BASHUNGWA AMKABIDHI DKT. MSONDE TAASISI YA TEMESA NA TBA, ATAKA MAGEUZI NDANI YA MIEZI MITATU

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 5 окт 2024
  • Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemuelekeza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Charles Msonde kuhakikisha anazisimamia Taasisi za Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kufanya mabadiliko na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazokabili Taasisi hizo ili kuboresha utendaji na ufanisi wa Taasisi hizo.
    “Namjua Dkt. Msonde nimefanya nae kazi nikiwa TAMISEMI, ni mzee wa kunyooka na mwenye kufuata utaratibu, kwa hiyo naomba mnipe miezi mitatu nimkabidhi Taasisi hizi Naibu Katibu Mkuu ili kufanya mabadiliko katika taasisi hizi”, amesema Bashungwa.
    Ametoa maelekezo hayo Agosti 20, 2024 jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya ukarabati na ujenzi wa vivuko vipya kutoka kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu jijini Dodoma na kuahidi Kamati hiyo kumpa miezi mitatu ili kufanya mabadiliko kwa Taasisi hizo.

Комментарии •