"SIJARIDHISHWA", BASHUNGWA AWA MBOGO UJENZI UWANJA WA NDEGE MSALATO

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 28 сен 2023
  • Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, ameagiza kampuni ya ujenzi ya Beijing kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa jengo la abiria na jengo la kuogozea ndege katika Kiwanja cha Kimataifa cha Msalato, Dodoma ifikapo Desemba, 2024 kulingana na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
    -
    Bashungwa amesema hayo leo Septemba 29, 2023 jijini Dodoma wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho na kutokuridhishwa na kasi ya maendeleo yake kutokana na kusuasua kwa mkandarasi huyo.
    -
    "Mkandarasi usivimbe kichwa kana kwamba umepata kazi nyingi, usipozingatia maelekezo ambayo nimekupatia, kulingana na vipengele vilivyopo kwenye mkataba, tunaweza kukusimamisha kazi kwa mujibu wa sheria " amesema Bashungwa.
    Amemtahadharisha Mkandarasi huyo iwapo atazembea kukamilisha kazi hiyo kwa wakati itampelekea kutopata kazi nyingine katika Sekta ya Ujenzi ndani ya nchi.
    -
    Ameelekeza msimamizi wa miradi kutoka Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kahakikisha anasimamia mradi huo masaa 24 ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa ubora na kwa wakati kama ilivyopangwa.
    -
    Akitoa taarifa ya mradi huo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta amesema kuwa watahakikisha wanawasimamia wakandarasi wote wawili wanaojenga Kiwanja hicho ili kumalizika ndani ya muda kwa kuweka sawa ratiba yao ili iendane na muda waliopangiwa na kupata matokeo yanayoyatarajia.
    -
    Ukamilikaji wa kiwanja hicho ambacho sehemu ya kwanza ya ujenzi wake inagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 165 ni moja ya mkakati wa Serikali katika kuboresha na kuimarisha usafiri wa anga, ambapo kiwanja hicho kitakuwa na uwezo wa kupokea abiria Milioni 1.5 kwa mwaka na abiria 800 kwa wakati mmoja.
    Follow us on:
    FACEBOOK;
    SpotiLeo: / spotileo-176. .
    HabariLeo: / habarileo
    DailyNews: / dailynewstz
    INSTAGRAM;
    HabariLeo: habarileo_tz?ig...
    SpotiLeo: spotileo?igshid...
    TWITTER;
    Twitter HabariLeo: HabariLeo?s=09

Комментарии • 2

  • @abdulrahmankafuku3449
    @abdulrahmankafuku3449 9 месяцев назад +1

    Duh mama anaupiga mwingi😂😂

  • @enockelia9567
    @enockelia9567 9 месяцев назад

    Mbona km ATC tower km ipo upande wa landside au mi ndo cjaona vizuri....