Unatoka Wapi na Unakwenda Wapi? | Ibada ya Mkesha wa Mwaka Mpya 2025 | Rev. Dr. Eliona Kimaro

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 8 фев 2025
  • IBADA YA MKESHA WA MWAKA MPYA
    31/12/2024
    UJUMBE WA LEO: UNATOKA WAPI NA UNAENDA WAPI?
    WHERE HAVE YOU COME FROM AND WHERE ARE YOU GOING?
    ( 2025 NI MWAKA WA YUBILE KATIKA MAISHA YAKO )
    2 Wakorintho 9 : 15
    15 Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu kama ipasavyo.
    Mwanzo 16 : 5 - 12
    5 Sarai akamwambia Abramu, Ubaya ulionipata na uwe juu yako; nimekupa mjakazi wangu kifuani mwako, naye alipoona kwamba amepata mimba, mimi nimekuwa duni machoni pake. Bwana na ahukumu kati ya mimi na wewe.
    6 Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mkononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake.
    7 Malaika wa Bwana akamwona kwenye chemchemi ya maji katika jangwa, chemchemi iliyoko katika njia ya kuendea Shuri.
    8 Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, nawe unakwenda wapi? Akanena, Nakimbia mimi kutoka mbele ya bibi yangu Sarai.
    9 Malaika wa Bwana akamwambia, Rudi kwa bibi yako, ukanyenyekee chini ya mikono yake.
    10 Malaika wa Bwana akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi.
    Walawi 25 : 13
    13 Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake.
    Leviticus 25 : 13
    IN THE YEAR OF THIS JUBILE YE SHALL RETURN EVERY MAN UNTO HIS POSSESSION
    NAUTANGAZA MWAKA WA 2025 KUWA MWAKA WA YUBILE KATIKA MAISHA YAKO
    UNATOKA WAPI NA UNAKWENDA WAPI?
    (2025 MWAKA WA YUBILEE) :WATU 25 KATIKA BIBLIA:
    1 . ADAMU alitokea kwenye udongo/mavumbi/kifusi na akawa mwanasayansi bingwa kwa kuvitambua na kuviita majina viumbe na mimea bila kwenda chuo kikuu cha SUA.
    2. IBRAHIMU alitokea kwenye upagani na kuwa Baba wa Imani
    3. SARAH Alitokea kuwa mwanamke tasa aliyekoma kibaiyolojia na kuzaa Taifa.
    4. ISAKA: alitokea kwenye njaa kali na kulima ktk Nchi ya ugeni na akavuna kipimo kimoja kwa mia. Akawa mkuu sana ktk nchi hiyo ya gerari. Mtu mmoja akaizidi Nchi kwa uchumi na FEDHA.
    5. YAKOBO: alitoka nyumbani kwa Baba yake na kuvuka mto akiwa na fimbo yake tu na akarudi kutoka kwa Labani na kwenda kwa Baba yake akiwa na matuo mawili ya utajiri
    6. YUSUFU: alitoka kwa ndugu zake na aliuzwa kwenda Misri akiwa uchi, na baadae akawa waziri mkuu na kuilisha Dunia miaka saba.
