KIMEUMANA! MKANDARASI ABANANISHWA, ATAKIWA KUJISALIMISHA KWA DC LUSHOTO..

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 25 окт 2022
  • KIMEUMANA! MKANDARASI ABANANISHWA, ATAKIWA KUJISALIMISHA KWA DC LUSHOTO..
    Wakurugenzi wa Kampuni ya M/S PNR SERVICES ya Jijini Dar es Salaam
    waliopewa zabuni ya shilingi Bilioni 1.8 ya kuvuta maji km 14 kutoka
    Hifadhi ya Msitu wa Magamba hadi katika Mji wa Lushoto kujisamilisha
    wenyewe ofisini kwake kwa nini hadi Sasa wameifanya kazi hiyo kwa
    asilimia 20 tu wakati mradi huo wanapaswa kuukabidhi kwa Mamlaka ya
    maji Lushoto(RUWASA) januari 30 mwaka kesho.
    Lazaro alisema hayo katika chanzo Cha maji Cha Msitu huo alipotembelea
    Mradi huo na kusikitishwa kuona Mkandarasi amelipwa zaidi ya shilingi
    milioni 200 kwa ajili ya kazi hiyo lakini amekuta wafanyakazi saba tu
    katika ujenzi wa chanzo Cha maji Hali iliyomsikitisha na kupata
    taarifa kuwa Wakurugenzi wa Kampuni hawajawahi fika Lushoto pamoja na
    kutakiwa na uongozi wa RUWASA zaidi ya Mara tatu.
    Alisema na kumwagiza msimamizi wa mradi wa Kampuni hiyo, Singo Omari
    aliyemkuta eneo la Mradi kuwataarifa Wakurugenzi wake kuwa anawahitaji
    haraka ofisni kwake Alhamis octoba 27 mwaka huu saa 1.30 asubuhi kuja
    kujieleza Ni kwa Nini wasichukuliwe hatua kwa kupuuza wito wa Meneja
    wa RUWASA Wilaya ya Lushoto na kwa nini kazi haifanyiki wakati
    wameshachukua mamilioni ya pesa za Serikali kwa ajili ya Mradi huo
    Mkuu wa Wilaya alisema tanki ya maji lenye uwezo wa kubeba Lita
    600,000 bado halijajengwa,usambazaji wa bomba za maji za umbali wa km
    14 kutoka Msitu wa Magamba hadi Mjini Lushoto bado mtaro haujachimbwa
    Wala mabomba hayajafika eneo la Mradi na alisema dharau za Wakurugenzi
    wa Kampuni ya M/S PNR SERVICES waliifanya haitavumiliwa kamwe lazima
    waeleze ni kwa nini muda wote hawajafanya kazi na pesa ya Serikali
    wameshapewa.
    ⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: ndstream.net/globalradio/
    ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
    ⚫️ ANDROID:bit.ly/38Lluc8
    ⚫️ iOS:apple.co/38HjiCx
    ⚫️ VISIT COMEDY PLAYLIST: • GLOBAL COMEDY/MOVIES
    ⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
    ⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 657 693 210), ( +255 784 888982)
    ⚫️ Email: globaltvonlinenews@gmail.com OR abbymrisho@gmail.com
    ⚫️ OUR PLAYLISTS:
    ⚫️ MICHEZO na BURUDANI: • Habari zote za michezo...
    ⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: bit.ly/mikasa_ya_kusisimua
    ⚫️ GLOBAL RADIO TV: bit.ly/255globalradio
    ⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: bit.ly/exclusive_interviews
    ⚫️ Subscribe Global TV bit.ly/globaltvonline

Комментарии • 8

  • @collinscosmas9484
    @collinscosmas9484 Год назад +1

    Mfumo mfumo mfumo haya mambo kila siku yapo na hakuna hataua yeyote

  • @hezekiamtera3559
    @hezekiamtera3559 Год назад +1

    Mbunge naye hajui?Kuna shida kubwa hapo

  • @abuuramadhan8093
    @abuuramadhan8093 Год назад

    Funga ndan akalale kwanza

  • @abuuramadhan8093
    @abuuramadhan8093 Год назад

    Akalale ndan kwanza

  • @mohamedjeizan5929
    @mohamedjeizan5929 Год назад

    Ashikwe aliyempa kazi sio huyo Mzee.
    Mbona madudu yameanza kuibuka tena

  • @mohamedrashid9035
    @mohamedrashid9035 Год назад

    Jamani Serikali ijitasmini kuwapata wakandarasi huyo mzee ni feki na kapewa kazi vipi hao hawawezi kufanya chochote hapo wapeni jeshi hapo