TUNAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUREJESHA MIKOPO YA 10% - MKURUGENZI ELIHURUMA MABELYA

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 5 окт 2024
  • Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndg. Elihuruma Mabelya ameeleza kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inatekeleza agizo la Serikali la kuhakikisha Wasimamizi, Waratibu na Wajumbe wa Kamati za huduma ya mikopo kuanzia ngazi ya Kata, Halmashauri na Wilaya wanapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo katika utoaji na usimamizi wa mikopo kwa kutumia mfumo mpya.
    Mkurugenzi Mabelya ameyasema hayo leo Octoba 04, 2014 wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wajumbe wa Kamati za Huduma za mikopo ngazi ya Kata, Halmashuri na Wilaya ya utoaji na usimamizi wa mikopo ya asilimia (10%) kwa vikundi vya Wananwake, Vijana na Watu wenye ulemavu yanayofanyika kwa muda wa siku 3 katika Ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Iliyopo Kibaha Mkoani Pwani.
    "Mnano mwezi Aprili, 2024 Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alitangaza kurejesha tena utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kuanzia Julai 2024 kwa utaratibu wa kutumia benki kwa Halmashauri 10 za majaribio Halmashauri ya jiji la Dar es salaam ikiwa ni mojawapo hivyo niwahakikishie tu baada ya mafunzo haya nitashirikiana na Watendaji wangu kuhakikisha mikopo hiyo inatolewa kwa ufanisi pia nitoe rai kwenu kuhakikisha mnawajibika katika kushiriki, utulivu na uelewa ili mkatende kwa weledi na kuongeza ufanisi na tija zaidi ili kutimiza maono ya Mheshimiwa Rais ya kuwakwamua Wananchi kiuchumi". Alisema Mkurugenzi Mabelya.
    Aidha Ndugu Mabelya ameeleza kuwa Serikali imeanza kutoa mikopo ya asilimia 10 baada ya hapo awali kusitishwa kutokana na changamoto zilizojitokeza huku akimshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kurejesha mikopo ya asilimia 10 na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuwa miongoni mwa Halmashauri zilizochaguliwa kwa awamu nyingine.

Комментарии •