ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 12 ZIMEPATIKANA KWENYE HARAMBEE UJENZI WA KANISA LA TAG MASHUJAA MAKAMBAKO

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 15 сен 2024
  • Fedha zaidi ya shilingi milioni 12 na laki tatu zimepatikana katika harambee ya ujenzi wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Mashujaa lililopo kata ya Kivavi mjini Makambako wilayani Njombe huku mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Songwe @daniel_godfrey_chongolo akichangia kiasi cha shilingi milioni nne.
    Katika fedha hizo kiasi cha shilingi 5,790,000 taslimu kimepatikana huku ahadi ikiwa ni milioni 6,540,000,
    Akiwasilisha mchango huo mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kanisa hilo ambaye ni diwani wa kata ya Kivavi Alimwimike Sawhi amesema Chongolo amechangia kiasi hicho baada ya kualikwa kuwa mgeni rasmi, huku akitaka kanisa hilo kutumika kurejesha maadili mema katika jamii.
    Mchungaji wa kanisa hilo Raphael Migodela amemshukuru mkuu wa mkoa wa Songwe kwa mchango huo na kueleza kuwa kanisa hilo litakuwa mstari wa mbele kuhamasisha jamii kuachana na imani za kishirikina ambazo zinepelekea mauaji kwenye jamii.
    Nao baadhi ya waamini wa kanisa hilo Godfrey Mabena, Frola Mwakanyamale wamewataka viongozi wa serikali na kisiasa kuwekeza kwenye ujenzi wa makanisa kwani huko ndio chanzo cha amani.

Комментарии •