    7. MUSA: alitoka Misri na kukimbia nchi kwa kesi ya mauaji, na akarudi kama mkombozi wa Israel na Bwana kwa farao. Huyo Musa Maneno ya watu yalimtisha na kumwondosha, ila Neno la Mungu lilisema naye kutoka kijitini na kumtia ujasiri wa kurudi.NDANI YA KIJITI MUNGU ALISEMA NA MUSA.
    8. YOSHUA: alitkea kuwa mjakazi wa Musa mpaka kuwarithisha Israel Nchi kwa kupigana vita kiwango cha kulisimamisha Jua.
    9. RAHABU: alitoka kuwa kahaba mpaka kuingia kwenye kitabu cha ukoo wa Yesu. GRANDMOTHER WA YESU.
    10. YEFTHA: alitokea kuwa mtoto wa mwanamke kahaba, mwana haramu mpaka kuwa mtawala wa kuliongoza Taifa la Israel.
    11. SAMSONI :mtoto wa Mwanamke tasa aliyeipiga serikali ya wafilisti miaka mingi. Jeshi la mtu mmoja.
    12. GIDEON :kijana mdogo kutokea familia masikini kabisa na akaliongoza na kulihamua taifa la Israel miaka mingi.
    13. SAMWEL :mtoto wa Mwanamke tasa na kuwa kuhani ktk Taifa la Israel na kuwapaka mafuta WAFALME mawili wa Israel yaani Sauli na Daudi.
    14. RUTH: Kutoka kwenye ujane na Utasa na kuzaa wafalme
    15. DAUDI : tokea kuwa Mchungaji wa kondoo porini na kuwa mfalme wa pili wa Israel.
    16. MEFIBOSHETHI :kutoka kwenye LAANA YA NYUMBA YA SAULI Hadi kukaa mezani pa mfalme.
    17. ESTA: kutokea kuwa Yatima mtumwa na mkimbizi toka Israel na kuwa Malkia wa Babeli yote.
    18. MORDEKAI : tokea kuwa kuwa mtumwa, mkimbizi na kibarua wa ulinzi ikulu mpaka kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo ya ugenini Babeli.
    19. AYUBU: Kutoka kwenye Aibu na kufulia na KUHESHIMIKA TENA MJINI.
    20. DANIELI: tokea kuwa mateka, mtumwa na mfungwa na kuwa Waziri mkuu ktk serikali mbili za Babeli.
    21. YESU KRISTO: mwana wa BIKIRA maria, aliyezaliwa ktk hori ya kulia Ng'ombe, aliyekosa nafasi ktk nyumba ya wageni, ALIYEVIKWA TAJI YA MIIBA hapo kwanza na kuvalishwa taji ya Dhahabu na kupata nafasi ya kuketishwa mkono wa kuume wa Mungu Mwenyezi.
    22. PETRO: kutokea kuwa mvuvi wa samaki na kutoka ktk mashaka makubwa ya kumkana Yesu mara tatu, na baadaye kuhubiri na kumfufua Dorkas toka kwa wafu, na kuwa Askofu wa kwanza wa Kanisa
    23. MTU ALIYEPOOZA miaka mingi na kubebwa na marafiki...alijitwika Godoro lake na kwenda mwenyewe AKIJITEGEMEA
    24. PAULO MTUME tokea kuwa muuaji na kuwa muhubiri mkubwa wa Injili na kufufua wafu.
    25. MWIZI PALE MSALABANI: Kutoka ujambazi na hukumu ya kufa msalabani na kwenda Peponi/Paradiso
    Mhubiri: Rev. Dr. Eliona Kimaro
    Kwa maombi na ushauri :
    Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
    Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053

