"MARUFUKU HOSPITALI KUZUIA MAITI"- RC MAKONDA

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 26 май 2024
  • "MARUFUKU HOSPITALI KUZUIA MAITI"- RC MAKONDA.
    Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amepiga marufuku hospitali za Mkoa wa Arusha kuzuia maiti kutokana na gharama za matibabu na badala yake zibuni njia mbadala za kudai malipo hayo.
    Mkuu wa Mkoa Mhe. Makonda ametoa katazo hilo leo Mei 27, 2024 alipofanya ziara katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli kukagua maendeleo ya Ujenzi wa jengo la mionzi na la upasuaji pamoja na kuzungumza na wahudumu wa hospitali hiyo na kuangalia namna huduma zinavyotolewa hospitalini hapo.
    Mhe. Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa na Waganga wakuu wa wilaya zote za Mkoa wa Arusha kusimamia agizo hilo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alilolitoa kupitia kwa Waziri wa afya.
    Katika hatua nyingine Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Arusha akiwa Hospitalini hapo amewataka wahudumu wa afya mkoani Arusha kutoa huduma nzuri kwa wananchi wanaofika hospitalini na kwenye vituo vyote vya afya ili kuwa sehemu ya kuwapunguzia maumivu wananchi kutokana na magonjwa yanayowasumbua.
    Mhe. Makonda amesema Mkoa wa Arusha unafaa kuwa Mfano wa huduma nzuri za afya ili kuendana na uwekezaji mkubwa wa serikali ya awamu ya sita kutokana na Rais Samia Suluhu Hassan kutoa fedha nyingi za kuwezesha miundombinu bora ya utoaji wa huduma za kiafya.
    Mhe. Paul Makonda anaendelea na ziara yake ya Kikazi Wilayani Monduli ambapo pamoja na mambo mengine amepangiwa pia kukagua mradi wa maji wa Kijiji cha NAFCO kabla ya kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara unaotarajiwa kufanyika eneo la Meserani maarufu kama Duka bovu.

Комментарии • 44

  • @neemanziku5403
    @neemanziku5403 21 день назад +8

    Makonda wetu hoyeeee🙏💪

  • @user-xk7vy4gb6g
    @user-xk7vy4gb6g 21 день назад +2

    Safi sana Mh Makonda Mungu akubariki sana. Hakika tunajivunia uwepo wako na Rais Samia kukuteua 🎉🎉🎉🎉

  • @dorahmushi-we6ts
    @dorahmushi-we6ts 21 день назад +1

    T M U
    Mungu azidi kuwatangulia, asante mama Samia mama, Mungu azidi kuwalinda wote, uongozi wako na washauri wako...

  • @kiningashukran5177
    @kiningashukran5177 21 день назад +4

    Makondaa unapambana sana hata kama unachengamoto nyingi sanaaa

  • @emmanuelbernard9552
    @emmanuelbernard9552 21 день назад +5

    Mkuu wa Mkoa wa wakuu wa mikoa yote Tanzania Makonda akiongea

  • @charlesmakelele4268
    @charlesmakelele4268 19 дней назад

    MWENYEZI MUNGU azidi kukupigania makonda.

  • @OmanOman-dn6dj
    @OmanOman-dn6dj 21 день назад +4

    Kwakweli sio vzr kukataza maiti itoke hosptal kisa pesa

  • @mercyzakariah
    @mercyzakariah 20 дней назад +1

    Niukweli, usio pimika kabula makonda hajateuliwa kua mwenezi CCM Nani kiongozi Alie jitwika jukumu la kuwasikiliza WA tz kama sio makonda, halihii tukua tunaiona kwa magufuli pekee

  • @Nedjadist
    @Nedjadist 21 день назад

    Safi sana. Nakushauri uandike mwongozo upelekwe hospitali zote. Vinginevyo ukiondoka tu, yamekufa. Au ichagize Wizara ya Afya iandike mwongozo huo kwa hospitali zote za serikali na binafsi, na adhabu ya asiyefuata.
    Kuna namna nyingi za kistaarabu kuwadai wafiliwa. Kwa mfano, kuwauliza wana uwezo wa kulipa kiasi gani kila mwezi (kama wafanyavyo huku Ulaya watu waliostaarabika). Pia anzisheni bima za mazishi au katika bima ya afya include hiyo (lakini msiwawekee watu kulipa laki mbili kwa mwezi. Elfu tatu kwa mwezi tosha). Of course, itatazamwa mtu anaikata wakati gani, siyo yuko mahtuti .....
    Mambo mengi Tanzania yanasababisha usumbufu kwa wananchi kwa vile watendaji wengi hawana/ hawatumii akili tu.

