WAZIRI BASHUNGWA, Akabidhi Vyeti na Kuhitimisha Mafunzo ya Kozi ya Ukamanda na Unadhimu

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 14 окт 2024
  • Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Innocent Bashungwa (Mb) leo Juni 17, 2023 amehitimisha Mafunzo ya Kozi ya Ukamanda na Unadhimu Kundi la 37/22-23, mahafali yaliyofanyika katika Chuo cha Ukamanda na Unadhimu, Duluti, Jijini Arusha. Katika mahafali hayo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, alikuwa Mgeni rasmi ambapo amewatuniku Wahitimu 65 Hadhi ya psc (Pass Staff College) na kuwakabidhi vyeti na zawadi kwa washindi.
    Katika Hotuba yake, Mheshimiwa Waziri Bashungwa, amewapongeza Wahitimu wote na kuwataka wanaporudi maeneo yao ya kazi wakatumie vilivyo maarifa na taaluma wayopata katika Chuo Cha Ukamanda na Unadhimu, Duluti
    Aidha, kwa Wahitimu kutoka Nchi rafiki, Mgeni rasmi amesema anaamini wataendelea kuwa mabalozi wazuri wa Nchi ya Tanzania, ili kudumisha diplomasia ya Ulinzi na urafiki uliopo.
    Naye, Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu, Brigedia Jenerali Sylvester Damian Ghuliku, aliwapongeza Wahitimu na kuwatakia kila la heri wanaporejea kwenye vituo vyao vya kazi na amewahakikishia kuwa, Chuo kinaona Fahari na kujivunia maarifa waliyopata Maafisa hao wakuu kutoka ndani na nje ya Nchi.
    Akitoa maelezo ya Kozi ya Ukamanda na Unadhimu, Kundi la 37/22-23, Mkufunzi Mkuu, Kanali Khaji Maulid Mtengela, alimthibitishia Mgeni rasmi kuwa, Wanafunzi wote wanaohitimu wamefuzu na kufikia viwango vilivyowekwa, hivyo wanastahili kutunukiwa hadhi ya psc.
    #wizarayaulinzi #jwtz #jkt

Комментарии • 7