ZIJUE ALAMA ZA DASHBOARD YA GARI YAKO NA MATUMIZI YAKE

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 3 дек 2024

Комментарии • 69

  • @ngusakabinza9238
    @ngusakabinza9238 10 месяцев назад +4

    Unajua kupresent 💯

    • @yourportal
      @yourportal  10 месяцев назад

      Karibu sana Ngusa, Shukrani sana na Tunajivunia wewe. Usisite kushare na wale unaowajali.

  • @ManePaul-c1l
    @ManePaul-c1l 8 дней назад +1

    Naitaji kufahamu udreva wa backho vp inawezekna kuipata

  • @drvidah7030
    @drvidah7030 6 месяцев назад +4

    Aisee unaelezea vizuri sana nimekuelewa kuliko mwalimu wangu anaenifundisha driving😂

    • @yourportal
      @yourportal  6 месяцев назад

      Karibu sana, Usisite kushare na wale unaowajali pamoja na KuSubscribe Channel yetu pia. Ahsante.

  • @Samwelsamwel1152
    @Samwelsamwel1152 Год назад +3

    Asante Santa Kwa mafunzo yako

    • @yourportal
      @yourportal  Год назад

      Karibu sana Anna, Tunajivunia wewe.

  • @lucyasava9266
    @lucyasava9266 4 месяца назад +1

    Asante sana

    • @yourportal
      @yourportal  4 месяца назад

      @@lucyasava9266 Karibu sana, Tunajivunia wewe.

  • @machanohaji9841
    @machanohaji9841 9 месяцев назад

    Asante bro mimi nataka unifanyie mipango nije unifubdishe binafs than baadae nataka niende chuo nikasomee kuendesha ila natakanikienda niwe nnaelewa baadh na mambo

  • @Dullahvoicetz
    @Dullahvoicetz 9 месяцев назад +1

    Nimependa sana jinsi ya kujua usalama wako kwenye dashboard

    • @yourportal
      @yourportal  9 месяцев назад

      Karibu Maneno, Tunajivunia wewe. Usisite kushare na wale unaowajali.

  • @uwezawamungumkuu.amaniafrika
    @uwezawamungumkuu.amaniafrika Год назад +3

    Nilisha uliza mafundi sana swali hili. Gari yangu natoka Arusha hadi dar lakini mshale wa maji inapanda nafasi moja nikipita moshi inashuka mpaka c kama gari aitembei na inapoteza ngurumo kabisa.lakini mshale wa spidi unapanda mpaka 100,220,80. Lakini nikizima kula nikija kuwasha mfano korogwe inapanda tena kidogo nikifika Segera inashuka tena mpaka c na kukata sauti kabisa. Gari ni piston 6 ya petroli. Tatizo nini?. Nikifika rejeta niya baridi. Nikiweka ic joto kinapanda hadi nusu badae inashuka lakini aifiki kwenye c. Je kuna tatizo?. Barikiwa. Amen.

    • @yourportal
      @yourportal  Год назад +1

      Karibu sana Uweza wa Mungu mkuu, Kwa mujibu wa maelezo yako mtafute fundi bingwa aangalie maeneo haya; 1. Atizame sensor inayopima joto la engine kama ipo sawa kwani ndio inayo control ule mshale wa maji/joto la engine kuwa katikati. 2. Atizame ufanyaji kazi wa Pump ya maji ambayo ndio husukuma maji yaliyopoozwa kutoka kwenye rejeta kwenda kwenye engine and vice versa. Kama maeneo yote hayo yapo vizuri, jaribu kuingia online na udownload user manual na car specifications kulingana na aina ya gari yako ili ujue kama imeundwa na mfuno wa kipekee au la! Karibu sana.

    • @uwezawamungumkuu.amaniafrika
      @uwezawamungumkuu.amaniafrika Год назад +2

      Amen amen.sawa. lakini gari aikosi nguvu hata kwenye milima.mfano nilitoka mwanza mlima Sekenke ilipanda na 80. Aichemshi kabisa wala misi akuna. Mwaka jana nilienda njia ya iringa Kitonga nilipanda na 60,80 . Tatizo langu ni mshale wa maji kushuka mpaka c ninapo kwenda kuanzia kilomita 80 na ngurumo kupotea kabisa kiasi kusogelea bila kushika bodi tena kwenye bonet uwezi jua gari ajazimwa. Yote mema nitajaribu. Amani barikiwa nyote kwa darasa lenu. Amen.

