??

  • @witnesmkemwa2562
    @witnesmkemwa2562 9 месяцев назад +4

    2023naona umekuwa mwaka wa shetan🙏🙌🙌nilipitia magumu sana😭😭but mapenz Yana changamoto sana🙏🙏ILa nyimbo hii ilinipa moyo sana

  • @mabulaamos9256
    @mabulaamos9256 Год назад +1

    Kaka napenda unavyopangilia maudhui yako na uimbaji wako, Mwenyezi Mungu azidi kukubariki sana.

  • @apostlejoshuakuhanda5524
    @apostlejoshuakuhanda5524 Год назад +39

    My brother Ambwene. Thank you for this deep message. Your song and the message in it has healed and restored my heart. I'm a new person. I cried out for help and now through this song I realise that the lord God has heard my prayer. May you be more anointed and live long in his presence. Amen Amen Amen

  • @kwilasajunior5367
    @kwilasajunior5367 2 месяца назад +5

    KUNA NYAKATI TUNAZIPITIA HAKIKA HUU WIMBO UNAKUPONYA KABISA 🎉🎉🎉

  • @carolinejohn9201
    @carolinejohn9201 Год назад +4

    Kwakweli inatupasa tuachilie ili Mungu Ainue ukuu wake ndani yetu 🙌🏾🙌🏾

  • @marthakambona87
    @marthakambona87 Год назад +1

    YESU utuhurumie utufunulie vilivyo vyetu😭🙌

  • @eunicenyaboke86
    @eunicenyaboke86 Год назад +12

    najuwa na nimeamini Mungu uko na sababu na mimi huu wimbo umenipata wakati wa machozi 😭😭wacha nilie yote kisha niwachilie 💔🙌 ahsante mtumishi wa Mungu umenifunza kitu 🙏

  • @JoyceAmlima-mg4hl
    @JoyceAmlima-mg4hl Год назад +10

    🙏🙏🙏 huu wimbo umenigusa sana ni maisha yangu kabisa.... Ubarikiwe sana ambwene ♥️♥️♥️ nikweli vingine Mungu huviondoa Ili tubaki salama.

  • @iddymwakapugi7894
    @iddymwakapugi7894 Год назад +11

    Hakika Mungu ni Mwema sana wimbo mzuri sana na hakika tumebarikiwa sana🙏🙏

  • @bonifacelutumo1196
    @bonifacelutumo1196 Год назад +3

    Huu wimbo umetaja Kila kitu kunihusu Asante yehova Kwa uzima Asante pia Kwa mtumishi

  • @sir_niccobrian
    @sir_niccobrian Год назад +11

    The wait is a finally over
    Kenyans 🇰🇪🇰🇪leave a Like and show this Great Man Of God love

  • @bestchoice383
    @bestchoice383 Год назад +1

    Yani huyu kaka anaimba jamani ...nyimbo zake zinanirudisha sana kwenye uwepo ....God bless you @ ambwene

  • @Frednzunda-sl7qn
    @Frednzunda-sl7qn Год назад +5

    Barikiwa sana mtumishi nyimbo zako zinafariji sana maisha ya mtu

  • @renatusmillambo2014
    @renatusmillambo2014 Год назад

    Huyu ndugu ndiye hunipa MAHUBIRI ya madhabahuni.....dah....siyo kwa jumbe hizi....Wala huu siyo wimbo...Bali Ni wito kwa kila MMOJA wetu........Ambweneeeeeeeeeeewwwww

  • @GabrielManyaji-zl2zh
    @GabrielManyaji-zl2zh Год назад +4

    Kaka ambwene kweli unakarama njema San mungu akubariki sana

  • @SandrahTumain
    @SandrahTumain 2 дня назад

    Nimeachiliaa .nimesamehe..nimesahau..thanks God🙏
    Ma fav song nikiskiliza ni machozii tu yananitokaa

  • @ChobaaB4
    @ChobaaB4 7 месяцев назад +3

    Nimeachilia maumivu yote ndan ya moyo wangu

  • @JosephineSamila-uy4cg
    @JosephineSamila-uy4cg 7 месяцев назад +2

    Nimeweza kusamehe kupitia wimbo huu Mungu akubariki kaka

  • @abelpilato8851
    @abelpilato8851 Год назад +3

    Congratulations mwamba hakika siku zote huwa nasema hujawahi kosea kwenye kazi zako uko full package mtumishi hukurupuki mungu akutunze my brother God is good all the time 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿💛💚💛💪

  • @joshuaayoub840
    @joshuaayoub840 Год назад +9

    Ni nyimbo ambayo kama vile nilikua naisubiri katika uponyaji wangu wa kuachilia niliyoyashika na yalionitesa kwa mdaa. Ubarikiwe sanaa mtumishi wa bwana. #NIMEACHILIA SASA😢

  • @nehemiamwashinani1821
    @nehemiamwashinani1821 Год назад +4

    Thank you 🙏 Dear Lord nilisha achilia yote yamepita nashukuru Mungu ulinivusha salama!! 🙏🙏✅

  • @florianmwaibabile2541
    @florianmwaibabile2541 Год назад

    Ulikinyamana Kyantwa!!!! Huiiii!!!! Usajighwe untwa mallafyalle!!.

