MBUNGE ATISHIA KULALA BUNGENI

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 23 июн 2024
  • DODOMA: MBUNGE wa Ngara, Ndaisaba Ruhoro ametishia kulala juu ya meza ndani ya ukumbi wa bunge endapo Serikali haitotatua changamoto ya miundombinu ya barabara jimboni kwake.
    Ndaisaba ametoa tishio hilo wakati akichangia hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali 2024/2025 bungeni mjini Dodoma leo.
    Amesema wananchi wake wanahitaji kujengewa barabara waliyoahidiwa kwa zaidi ya miaka 15 iliyopita jambo ambalo limekuwa ni kero ya muda mrefu sasa licha ya kulisemea mara kwa mara bungeni.
    Mbunge huyo amesema kuwa kuchelewa kujengwa kwa barabara hiyo kumechelewesha utekelezaji wa miradi ya kimkakati ambayo ingekuwa na tija kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na kuzalisha fedha ambazo zingenufaisha wananchi wa maeneo mengine.
    Ruhoro ameeleza hayo wakati akichangia bajeti ya Serikali na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2024/25 bungeni jijini Dodoma.
    Imeandaliwa na Benedict Msungu
    Follow us on:
    FACEBOOK;
    SpotiLeo: / spotileo-176. .
    HabariLeo: / habarileo
    DailyNews: / dailynewstz
    INSTAGRAM;
    HabariLeo: habarileo_tz?ig...
    SpotiLeo: spotileo?igshid...
    TWITTER;
    Twitter HabariLeo: HabariLeo?s=09
  • СпортСпорт

Комментарии •