    • @daiskilemele9088
      @daiskilemele9088 Год назад

      Mtaalam katka suala la taa ya betry kwa kuongezea hiyo taa ikibakia imewaka solution sio kwenda dukani na kununua bettry bali yafaa ufanyike ukaguzi wa mfumo wa kuchaji bettry katika gari mfano ; autonetor, fenbel, autonetor fuse nk

    • @mashimbazephania3511
      @mashimbazephania3511 7 месяцев назад

      Gari lako halina thermostat nunuwa weka mpya

  • @SiyaleoNdaba
    @SiyaleoNdaba 8 месяцев назад +1

    Kupitia ww naweza kujua kuendesha gari unajua sanaa

    • @yourportal
      @yourportal  8 месяцев назад

      Karibu sana. Tunajivunia wewe. Usisite kushare na wale unaowajali.

  • @AbednegoGwalugwa
    @AbednegoGwalugwa 2 месяца назад +1

    Sijakuelewa kwenye battery kabisa kazi ya battery nikusapoti tu kuwasha gari. Gari ikishawaka battery Haina kazi Tena Bali otonete ndoyo inayobaki kufanya kazi ya uendeshaji wa umeme kwenye gari sar

    • @yourportal
      @yourportal  2 месяца назад

      @@AbednegoGwalugwa Asante kwa Mchango wako, Tunajivunia wewe.

  • @RonnieBertin
    @RonnieBertin 2 месяца назад +1

    Alama ya betri ni otoneta haichaji betri pindi unapostat gari yako otoneta ndo inashughulika na mambo yote. Kama ukiwasha taa ukisiliza redio nk

    • @yourportal
      @yourportal  2 месяца назад

      @@RonnieBertin Karibu sana na Asante kwa Mchango wako Muhimu.

  • @OmaryAbbas
    @OmaryAbbas 2 месяца назад +1

    Una patikana wapi kaka?

    • @yourportal
      @yourportal  2 месяца назад

      @@OmaryAbbas Karibu sana, Tupo Dodoma kwa Sasa.

  • @mashimbazephania3511
    @mashimbazephania3511 7 месяцев назад +4

    Teacher umechemka alama ya oil cyo kupunguwa tu oil inaweza ikawemo na hiyo taa ikawaka hapo umechemka tafuta jibu sahihi unapoamuwa kuelimisha watu, suara la alama ya better unaweza ukaweka jipya bado hiyo alama ikawaka napo tafuta jibu upya jipange kabla haujaamua kuelimisha watu.

    • @yourportal
      @yourportal  7 месяцев назад +7

      Karibu sana Ndugu Mashimba, Tunajivunia wewe. Hoja yako ina mashiko na ni nzuri sana. Tafadhali zingatia YAFUATAYO:
      1. Jitahidi wakati wote unapotaka kuchangia hoja katika platform kama hizi dhamira iwe ni kuongezea uzoefu ulio nao SI kuuonesha umma kwamba wewe ni Bora! La ha sha! Kwa sababu wapo wengine ambao pengine ni bora kushinda sisi sote.
      2. Unapotoa hoja ya kuwa Muelimishaji "AMECHEMKA" tafsiri yake ni kwamba Amepotosha Umma kwa ujumla, Kitu ambacho SI SAHIHI na ni Uchochezi. NB: Muelimishaji ameeleza kuwa ishara ya taa ya oil kuwaka inaashiria upungufu wa oil katika tanki la oil ambao unaweza sababishwa na factors mbalimbali kama kuvuja kwa tank lake ama kutobadili oil kwa muda mrefu ...'NA HIYO NDIYO MAANA KUU YA ILE TAA KWA MUJIBU WA WATENGENEZAJI WA VYOMBO HUSIKA'. Sasa Ungetumia Busara kidogo kujenga Hoja yako Ungesema hivi... {kwa kuongezea, taa ya oil pia inaweza kuwaka kama pump yake ina misbehave au sensor ya oil ina misbehave hivyo kushindwa kupeleka taarifa sahihi kwenye control unit ya gari.} Hivyo hivyo katika Betri, Taa yake Maana Kuu kwa Mujibu wa Watengenezaji NI KUASHIRIA KUWA BETRI YAKO INA TATIZO HIVYO IFANYIE UCHUNGUZI...sasa hizo factor zingine sijui hata ukiweka betri mpya taa inaweza kuwaka pia TUNAITA minor factors ambazo kwa vyovyote vile huwezi kuziorodhesha kwa video ya dk 8 na lazima uzingatie technical awareness ya wale unaowapa uelewa.
      3. Unatakiwa Ufahamu kwamba Video ina serve kusaidia wahitaji kupata COMMON BASICS za Ujuzi wa kutumia chombo cha Usafiri na sio Kumfundisha Mtu kujua Kutengeneza Gari au Kuliunda Gari. NB: Hivyo, Unaposema Muelimishaji 'AJIPANGE' tafsiri yake una hulka ya kupenda 'ARGUMENT' na sio 'DISCUSSION' (you better prefer finding out WHAT IS RIGHT than WHO IS RIGHT).
      4. Hata Tukikupa wewe nafasi UJIPANGE kama unavyosema, Utuletee Darasa...Kamwe huwezi kuwa bora kushinda wengine na hivyo utahitaji mawazo mapya na watakao kupa hawatakwambia 'UMECHEMKA' au 'KAJIPANGE' kwa sababu wana Busara.
      5. Usisahau KUSUBSCRIBE Channel Yetu Hii ili Ufikiwe na Maudhui mengi zaidi na Uweza KU-COMMENT Kwa sababu Tunazihitaji Hoja zako nyingine nyingi ambazo ni Muhimu sana Kwetu. Ahsante.

