SWALI: Mwanamke anapomaliza EDA ya kufiwa au kuachwa je anatakiwa Afanye nini....???
HTML-код
- Опубликовано: 7 фев 2025
- Eda ni muhula maalum ambao mwanamke, aliyekwisha olewa, anatakiwa kusalia bila ya kuolewa wala kuposwa kutokana na mojawapo wa sababu mbili kuu:
A. kutalikiwa\kuachwa au kuachika na
B. Kufiwa na mumewe (au mume kutoweka au kukimbia pasipo kujulikana aliko…).
#MwanamkeanapomalizaEDAyakufiwaaukuachwajeanatakiwaAfanyenini #EDAndioniniaumaanayakenini #Edazikozaainangapi #niniHekimayaEda
Kwa maana hiyo, Eda ni muhula wa wajibu, uliofaradhishwa ndani ya Qur’ani Tukufu na Hadithi za Mtume ﷺ ambazo ziko nyingi. Mwenyezi Mungu anasema:
وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلاَثَةَ قُرُوَءٍ وَلاَ يَحِلُّ لَهُنَّ أَن يَكْتُمْنَ مَا خَلَقَ اللّهُ فِي أَرْحَامِهِنَّ )
. وقوله تعالى (وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجاً يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْراً )
“Na wanawake walioachwa (watalikiwa): wangoje (wasiolewe) mpaka tohara tatu zishe. Wala haiwajuzii kuficha mimba aliyoumba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao, ikiwa wanamuamini Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho”.Q;2.28.
“Na wale wanaofiwa na waume zao, miongoni mwenu na kuacha wake, wake hao wangoje (wakae eda) miezi mine na siku kumi.” Q.2:34.
Ama mja mzito aliyefiwa na mumewe, basi eda yake ni tokea tarehe ya kufa mumewe hadi ajifungue.
Vivyo hivyo, mtalikiwa mja mzito, eda yake ni hadi kujifungua.
Akijifungua tu basi eda yake imeisha.
(وَأُوْلَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ ).
“Na wale waja wazito, basi muhula wao ni pale watapotua ujauzito wao.”
Ama mwanamke alieachwa kabla ya kujamiiana na mumewe, yeye hakai eda yoyote, na wala hana mahari -iwapo mahari hayo hayakutajwa kinaganaga-, isipokuwa kiliwazo (i.e. kiacha nyumba, yaani kitu cha kuanzia maisha ya ujane).
Lakini ikiwa kima cha mahari kilishatajwa na akaachwa kabla ya kujamiana na mumewe, basi mwanamke huyo, pamoja na kwamba hakai eda, anapaswa kulipwa nusu ya mahari ya kima kilichotajwa; ila kama yeye mwenyewe au walii wake (mzee wake, kwa mwanamwari) atasamehe malipo hayo Q.2;37. Na katika aya nyengine Q.33.49 Mwenyezi Mungu anasema:
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَكَحْتُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ فَمَا لَكُمْ عَلَيْهِنَّ مِنْ عِدَّةٍ تَعْتَدُّونَهَا فَمَتِّعُوهُنَّ وَسَرِّحُوهُنَّ سَرَاحاً جَمِيلاً )
“ Enyi mlioamini! Mtakapowaoa wanawame; wenye kuamini kisha mkawpa talaka kabla ya kuwagusa (kuingiliana kimwili), basi hamna eda juu yao mtakayoihisabu. Na wapeni cha kuwaliwaza na muwawache muachano mzuri” Q.33.49.
Ama mwanamke anayefiwa na mume basi eda yake ni miezi mine na siku kumi, kama nilivyotaja hapo juu na kunakili aya ya Qur áni. Na ni sawa ikiwa mume huyo alikwisha jamiiana na mkewe au la; mke atakaa eda ya miezi mine na siku kumi. Yaani, mfiwa na mume anakaa eda ya miezi mine na siku kumi. Iwapo ana mimba basi mpaka ajifungue.
Vile vile, mke huyo anamrithi mumewe huyo aliyefariki, awe aliingiliana naye kimwili au la. Kama mume hakuacha mtoto au watoto (kwa mke mwengine, kwa mfano) basi mwanamke atarithi robo ya mali yote ya mume na kama mume aliacha mtoto au watoto basi mke atarithi thumuni (one eighth) ya mali yote ya mume.
Hivyo ndivyo alivyoamua Mtume ﷺ kwa Sahaba mmoja aliyekuwa akiitwa: Ma’qal Ibn Yasar ambaye alifariki na kuacha mke kabla ya kuingiliana naye kimwili.
Hali kadhalika, Ibn Masúd - mmoja wa Maswahaba wakubwa- alikabiliwa na kesi kama hiyo ya mke kufiwa na mume ambaye bado hajaingiliana naye kimwili. Ibn Mas’ud akatoa fatwa ya mke kukaa Eda na pia kumrithi mumewe. Akapewa khabari kuwa Mtume ﷺ alitoa hukumu kama hiyo kwa Ma’qal Ibn Yasar! Ibn Mas’ud alifurahi sana kuona kuwa hukumu yake imewiana na hukumu ya Mtume ﷺ .
Pili, ni muhimu kujua kwamba mwanamke anakaa eda kwenye nyumba ya mumewe, awe mume yuhai au la, na katika muhula wote wa eda, mwanamke huyo anaendelea kulishwa kama kawaida kuktokana na mali ya mume, mpaka eda yake ishe. Mwenyezi Mungu anasema:
(لَا تُخْرِجُوهُنَّ مِنْ بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخْرُج
Yupi Yatima Zaidi Aliyefiwa Na Mama Au Baba?
👇👇👇👇👇👇
ruclips.net/video/Muaf6zyM_Iw/видео.html