  • @SaraMdoe
    @SaraMdoe 5 месяцев назад +6

    Kwa wimbo huu naamini nitavuka maumivu haya maana kwa uwezo wangu siwezi😢

  • @MTABAZIJUMA-u4w
    @MTABAZIJUMA-u4w 4 дня назад

    kwa kwelihuu wimbo umenigusa HASANTE SANA MUNGU ANDELE KUKUTUMAI AWE PAMOJA NAWE MAISHA YAKO YOTE

  • @DannyMuvunga-cz9zs
    @DannyMuvunga-cz9zs 2 месяца назад +3

    Nduguyangu Ambwene Mungu wa Mbinguni aku tumiye kama chombo kyake kya sifa

  • @einothlaizer7563
    @einothlaizer7563 Год назад +1

    Story of my life,,barikiwa sana mtumishi wa Mungu

  • @hurumaelmanyareg
    @hurumaelmanyareg Год назад +22

    A verily healing song. Mungu azidi kukubariki na kukuinua kaka Ambwene Obadia Mwansongwe

  • @emmanuelmhina7176
    @emmanuelmhina7176 Год назад +3

    True story about me. Wakati nikitafakari nikakuta mtu mwingine anasononeka Kwa anayoyapitia, rafiki ake akamwambia usilie, sikiliza NIMEACHILIA. Ndipo nami nikajikuta hapa. Naamini lipo suluhisho mbeleni 🙏

  • @kwilasajunior5367
    @kwilasajunior5367 Год назад +3

    Hiii nyimbo Ina nifikilisha mengi mnoo dah nasijawahi imaliza kusikiliza coz ninameng ya moyon now nachiliaa Niko na amani Asante mungu 🙏🏼

  • @suzanneullimboka-hp2hz
    @suzanneullimboka-hp2hz Год назад +1

    Baba huwa unaimba nyimbo nzuri sana zinanibariki lakini huu wimbo umenibariki zaidi

  • @SPK450
    @SPK450 Год назад +23

    Ambwene is not only talented, but also blessed I really feel blessed too listening to this song

  • @prospermsogoya177
    @prospermsogoya177 Год назад +2

    Im just healed psychologically instantly...Yesu Kristo nitakuweka moyoni mwang ukae wewe tuuu other things baadae

  • @KahindoChristelle-o6v
    @KahindoChristelle-o6v 2 месяца назад +3

    Wimbo inanibariki sana mungu akupe Maicha marefu😢😢😢😢 ukuenaniombea sana

  • @Allyabdalah-oj2wc
    @Allyabdalah-oj2wc 9 месяцев назад +2

    Asante kwa wimbo mzur nilipousikia tu 2024 nikaingia kwa aman mpaka sasa jaman barikiwa Ambwene

  • @nebartsanga7890
    @nebartsanga7890 Год назад +13

    Ubarikiwe mtumishi kwakwel umefanyika baraka sana kwa utunzi wa nyimbo zako zote zina tia moyo sana na kufariji saana
    Najivunia uwepo wako ktk Tanzania yetu
    Mungu akubariki sanaaa

    • @jeninyereu5576
      @jeninyereu5576 Год назад +1

      Barikiwa mtumishi wa Mungu binafsi nimeachilia yoooteee

  • @Ngendaruheze
    @Ngendaruheze 8 месяцев назад +4

    Moja ya mtumishi wangu bola nchi hii namba Moja wewe

  • @muniramsigwa8537
    @muniramsigwa8537 Год назад +5

    Ubarikiwe sana mtumishi hakika nimeachilia wimbo umeniponya sana

  • @georgekambofi-zv8rw
    @georgekambofi-zv8rw Год назад

    Nimeachilia Kwa kweli haikuwa yangu nashukuru sana Kwa ujumbe mzuri mtumishi Wa MUNGU

  • @nossimlukumay5327
    @nossimlukumay5327 Год назад +3

    Kuna mambo hatuwezi kuelezea kwenye maisha yanatuumiza kiasi cha kuwaza kujiua huu wimbo umenifunza mengi kwa sasa NIMEACHILIA

  • @namdigumagwenge193
    @namdigumagwenge193 Год назад

    Amen 😢😢😢eeee yesu nionekanie Mimi ninyoshee mkono wa ukombozi juu ya maisha yangu ponya moyo wangu, maisha yangu na vizazi vyangu vyote