    • @jacobmakono4399
      @jacobmakono4399 20 дней назад

      Nakubaliana nawe!mtu Kesha kufa ..daini hizo 3000 kila mwezi hata miaka 3..potelea mbali lkn siyo kuzuia maiti?

  • @angellomarcel5677
    @angellomarcel5677 21 день назад +3

    Makonda atakuja kifitiniwa maana kashawafunika wengine sasa tusubiri tuone

  • @SalumuMashauri
    @SalumuMashauri 19 дней назад

    Arusha mshukuruni mungu kuwaletea mwamba huyu

  • @ghhhhy1812
    @ghhhhy1812 21 день назад +1

    Ilo kwel

  • @LaizaLaiza-oj9uw
    @LaizaLaiza-oj9uw 19 дней назад

    Makonda wape somo hajuwi kitu viongozi wa arusha

  • @user-ff1pj3wx9t
    @user-ff1pj3wx9t 21 день назад

    Kwakweli Makonda anajitahidi, hakuna mkuu wa mkowa anaefatilia matatizo ya wananchi wamkoa wake km huyu mtumishi wa Mungu,,

  • @dorahmushi-we6ts
    @dorahmushi-we6ts 21 день назад

    😭😭😭😭😭🙏🙏🙏🙏🙏

  • @Optionxll_Playz1
    @Optionxll_Playz1 21 день назад +1

    Mbona ilikuwa Ni shida sana Ni Kwa nini wanganganie maiti ?

  • @halimadamasi2770
    @halimadamasi2770 21 день назад +1

    Twayeeeeeb ❤

  • @mussakimaro5588
    @mussakimaro5588 21 день назад +2

    raisi ajae mbeleni

  • @RamadhanAthuman-jg3us
    @RamadhanAthuman-jg3us 21 день назад +1

    Rais ajaye baada ya mama

  • @msafiriomary893
    @msafiriomary893 20 дней назад +1

    Hyo turizika chato hakuna daktari au muuguzi mwenye tabia nzuri saiz ukienda hospital za serikal awamu hii nisawa na kusaini hati ya kifo

  • @userKAZIEYENDELEE
    @userKAZIEYENDELEE 21 день назад

    pongezi kubwa kwako binafsi

  • @theempire4058
    @theempire4058 21 день назад

    Makonda rais jerry silaa waziri mkuu = Magufuli ( hapa kazi tu)

  • @dorahmushi-we6ts
    @dorahmushi-we6ts 21 день назад

    T M U chini ya uongozi wa mama Samia na Serikali yake, sisi wanyonge tuko nyuma yenu kwa maombi kila mmoja kwa imani yake,
    Mtu ambae hajapitia hayo Makonda na timu yake wanayafanyia kazi katu hawatamuelewa!!
    Lkn upo usemi usemao mwenzio akinyolewa .......

  • @user-cx9lt8hh4l
    @user-cx9lt8hh4l 21 день назад

    🫡🇹🇿

  • @faustinluambano2958
    @faustinluambano2958 21 день назад

    Kiongozi wa hovyo

    • @charlesjohnjohn7953
      @charlesjohnjohn7953 21 день назад

      Kwakusema maiti zisitozwe hela kwa wananchi wasio na uwezo au?

    • @abdulwadi8667
      @abdulwadi8667 21 день назад +1

      Ww ndio wahovyo huna akili hata kidogo

  • @maharagendondo
    @maharagendondo 21 день назад

    MAKONDA, HONGERA TWASHANGA HOSPITALI ZOTE NCHINI TZ ZINAZUIYA MAITI WAKATI DADA UUMI ALIKATANZA KUZUUIWA MAITI LAKINI BADO WANAZUIYA TATIZO NN

  • @hamadsheni8997
    @hamadsheni8997 21 день назад

    AMRI BILA KUPELEKA BARUA INAYO ELEKEZA HLO.HYO TUNAITA SIASA.

    • @FahadAbubakari
      @FahadAbubakari 21 день назад

      Kwa hiyo uambiwe itapopelekwa barua amri zoote zitolewazo hutoka na barua

    • @nicodemashaggite8429
      @nicodemashaggite8429 21 день назад +1

      Huelewi wewe.
      HIVI unadhani Makonda anafanya siasa!!

    • @user-ih1pk1vs4q
      @user-ih1pk1vs4q 21 день назад

      Ww jinga

    • @user-ih1pk1vs4q
      @user-ih1pk1vs4q 21 день назад

      Makonda piga spana watu waby sn

    • @MiriamAbdallah
      @MiriamAbdallah 21 день назад

      Mmesikia alichosema waziri au hamjamsikia na Kila AMRI unakuwa na barua hakuna AMRI bila barua, tukiangalia kwa majini ni siasa vipi AMRI aliyoitoa kumhusu yule mdada Sabrina ilitekelezwa au alienda kulimwa talaka