SHEIKH YUSUF ABDI - KISA CHA MLEVI ALIYEINGIA PEPONI / MWISHO MWEMA

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 5 сен 2024
  • Sheikh Yusuf Abdi leo ametuletea mawaidha yakiwa na mada ya juu ya mwisho mwema
    Ee binaadamu! Mche Mwenyezi Mungu na jiandae kukutana na Mola wako kwa maandalizi ya waja wema. Hakika hali ya (kila) mwanadamu ni kama Anavyosema Mwenyezi Mungu
    Ewe Muislamu, hakika binaadamu hajui wapi atafariki wala hajui lini atafariki kama Anavyosema Mwenyezi Mungu
    Ikiwa hatujui tutakachokichuma kesho, jambo ambalo ni katika matendo yetu, basi hakika hatujui pia lini tutakufa kwani hilo ni katika matendo ya Mwenyezi Mungu. Na ikiwa hatujui nchi (au mahali) gani tutakufa juu ya kwamba mtu anakwenda nchi (au mahali) anayoichagua mwenyewe, basi hakika yeye hajui lini atakufa. Kwa hivyo basi, mahali pa kufariki na wakati wa kufariki haujulikani! Tunamuomba Mwenyezi Mungu Aturuzuku husnul-khaatimah (mwisho mwema)
    #SHEIKHYUSUFABDIKISACHAMLEVIALIYEINGIAPEPONIMWISHOMWEMA #yusufabdimwishomwema #yusufabdmawaidha
    Na si muhimu mtu kujua kufariki lini wala kufariki wapi. Hakika hakuna la muhimu isipokuwa jambo la muhimu ni katika hali gani mtu atafariki? Hili ndilo la muhimu; atafariki katika hali gani? Je, utafariki ukiwa katika Imani na ikhlaasw na Tawhiyd? Tunamuomba Mwenyezi Mungu Atujaalie hayo yote (kufariki katika hali hizo za Imani, ikhlaasw na Tawhiyd). Au je utafariki katika shaka na shirki na kufuru na ukanushaji? Hili ndilo muhimu, hili ndio! Lakini anayetaka kufariki kifo kizuri, basi afanye kheri kwani Mwenyezi Mungu ni Mkarimu mno na Mpaji mno Hatomwacha mja Wake katika dhiki ikiwa mja atakuwa ni mwenye kumkumbuka (na kumdhukuru) Mwenyezi Mungu wakati anapokuwa katika hali ya raha. Mtume ﷺ amesema:

Комментарии • 21