BoT YAELIMISHA UMMA SABASABA KUHUSU KAZI ZAKE

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 6 окт 2024
  • Benki Kuu ya Tanzania (BoT) hushiriki Maonesho mbalimbali nchini kwa lengo la kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake, ambapo wananchi wanapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo sera za fedha, namna ya kuwekeza katika dhamana za serikali, mifumo ya malipo ya taifa, na namna BoT inavyosimamia sekta ya fedha nchini.
    Vilevile, BoT inaelimisha umma kuhusu utatuzi wa malalamiko ya mtumiaji wa huduma za kifedha, masuala ya ajira na utumishi Benki Kuu, pamoja na nafasi za masomo katika Chuo cha BoT na Bodi ya Bima ya Amana.
    Pia, BoT inatoa elimu kuhusu utambuzi wa alama za usalama katika noti za Tanzania na njia sahihi za utunzaji wa noti na sarafu. Wananchi wanaotembelea banda la BoT hupata fursa ya kuona na kujifunza kwa vitendo alama hizi muhimu zinazosaidia kutambua noti halali za Tanzania.
    Ushiriki wa BoT katika Maonesho ya Sabasaba umewezesha kuwasiliana moja kwa moja na wananchi, kutoa ufafanuzi kuhusu masuala ya kifedha, na kujibu maswali yanayohusiana na kazi za Benki Kuu. J
    Jitihada hizo za BoT zinachangia kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu masuala ya kifedha na kuwajengea uwezo wa kufanya maamuzi sahihi ya kifedha, hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza sekta ya fedha na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Комментарии • 2

  • @JoshuaBundala-cw4ek
    @JoshuaBundala-cw4ek 2 месяца назад

    Naitwa Joshua bundala naomba mnisaidie ninataka kujua kampuni au taasisi zinazotoa mikopo mtandaoni maana Kuna wizi mkubwa sanae

  • @JoshuaBundala-cw4ek
    @JoshuaBundala-cw4ek Месяц назад

    Kuna watu wapo humu mtandaoni wanajiita ni kampuni zinatoa mikopo mtandaoni sasa basi kinafanyika hapo ni kitu Cha ajabu sana unakopa 80 elfu unarudisha laki na nusu je benki kuu mumewapa leseni kufanya biashara kwa riba Kubwa? Kibaya zaidi ndani ya siku saba urudishe ukichelewa unatangazwa Kwa ndugu zako woote