LIFAHAMU KUNDI LA M23, SABABU ZA KUIVAMIA DRC

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 4 фев 2025
  • Kundi la waasi wa M23 wanaotajwa kufadhiliwa na Serikali ya Rwanda wanadaiwa kuuteka Mji wa Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) baada ya mapigano yaliyodumu kwa wiki kadhaa dhidi ya vikosi vya jeshi la nchi hiyo (FARDC).
    Kwa mujibu wa tovuti ya The Guardian, eneo lililotawaliwa na mapigano hayo lenye majimbo ya Ituri, Kivu Kusini na Kivu Kaskazini yanaundwa na makundi ya zaidi ya 129, kundi kuu katika maeneo hayo ni kundi la waasi wa M23.
    Lifahamu kundi la M23
    Kwa mujibu wa Tovuti ya The Guardian, ni vigumu kuzungumzia waasi wa M23 bila kutazama historia ya jamii ya Watutsi eneo la Mashariki mwa DRC, jamii hiyo pia inapatikana nchini Rwanda.
    Mwaka 2006 liliundwa kundi la National Congress for the Defence of the People (CNDP) lililoundwa na viongozi wa Watutsi waliopo Mashariki mwa DRC.
    Kundi hilo liliibuka kutokana na kuibuka mvutano wa kikabila kati ya Watutsi na makabila mengine, hasusan baada ya mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994 na mgogoro wa wakimbizi nchini DRC.
    Kundi la waasi la RCD, ambalo lilikuwa limedhibiti eneo la Mashariki mwa DRC, lilikata tamaa kupata mwafaka wa kuingia kwenye maridhiano ya amani na Rais Joseph Kabila, wakihofia kupoteza ushawishi wao eneo hilo.
    Wakiongozwa na Laurent Nkunda, CNDP ililenga kuwalinda raia wa Kitutsi dhidi ya mashambulizi ya makundi ya wanamgambo wa Kihutu na kupata uwakilishi bora wa kisiasa kwa Watutsi katika Serikali ya DRC chini ya Rais Kabila.
    Kuundwa kwa CNDP kwa kiasi kikubwa kulitokana na kushindwa kwa mchakato wa amani na kutozingatiwa kwa mahitaji na usalama wa jamii ya Watutsi.
    Vita vya Kwanza na vya pili vya DRC kati ya mwaka 1996 hadi 2003 ziliingilia kati kisha mtandao tata wa ushirikiano wa kukabiliana na makundi hayo.
    Mtandao ulilenga kukabiliana na makundi ikiwemo Congress of the National Congress for the Defence of the People (CNDP) na M23 ambayo ni mrithi wa CNDP.
    Makundi hayo yanatuhumiwa kunufaika na mizozo ya ndani ya Serikali na biashara haramu ya madini kutoka migodi iliyopo mashariki mwa DRC.
    M23 ilianzia wapi?
    CNDP, kikiongozwa na Laurent Nkunda, awali kiliundwa ili kulinda jamii za Watutsi lakini lilijulikana kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na biashara haramu.
    Mnamo 2009, makubaliano ya amani yalitaka kuunganisha vikosi vya CNDP katika jeshi la DRC, lakini mvutano uliendelea na kusababisha kuundwa kwa M23 mnamo 2012.
    Kundi hilo lilipewa jina baada ya makubaliano ya amani ya Machi 23, 2009 ambayo yaliahidi kuunganishwa kwa wapiganaji wa CNDP katika jeshi la DRC na kutambua mrengo wao wa kisiasa.
    Hata hivyo, kikundi cha CNDP kilidai kuwa makubaliano hayo hayakutekelezwa vyema na kuzaliwa kwa M23 ili kushinikiza madai yao.
    M23 inadai kulinda jamii za Watutsi na wanaozungumza Kinyarwanda nchini DRC, ikitaja vitisho kutoka kwa wanamgambo wa Kihutu na kushindwa kwa serikali kulinda usalama wao.
    Licha ya madai hayo, kundi hilo limekuwa likishutumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwemo mashambulizi dhidi ya raia.
    Ripoti ya Umoja wa Mataifa inakadiria kuwa kufikia Januari 2025, kundi la M23 lilikuwa na wapiganaji kati ya 3,000 na 4,000.
    Hata hiyo UN imekuwa ikiishutumu Rwanda kwa kufadhili kundi hilo tuhuma ambazo Rwanda imekuwa ikikanusha kila mara.
    Balozi wa Rwanda katika Umoja wa Mataifa, Ernest Rwamucyo, jana alipokuwa akihutubia mkutano wa Baraza la Usalama la Afrika hakukanusha wala kuthibitisha madai hayo ya kuwa na mkono wao katika uvamizi huo wa M23.
    Aidha Rwanda imeendeleza madai kwamba kundi la wapiganaji la FDRL ambalo lilitajwa kuhusika katika vita vya kimbari vya 1994, lilikimbilia DRC na linatumiwa na taifa hilo kuendeleza muaji ya kimbari eneo la Mashariki mwa DRC, jambo ambalo Serikali ya DRC imekuwa ikikanusha.
    Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe aliieleza Associated Press (AP) kuwa uamuzi wa DRC kukatisha mahusiano yake na Rwanda ni kukiuka makubaliano ya kimataifa.
    “Kwa upande wetu tumechukua hatua stahiki kuwaondoa wanadiplomasia wetu nchini DRC ambao walikuwa hatarini kudhuriwa na vikosi vya usalama vya Congo,” amesema Nduhungirehe.
    Ripoti ya Umoja wa Mataifa mwaka 2022 iliangazia ushahidi wa Vikosi vya Ulinzi vya Rwanda kusaidia M23 na kuzidi kuzorotesha uhusiano kati ya Rwanda na DRC huku mzozo wa rasilimali ikiwemo madini ukitajwa kuwa sababu kuu ya vita hiyo.
    M23 wanavyojitanua
    M23 inaendelea kujitanua ndani ya DRC ambalo ni Taifa la nne kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika, wanaokadiriwa kufika milioni 109 mwaka 2024.
    Mashambulizi ya M23 yaliyoanza wiki moja iliyopita nchini DRC yamebadilisha upepo wa hali ya usalama Mashariki mwa DRC.

