Это видео недоступно.
Сожалеем об этом.

Miujiza ya Yesu Kristo Kuwalisha Watu 5000 {Mathayo

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 15 июн 2024
  • Miujiza ya Yesu Kristo Kuwalisha Watu 5000-Mathayo 14:13-21; Yohana 6:1-13;
    Yesu alikuwa amechoka na alitaka kutumia muda na wanafunzi wake. "Hakuna hadithi nyingine kwa sasa," Yesu akasema.
    Walipanda mashua wakavuka ziwa la Galilee.
    Walipofika ng'ambo ya pili, umati mkubwa wa watu ulimmfuata kwa sababu waliona miugiza aliyokuwa amefanya kwa kuwaponya wagonjwa.
    Ndipo Yesu akapanda mlimani na kukaa chini na wanafunzi wake. Watu walimfuata Yesu mlimani.
    Walitaka kuwa karibu na Yesu na kusikiliza mafundisho yake.
    "Haraka, mtoto mdogo, leta chakula chako cha mchana. Samaki wako wawili na mikate yako mitano. Sasa nenda kumtafuta Yesu." Kijana mdogo aliambiwa na mamake
    Pale mlimani mtoto alikiweka chakula chake vizuri na kuskiliza Yesu.
    Yesu aliwapenda watu na aliwaponya wengi waliokuwa wagonjwa.
    Siku nzima Yesu aliwafundisha watu na kusimulia hadithi. Jioni ilipokuwa inakaribia, kila mtu alikuwa anahisi njaa. Kuanzia watoto wadogo, wanaume na wanawake.
    "Waruhusu watu waende," marafiki wa Yesu wanasema.
    "Hapana, watu wamechoka," Yesu akasema.
    "Tutanunua wapi mkate wa kuwapa watu hawa?" Yesu akamuuliza Filipo, mmoja wa wanafunzi wake.
    Filipo akamjibu, "Hatuwezi kununua chakula kwa kila mtu kwa sababu hatuna pesa za kutosha."
    "Hapa!" akasema mtoto mdogo. "Mpeleke Yesu chakula changu."
    Wakachukua samaki wawili na mikate mitano kwa Yesu.
    Akitazama juu mbinguni, Alisali na kumshukuru Mungu. Yesu akavunja mikate na kwa muujiza wa Mungu, mikate na samaki vilikuwa vya kutosha kwa kila mtu.
    Yesu aliwapa wanafunzi, nao wakawagawia watu.
    Wakala wote na kushiba, na wanafunzi wakachukua vikapu kumi na viwili vya vipande vilivyobaki.
    Hadithi hii inapaswa kutukumbusha kwamba Yesu anaweza kutimiza mahitaji yetu yote na anajua tunayopitia, hata tunapokuwa na njaa.

Комментарии • 1