SERIKALI YAJA NA MUAROBAINI WA ENEO LA MTANANA, BARABARA KUU MOROGORO - DODOMA KUJAA MAJI

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 18 янв 2024
  • Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Mhandisi Aisha Amour kuwasimamia wataalamu kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS) kuhakikisha hadi kufikia mwezi Desemba mwaka huu uboreshaji wa miundombinu ya barabara katika eneo Mtanana katika barabara kuu ya Morogoro - Dodoma uwe umekamilika na kupitika vipindi vyote vya mwaka.
    Aidha, Bashungwa amesema kuwa tatizo la kukatika mawasiliano ya barabara kutokana na mvua za Elnino zinazoendelea kunyesha katika eneo la Mtanana jijini Dodoma litakuwa historia mara baada ya Serikali kupata suluhu katika eneo hilo.
    Ameyasema hayo leo Tarehe 19 Januari 2024, jijini Dodoma mara baada ya kukagua eneo hilo ambapo mnamo tarehe 9 Januari, 2024 alimuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mohamed Besta kufanya tathmini ya eneo hilo ambalo lilijaa maji na kusababisha barabara hiyo kufungwa majira ya asubuhi.

Комментарии • 3

  • @abuuramadhan8093
    @abuuramadhan8093 5 месяцев назад

    Huyu waziri ni mzigo san kwann mama anamlea

  • @rasheedabby2871
    @rasheedabby2871 6 месяцев назад

    Mvua inaleta athari za kimundombinu,nyumba na maisha ya watu kwa ujumla ila haijazi mabawa tupate umeme wakutosha hapo ndo shida inakua ngumu

  • @abuuramadhan8093
    @abuuramadhan8093 5 месяцев назад

    Hakuna wizara hata moja ambayo alishawah kufanya vizuri na wizara aliopewa saiv ndo kawa mzigo kwa Taifa