Sheikh Bachu - Mauti A
HTML-код
- Опубликовано: 7 фев 2025
- Popote mtakapokuwa yatawafika mauti na hata mkiwa katika ngome madhubuti.
Umetangulia mfano wake wakati wa kufasiri 3: 145 kifungu 'Ajali imeandikwa.'
Likiwafikia zuri wao husema: Hili linatokana na Mwenyezi Mungu na likiwafika baya, husema hili linatokana na wewe.
Kila alionalo mtu ni zuri, husema ni zuri na kulifuatishia na neno ‘heri’ ambalo mtu hulipendelea na kulitamani. Na kila alionalo mtu ni baya, husema ni baya, na kuliufuatishia na neno ‘shari’ ambalo mtu hujiepusha nalo na kulikataa.
#SheikhBachuMauti #bachumauti #mawaidhayaumauti #mawaidhayakifo #mauti
#sheikhnassorobachu
Kheri inaweza kuwa ya watu wote; kama vile rutuba na fanaka ambayo haimhusu mtu au kundi pekee. Na mara nyingine huwa inamhusu mtu; kama ufanisi wa mtu baina yake na familia yake. Vilevile shari inaweza kuwa ni ya kiujumla; kama vile ukame na ughali wa vitu; au kuwa ni ya mtu binafsi; kama vile kuwa mke mwovu na watoto wake.
Makusudio ya uzuri katika Aya hii ni heri ya kimaumbile ambayo inaenea kwa wote; kama vile mvua na mfano wake. Na ubaya ni shari inayoenea kwa wote; kama vile kahati na mengineyo. Kwa sababu washirikina walipokuwa wakipata neema; kama vile mvua, husema; Mwenyezi Mungu ametukirimu. Na wakipatwa na adhabu; kama vile kahati, husema: Hii imesababishwa na Muhammad; sawa na vile walivyokuwa wakisema wana wa Israil, ambao Mwenyezi Mungu amewaelezea kwa kusema: "Unapowafikia uzuri husema: Huu ni kwa ajili yetu. Na ukiwafikia ubaya humnasibishia ukorofi Musa …" (7:131)