JINSI YA KUACHILIA DAMU YA YESU KATIKA KILA ENEO LA MAISHA YAKO - Innocent Morris

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 23 май 2024
  • JINSI YA KUACHILIA DAMU YA YESU KATIKA KILA ENEO LA MAISHA YAKO - Innocent Morris
    Jifunze kuachilia damu ya Yesu katika kila eneo la maisha yako kila siku. Na utaona ushindi mkubwa katika maisha yako. Kwa maana kuna nguvu kwenye damu ya Yesu.
    "Kwa kuwa Bwana atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, Bwana atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi."
    Kutoka 12:23
    Ukiachilia damu ya Yesu nyumbani kwako, kazini kwako, kwenye biashara yako n.k Bwana hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwako na kuwapiga wewe na familia yako. Kwa maana damu ya Yesu imewafunika. Maana yake ni kwamba kuna ulinzi katika damu ya Yesu.
    Damu ya Yesu ina nguvu ya kukulinda wewe pamoja na familia yako, na kila kitu ulicho nacho.
    MAOMBI:
    "Ee Bwana Yesu, asante kwa damu yako takatifu iliyo mwagika pale msalabani. Ninafunika nyumbani yangu, watoto wangu, mume/mke wangu, biashara zangu, kazi yangu, afya n.k kwa damu yako takatifu katika jina la Yesu Kristo. Amina."
    Somo hili tumewawekea kwenye channel yetu ya RUclips ya Holy Spirit Connect linaitwa JINSI YA KUACHILIA DAMU YA YESU. Link ipo kwenye bio hapo juu.
    Somo litakusaidia kutembea katika ushindi katika damu ya Yesu kila siku.
    Ubarikiwe sana.
    Innocent Morris
    +255652796450 (WhatsApp)
    Instagram Page: holyspiritconnect
    Facebook Page: Holy Spirit Connect
    Contact: +255652796450 (WhatsApp)
    Instagram Link:
    / holyspiritconnect
    Facebook Link:
    / holyspiritconnect
    RUclips Link:
    / holyspiritconnect

Комментарии • 44