BASHUNGWA ATOA TAMKO MPASUKO WA BARABARA BUSUNZU - KIGOMA, SIO UPIGAJI.

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 5 сен 2024
  • Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kuwa uchunguzi umebaini mpasuko wa ardhi na kuporomoka kwa tuta la barabara uliojitokeza katika eneo la Busunzu lenye urefu wa mita 200 haijatokana na makosa ya Mkandarasi kwenye ujenzi bali umesababishwa na sababu za kigeolojia.
    Amebainisha kuwa kipande cha barabara hiyo kipo katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Manyovu - Kasulu - Kibondo - Kabingo Awamu ya tatu ya barabara ya Mvugwe hadi Makutano ya Nduta (km 59.35) ambayo ilikwishakamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
    Bashungwa ametoa taarifa hiyo Mkoani Kigoma leo Julai 10, 2024 mara baada ya kukagua eneo hilo na kupokea taarifa ya uchunguzi iliyofanywa na Wataalamu wa miamba kutoka Taasisi ya Geolojia na utafiti wa madini Tanzania (GST), Kitengo maalum cha Utafiti cha TANROADS, na School of Mines and Geosciences (SoMG) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Комментарии • 7