    • @noelmwaya6783
      @noelmwaya6783 5 месяцев назад +1

      @@yourportal hongera mkuu watu kama hawa hawakosi hata wasipohitajika na yeye kashindwa kuelewa kuwa hili ni darasa mtandaoni sio kila mtu anaweza kuchukua muda mrefu kuangalia video hizo pia wengine ni wajuaji sana hata kama hujakosea atataka akosoe tu

    • @yourportal
      @yourportal  5 месяцев назад

      @@noelmwaya6783 Karibu sana Noel, Asante kwa Mchango wako chanya kabisa. Tunajivunia wewe.

  • @sebastiankatalle2732
    @sebastiankatalle2732 6 месяцев назад +1

    Na ile ABS ikiwaka ndo nn

    • @yourportal
      @yourportal  6 месяцев назад

      Karibu sana, inaashiria kuwa mfumo wa break za gari yako unahitaji uchunguzi zaidi (maranyingi tunaanza kwa kuangalia sensor za ABS kama zinafanya kazi ipasavyo).

    • @sebastiankatalle2732
      @sebastiankatalle2732 6 месяцев назад +1

      @@yourportal Na gari yng imeanza kutoa moshi sana mpka inakuwa kero barabarani.Ukikanyaga msfita tuu inatoa but ukitulia hautoki

    • @yourportal
      @yourportal  6 месяцев назад

      @@sebastiankatalle2732 Tafadhali nenda kacheki piston ring huenda zimesha isha ubora, ama linkage ya oil kwenda kwenye sehemu ya uchomaji mafuta au linkage ya Coolant kwenda kwenye sehemu ya uchomaji mafuta...ikiwa pamoja na mfumo mzima wa exhaust system.

  • @issaselemani491
    @issaselemani491 Год назад +1

    Gari yangu muda wote inawaka hiyo check engine na ninamaliza safari ya km.200 hadi 260 bila tatizo.Hii inamaanisha nini?

    • @yourportal
      @yourportal  Год назад +1

      Karibu sana Issa, kuna mambo 2; Moja, huenda senser inayopeleka taarifa kwenye dashboard ina misbehave kwamaana ya kwamba haiko accurate kudetect hali halisi ya engine. Mbili, huenda Senser iko sawa ila wewe dereva umeshindwa kuitafsiri hiyo taa inaashiria nini kulingana na aina ya gari husika. Kwa ushauri angalia mifumo yote ambayo inahusiana na engine moja kwa moja kama vile: Uwepo wa oil ya kutosha(hakikisha hakuna sehemu inayovujisha oil au KAMA oil imeganda kwenye sample ya tank), Hakikisha uwepo wa Coolant ya kutosha(maji) au KAMA maji yapo angalia mfumo wa Pump kama inasukuma maji vizuri ili yazunguke kwenye ingine ipasavyo. Kitu kingine ni Mfumo wa Feni, cheki vizuri Huenda senser inayocommand feni izunguke haiko active. Mwisho ni Risk Kubwa Kutembea wakati Check engine inawaka! Ukiona imewaka usichukulie poa, pack gari pembeni ita Fundi mpaka agundue nn tatizo na sio akuzimie taa ya cheki engine...Hakikisha anagundua Tatizo kwanza.

  • @khalifasaid0047
    @khalifasaid0047 5 месяцев назад +1

    Unapatikana wapi kuongozi nataka ujuzi wa gari

    • @yourportal
      @yourportal  5 месяцев назад

      @@khalifasaid0047 Karibu sana Khalifa, kwa sasa tupo Dodoma na Dar.

    • @khalifasaid0047
      @khalifasaid0047 5 месяцев назад +1

      @@yourportal duuh sasa m kiongozi nipo znz sasa huduma hiyo nitaipataje

    • @yourportal
      @yourportal  5 месяцев назад

      @@khalifasaid0047 Karibu, Tutafanya mawasiliano.

    • @khalifasaid0047
      @khalifasaid0047 5 месяцев назад

      @@yourportal basi naomba namba yako ya whtsap

  • @BensonMwangi-f2z
    @BensonMwangi-f2z Год назад +1

    Thanks

    • @yourportal
      @yourportal  Год назад

      Karibu sana! Tunajivunia wewe. Usisite kushare na unaowajali.