Комментарии • 21

  • @emzodereal3106
    @emzodereal3106 7 дней назад +3

    Nafatilia kwa karibu sana

  • @magrethmbuma3045
    @magrethmbuma3045 8 дней назад +2

    Jamanii

  • @godlovekivuyo
    @godlovekivuyo 6 дней назад

    Inauma sana jaman watu wanakufa kama mbu

  • @BalimugegeKibungulu
    @BalimugegeKibungulu 7 дней назад +1

    Wanyarwanda wapeni amani wenzenu,tokeni namauwajiyenu,mulisha ibiya wakoncomani vyakutosha,hamna kugawa inchiii tumekattaaa,Mungu njo katupa utajiri wetu,rizikeni navyenu

  • @PaulBuza-b9m
    @PaulBuza-b9m 8 дней назад +3

    Kuweni na mshikamano wote wanakongo ilahata ss tunaumia selikari kaeni chini myamalize hayo mambo

  • @Godchila03
    @Godchila03 6 дней назад

    Daaa aseeee hawa wakongo hiyo ardhi inashida gqnii

  • @aliramadhan-bo1wr
    @aliramadhan-bo1wr 7 дней назад +2

    Hii hali inatia huruma. Hawa watoto wadogo wanamakosa gani jamani. Mtoto mdogo kabebeshwa mizigo. Jamani nyiii.

  • @SHINELOVETV
    @SHINELOVETV 7 дней назад +2

    Kwani hao m23 Wana ukubwa gani mpaka kuzidi jeshi la congo ..Yani miaka na miaka wanatamba wao tu ...kweli jeshi la congo linashindwa kuwasambaratisha ao m23

    • @X-ray47j
      @X-ray47j 7 дней назад

      Congo haina Jeshi la Nguvu hata silaha zenye nguvu hawana yani taifa la Congo ni bure tu

    • @BenjaminNickson
      @BenjaminNickson 7 дней назад +1

      Hao watusi asili yao ni Israel kuwashinda kivita ni ngumu sana

    • @silvesterrichardhelenya1319
      @silvesterrichardhelenya1319 6 дней назад

      Jeshi lenyewe linaondoa raia wake kuwa siyo wakongo

  • @JabiliMussa
    @JabiliMussa 5 дней назад

    Muyamaluze

  • @PolRicric
    @PolRicric 5 дней назад

    Naomba kuuliza kwn awa M23 wanaua hadi raia wa kawaida

  • @AthumaniBonneface
    @AthumaniBonneface 8 дней назад +1

    Kwanini serekali ya inchi ya kongo nizaifu sana? Rwanda ninchi ndogo sana inakweje wanaisumbuwa sana kongo? Kwasababu naisi waho ndo kipau mbele cha kuwapa sapoti M23

  • @AhmadZahor-b4e
    @AhmadZahor-b4e 2 дня назад

    Mnapata mpka kuwapiga picture si muwauwe kabisa wakati wa kuwapiga picture

  • @BalimugegeKibungulu
    @BalimugegeKibungulu 7 дней назад

    Angalieni kamtu kanako sumbuwa wenzie,sikabaki muinnci yake?

  • @gaspangowi9081
    @gaspangowi9081 6 дней назад

    Copy n paste from BBC!

  • @BalimugegeKibungulu
    @BalimugegeKibungulu 7 дней назад

    Angalieni kamtu kanako sumbuwa wenzie,sikabaki muinnci yake?

  • @BalimugegeKibungulu
    @BalimugegeKibungulu 7 дней назад

    Angalieni kamtu kanako sumbuwa wenzie,sikabaki muinnci yake?