Комментарии • 58

  • @DorcasNzau-qk2ki
    @DorcasNzau-qk2ki 5 дней назад

    Mchungaji Mungu akubariki ninasikia neno linanigusa sana. Amen 🙏

  • @odethamlyuka2552
    @odethamlyuka2552 Месяц назад +1

    Amen Imekuwa

  • @DerickMollel-b2d
    @DerickMollel-b2d 28 дней назад

    Ahsante mungu kwa kuniunganisha na mtumishi wako sijuti kabisa kumjua..tunabarikiwa mafundisho mazuri🙏🙏

  • @RehemaOscar-e5g
    @RehemaOscar-e5g Месяц назад

    Amina mtumishi ni natoka kwenye njaa ni na kwenda kwenye utukufu🙏🙏

  • @Given-g4g
    @Given-g4g 16 дней назад

    Hallelujah

  • @selinalawala2270
    @selinalawala2270 Месяц назад +2

    Amen, mchg Mungu akubariki sana kwa somo hili, hakika tuna kila sababu ya kushukuru, Mungu ametupendelea sana.

  • @elishiliamathayo8796
    @elishiliamathayo8796 Месяц назад +2

    Asante Mungu kwa kuniunganisha na madhabau hii

  • @rachelmwangoka3290
    @rachelmwangoka3290 18 дней назад

    Amen

  • @aisakibile-tv6th
    @aisakibile-tv6th Месяц назад

    Hakika ni ujumbe sahihi kabisa tunatoka wapi tunakwenda wapi ?Mungu akuinue zaidi mchungaji Kimaro

  • @MamaUisso
    @MamaUisso Месяц назад +9

    Mchungaji Mungu azidi kukuinua nimekuelewa naomba Mungu awaonekanie na wengine ktk hu ujumbe wa leo

    • @joyceurassa-n7r
      @joyceurassa-n7r Месяц назад +4

      Asante Yesu kwa zawadi ya uhai ktk mwaka huu mpya wa 2025.Naomba uso wako utembee nami na familia yangu kila hatua

    • @joyceurassa-n7r
      @joyceurassa-n7r Месяц назад +1

      Aminaa

  • @fifiyambayamba4121
    @fifiyambayamba4121 14 дней назад

    Ameeeeeen and Ameeeeeeeeeen

  • @marundimahugija8168
    @marundimahugija8168 Месяц назад +1

    Keep fire burning Pastor,lzm mtu binafsi akubali kufanya Critical Personal Evaluation,nzuri mnoooo

  • @abelpilato8851
    @abelpilato8851 Месяц назад +2

    Hakika mtumishi nimefundishika na kufaidika na umenitia moyo sana wa kuendelea na safari ya upambanaji wa maisha ili kuitimiza wajibu wangu nilioitiwa na mungu hakika homilia yako imenijenga mungu akusatunze Dr.

  • @helinahenry2363
    @helinahenry2363 Месяц назад

    Mungu nitengenezee heshima.

  • @michaelmusyoki1838
    @michaelmusyoki1838 Месяц назад +1

    That's a great message to many during the year

  • @JoshuaHilgath
    @JoshuaHilgath Месяц назад

    Nina sikia Neno la BWANA Asante baba ❤❤

  • @qatarrarre30
    @qatarrarre30 Месяц назад +7

    I'm blessed very much na neno hili LA mungu,hunatoka wapi,ukie nda wapi🙏🙏

  • @liliancharles8139
    @liliancharles8139 Месяц назад

    Amina 🙏🙏🙏

  • @MARTINEKUBUYA
    @MARTINEKUBUYA Месяц назад

    Be blessed pastor be blessed in the name of our Lord Jesus Christ

  • @Majaliwa2024
    @Majaliwa2024 Месяц назад +2

    Hili ni jembe la YESU penda you sana

  • @IsaakChuwa
    @IsaakChuwa Месяц назад

    Amen

  • @helinahenry2363
    @helinahenry2363 Месяц назад

    Amen, naenda kwenye Amani 2025

  • @MericyMdegela
    @MericyMdegela Месяц назад

    It's powerful 🔥🔥.. Be blessed pastor

  • @rogersodero3897
    @rogersodero3897 Месяц назад

    Amen nimebarikiwa sana.

  • @JoshuaHilgath
    @JoshuaHilgath Месяц назад

    AMINA AMINA 👏🏼 👏🏼👏🏼👏🏼👏🏼👏🏼👏🏼👏🏼

  • @serafinkimaro1308
    @serafinkimaro1308 Месяц назад

    Im highly blessed

  • @maureenmgeni
    @maureenmgeni Месяц назад

    Aminaa, I'm blessed

  • @leahmollel6589
    @leahmollel6589 Месяц назад

    Ninatoka wapi na ninakwenda wapi? Yesu nisaidie🙏🙏🙏

  • @MargaretLuseko
    @MargaretLuseko Месяц назад

    Your Msg is a blessing to many of us, Thank you so much 🙏🏾

  • @JohnBosco-d3g
    @JohnBosco-d3g Месяц назад

    Mwamba safi sanaaaa
    Where are we coming from?
    From Lugambwaz hospitals to Maji, udongo, ña vitambaa vya upako!!!
    Na mkuu wa Mkoa yupo hapo na Rais Samia wanashabikia huo upuuzi!!!
    Mkuu umepiga kwenye mshono!!!!!

