MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA BARABARA -DAR- ES SALAAM

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 14 окт 2024
  • MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA BARABARA DAR ES SALAAM
    Katika kipindi cha miaka mitatu Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetekeleza zaidi ya miradi 11 katika Jijini la Dar- es Salaam kati ya hiyo mradi 8 ni mikubwa ya kimkakati na 3 ni midogo ambayo itasaidia kutatua changamoto za barabara kutopitika vizuri na kupunguza msongamano wa magari.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari tarehe 11 Machi 2024 kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika Sekta ujenzi wa miundiombinu ya barabara na Madaraja; Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar- es Salaam Mha. John Mkumbo amesema kati ya miradi hiyo 5 imekamilika na 6 inaendelea kutekelezwa.
    Amesema miongoni mwa miradi ya maendeleo inayotekelezwa ni pamoja na mabasi ya mwendo wa haraka awamu ya pili (BRT 2) katika barabara ya Da- es Salaam - Kongowe eneo la Mbagala Rangi tatu, Chang’ombe (Keko- Mgulani JKT), Kawawa (Veta Chang’ombe JCT- Magomeni Mapipa) na Sokoine ambapo mradi umefikia 98%.
    Amesema ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo haraka Awamu ya tatu (BRT 3) km 23 katika barabara ya Tanganyika Motors - DIA TI, Uhuru (Buguruni - Msimbazi ) Bibi titi na Shauri moyo ( Karume - Bohari), unaendelea pamoja na ujenzi wa miundombinu ya Mabasi yaendayo haraka awamu ya nne (BRT 4) unaoanzia maktaba ya Taifa - Mwenge - Sam Nujoma km 13.5 ambao unapita pia katika barabara ya Mwenge - hadi (DAWASA) Tegeta km 15.63.
    Pia kuna utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa barabara ya Morogoro kutoka njia mbili kwenda njia nane km 19 na maegesho ya magari Kiluvya yenye urefu wa mita za mraba 36,000 awamu ya kwanza ikihusisha ujenzi wa maegesho yenye ukubwa wa mita za mraba 18,000 yatakayokuwa na uwezo wa kuchukua wastani wa malori zaidi ya 200 kwa siku, lengo ni kuondoa maegesho yasiyorasmi pembezoni mwa barabara ya mandela na hivyo kupunguza foleni zinazoweza kuepukika.
    Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara ikiwemo matengenezo ya muda maalum, matengenezo ya kawaida, matengenezo ya maeneo korofi na matengenezo ya madaraja ambapo kazi hizo zimekuwa zikitekelezwa na Wakandarasi wazawa ambapo kwa mwaka wa fedha 2023/ 2024 jumla ya miradi 33 imetekelezwa na Wakandarasi wazawa.

Комментарии • 19

  • @juma3473
    @juma3473 6 месяцев назад

    Barabara za juu zijengwe nyingi

  • @nickjustin2023
    @nickjustin2023 7 месяцев назад +6

    Muache kujenga barabara za line 4 kwa dar mji unakua huu, tunahitaji line kuanzia nane/nne kila upande..

  • @azmankiddo8872
    @azmankiddo8872 5 месяцев назад +1

    Barabara ya Haile Selassie ya Masaki itanueni hata kwa njia nne inatutia aibu hususani ikiwa kwenye maeneo tunayosema ya kitajiri Tz🙏🏾

  • @Kamikaze-ks9hr
    @Kamikaze-ks9hr 7 месяцев назад +2

    Tunahitaji fly over mwenge na morroco wakuu

  • @MustwafaSalum
    @MustwafaSalum 6 месяцев назад

    Nimekuelewa muheshiwa mirrradi

  • @omarysaid8725
    @omarysaid8725 7 месяцев назад +3

    Hapa ndio nimeamini kuwa Tanzania hatuna wakandarasi washauri Tanroad dah maana sio kwa mikona ile ya barabara ya tazara kuelekea gongo la mboto pale tumepigwa kweupe barabara nyembamba ujunga mtupu mji una kuwa huu bado tupo kwenye barabara line mbiki tu tupo kizamani sana hebu tanroad jiongezeni bhana

  • @MubarakaCloud
    @MubarakaCloud 7 месяцев назад +1

    Vipi kuhus fly over katika makutano ya mwenge na pale morroco ?

  • @omarysaid8725
    @omarysaid8725 7 месяцев назад +1

    Mnajenga BRT mabasi hakuna aisee hii nchi ya hovyo sana mbagala barabara imeisha lkn hakuna maendeleo mpaka leo

  • @omarysaid8725
    @omarysaid8725 7 месяцев назад +2

    Barabara mbili kwenda mbili kurudi mpaka miaka hii badirikeni miji inakuwa maendeleo yana hitajika sasa hapo mnatatua tatizo la foleni au mna ongeza foleni barabara zina kona kama kitonga kumbe Dar sidhani kama JPM ange kuwa hai kama ujinga huu unge fanyika hapa lazima kuna upigaji tu halafu jitu lina jisifu kama mhandisi mshauri sasa hapa kuna ushauri gani kwa kona hizo na wembamba huo

  • @omarysaid8725
    @omarysaid8725 7 месяцев назад

    Katika serikali ya awamu hii sijaona maendeleo yoyote yale wala mafanikio yoyote yale tuliyo piga kama nchi kwa ujumla miradi mikubwa ina lala ndio maana huwa sisikilizagi mimi mambo ya serikali

  • @omarybakunda2554
    @omarybakunda2554 7 месяцев назад

    Komaeni

  • @silasurio4645
    @silasurio4645 7 месяцев назад +1

    Vipi kuhusu Arusha mbona imetelekezwa wakati ndio mji wa kitalii kwa nchi yetu

    • @elinamilyatuu7337
      @elinamilyatuu7337 7 месяцев назад

      Imetelekezwaje..?

    • @abdulpagali7476
      @abdulpagali7476 7 месяцев назад +1

      Barabara za baiskeli na bodaboda. Utalii hauhitaji barabara za lami zinaweza kuharibu mazingira ya mbuga za wanyama pori. Ndiyo maana wana harakati wa mazingira wanatukataza kujenga miundombinu ya usafirishaji mbugani.

    • @homeboybeyondtheborders4935
      @homeboybeyondtheborders4935 7 месяцев назад +2

      Arusha wana Barbara nzuri kuliko mwanza

    • @brysonkaale3003
      @brysonkaale3003 7 месяцев назад +1

      Kwanini mnasema mnamshukuru Mama Samia badala ya kusema mnaishukuru serikali?,

  • @homeboybeyondtheborders4935
    @homeboybeyondtheborders4935 7 месяцев назад +1

    Miji yetu inakosa mipango miji sijui kwa nini

    • @omarysaid8725
      @omarysaid8725 7 месяцев назад +1

      Tatizo ni upigaji na wahandisi washauri walio pewa dhamana wanalala tu kazi kufuga vitambi