  • @ArafatOmar-d3b
    @ArafatOmar-d3b Год назад +1

    Majibu yangu sijapata mkuu

  • @luckysichone6705
    @luckysichone6705 Год назад +1

    Nashukulu Sana kiongozi wangu MUNGU akubaliki sana

    • @yourportal
      @yourportal  Год назад

      Karibu sana Lucky, Tunajivunia wewe. Usisite kushare na wale unaowajali ili Tubarikiwe sote🙏

    • @luckysichone6705
      @luckysichone6705 Год назад

      @@yourportal Amina kiongozi wangu

  • @ArafatOmar-d3b
    @ArafatOmar-d3b Год назад

    Asante sana tumejua,naomba kuuliza kuna utaalaam wowote kupitsha gar kwenye barabara yenye michanga mingi,kama haina four weel?

    • @yourportal
      @yourportal  Год назад +1

      Karibu sana! Kwa kawaida Sehemu zenye Michanga huwa Tunatumia Low gear, kwenye gari yenye automatic transmission Kuna Gear inaitwa 'L' so unaweka hiyo ili gari iwe nzito iweze kupita mchangani.

  • @fabianemmanuel6253
    @fabianemmanuel6253 Год назад +1

    Ahsant kwa darasa

    • @yourportal
      @yourportal  Год назад

      Karibu sana Fabian, Tunajivunia wewe. Usisite kushare na wale unaowajali.

  • @SaidTulia-d9j
    @SaidTulia-d9j 3 месяца назад +1

    Abari kaka

  • @ArafatOmar-d3b
    @ArafatOmar-d3b Год назад +1

    Naishi kwenye barabara za michanga sana kama kuna utaalaam wowote nielekeze pliz

    • @yourportal
      @yourportal  8 месяцев назад

      Karibu sana, Jitahidi kutumia gear namba 2 au L

    • @FredyKimale
      @FredyKimale 7 месяцев назад +1

      Asante kwa mafunzo mazuri! Naomba tuletee mafunzo ya namna ya kukagua injini na gear Box pls

    • @yourportal
      @yourportal  7 месяцев назад

      @@FredyKimale Karibu sana Fredy, Tunajivunia wewe. Hivi karibuni tutaleta tutorial kuhusu Engine na Gear box. Ahsante.

  • @drvidah7030
    @drvidah7030 6 месяцев назад +1

    Mfano unanunua gari kwa mtu.,,,atleast iwe imetembea kilometer ngapi ili na wewe uweze kulitumia kwa muda bila kuharibika

    • @yourportal
      @yourportal  6 месяцев назад

      Karibu sana, Tunajivunia wewe. Kitu cha msingi sana kabla hujaangalia idadi ya kilometers, ni namna Gari lilivyotunzwa vizuri na mmiliki husika. Naamanisha, unaweza kuta Gari ina kilometers nyingi lkn aliyekuwa anaitumia alikuwa anafanya services kwa wakati na alikuwa anazingatia uendeshaji wa kistaarabu...hivyo utatambua kuwa gari ilitunzwa kupitia ukaguzi wa engine, gearbox na suspension system nzima ya Gari. Lkn kigezo cha kilometers pia ni muhimu na husaidia kujua ni wakati gani ufanye overhaul ya engine (kuisafisha engine kwa ujumla kila baada ya kilometers 100,000) ili kuendelea kuliwega gari lako ktk hali nzuri, bora na salama wakati wote uwapo safarini. Lkn kiujumla watu wengi hupendelea kununua gari ikiwa kabla haijafika kilometers 100,000 (laki moja) ili hata kama ataitunza vizuri yeye mwenyewe ndio awe wa kwanza kuifanyia overhaul kwa mafundi wanaoaminika ktk utalaam wa mfumo wa engine. Ahsante.

  • @ziadaskitchen5060
    @ziadaskitchen5060 Год назад +1

    Nini nifanye ili nifaulu kwa haraka maana kilanikijifunza sielewi asant

    • @yourportal
      @yourportal  Год назад

      Karibu sana Ziada, zidisha tu umakini lazima utaelewa.

  • @robytechnicalservise
    @robytechnicalservise Год назад +1

    Vizuri mkuu

    • @yourportal
      @yourportal  Год назад

      Karibu sana Roby, tunajivunia wewe. Usisite kushare na wale unaowajali.

  • @ArafatOmar-d3b
    @ArafatOmar-d3b Год назад

    Naishi kwenye sehemu ya michanga mingi sana kila siku nakwama

    • @yourportal
      @yourportal  3 месяца назад

      Tafadhali, fuatilia maelekezo kwenye video hii utapata msaada.

  • @AnnaYohana-mj3vw
    @AnnaYohana-mj3vw Год назад +1

    Mimi naitaji kujifunza gari

    • @yourportal
      @yourportal  Год назад

      Karibu Anna, Tunajivunia wewe.