  • @jescannko4757
    @jescannko4757 Месяц назад

    Amiiiiiiiiiiiina 🙏🙏🏻🙏🏻

  • @SambaZainab
    @SambaZainab Месяц назад

    Amen mtumishi

  • @helinahenry2363
    @helinahenry2363 Месяц назад

    Amen👏👏👏

  • @rosekieti7902
    @rosekieti7902 Месяц назад

    Thank you God 🙏

  • @JoshuaHilgath
    @JoshuaHilgath Месяц назад

    Amina Amina

  • @agathamburu8910
    @agathamburu8910 Месяц назад

    HOLY NAME OF JESUS IS POWERFUL.AMEN

  • @TijaLilawola
    @TijaLilawola Месяц назад

    Amen

  • @justinendondi
    @justinendondi Месяц назад

    Naomba namba yamchungaji

  • @MARTINEKUBUYA
    @MARTINEKUBUYA Месяц назад

    Amen amen 🙏

  • @janechengula2833
    @janechengula2833 Месяц назад

    Amen 🙏🙏

  • @ritapiusnicolaus7068
    @ritapiusnicolaus7068 Месяц назад

    Amen 🙏

  • @dinahk.7622
    @dinahk.7622 Месяц назад

    Hallelujah

  • @dinahk.7622
    @dinahk.7622 Месяц назад

    Amen in Jesus name

  • @joycemoshi1515
    @joycemoshi1515 Месяц назад

    Ameen.

  • @upendokiwanga9538
    @upendokiwanga9538 Месяц назад

    Injili yenye uhai

  • @Nepasaka
    @Nepasaka Месяц назад

    ❤❤❤

  • @kilimanjarotv255
    @kilimanjarotv255 Месяц назад +2

    NAOMBENI MNIOMBE KWA MUNGU WATU WA MUNGU NILIWAHI KUMUUDHI MUNGU KWA KUMTUKANA KWAKWELI TOKA APO MAISHA YANGU YAMEKUA MACHUNGU HAPA DUNIA NI NI KWA SABABU YA KUCHANGANYA IMANI LEO BARIDI KESHO MOTO MARA VUGU VUGU YANI KWA KWELI NIMEFIKA 2025 ILA NATAMANI INGEKUA NI MWAKA JANA AU JUZI MATUMAINI YAMEKUA MADOGO NAITAJI MAOMBI YENU WATU WA MUNGU NIOMBENI KWA MUNGU ANISAME TURUDI KAMA ZAMANI MAANA LIKITAJWA JINA LA MUNGU TU NAPATA SHIDA SANAA SIJUI NIKIONANANE NITAMUAMBIA NINI NIKIMUONA

  • @Asurasimwandiya
    @Asurasimwandiya Месяц назад

    Nafarijika Sana kusikia mahubiri yako babangu 😭😭🤦

  • @barnabasmakilika-j1f
    @barnabasmakilika-j1f Месяц назад

    naombeni namba ya pastor

  • @MiriumMbwambo
    @MiriumMbwambo Месяц назад

    Kila siku Kila saa umwaminifu bwana,ulindwe nabwana

  • @helinahenry2363
    @helinahenry2363 Месяц назад

    🤣🤣🤣👏👏👏👏

  • @kilimanjarotv255
    @kilimanjarotv255 Месяц назад

    JINA CLIFFORD WALTER MAKWAIYA MAOMBI YENU KWA MUNGU JAMANI NIVUKE HAYA MAJARIBU HALI YANGU SIO NZURI

  • @irakazaeriekim4753
    @irakazaeriekim4753 Месяц назад

    Amiiin🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮

  • @georgengugi-h7l
    @georgengugi-h7l 16 дней назад

    Amen

  • @esmilykipele4008
    @esmilykipele4008 Месяц назад

    Amen

  • @rosekieti7902
    @rosekieti7902 Месяц назад +1

    Amen 🙏