Fafanuzi rahisi ya kitabu cha UFUNUO WA YOHANA - Sura ya 11(Na Bishop Dr. Fredrick Simon)

Поделиться
HTML-код
  • Опубликовано: 25 окт 2024
  • Fafanuzi rahisi ya kitabu cha UFUNUO WA YOHANA - Sura ya 11(Na Bishop Dr. Fredrick Simon)
    MASHAHIDI WAWILI AU MIZEITUNI MIWILI - SURA YA 11
    11:1 Kipimo cha hekalu la kipindi cha Dhiki Kuu. Mwanzi mmoja ulikuwa na urefu
    wa futi 20.
    “2 ....... nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili. 3
    Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku
    elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia.”
    Hao ni manabii wawili watakaotoa unabii kwa miezi 42 au siku 1260 (Hiyo ni
    sawa na miaka 3½ ) ya mwishoni mwa kipindi cha Dhiki kuu. Manabii hao ni Eliya
    na Henoko.
    Wengine hudai ni Eliya na Musa, kwa kuzingatia miujiza inayotajwa; mimi naamini
    ni Eliya na Henoko, kwa sababu:-
    a. Wote wawili hawakufa katika nyakati zao - MWANZO 5:24;
    2WAFALME 2:11.
    Wakati huo watauwaliwa na Mpinga Kristo kwa idhini ya Mungu mwenyewe
    (11:7,8). Kwa sasa wapo mbinguni wakiwa na miili ya duniani!.
    b. Wote wawili walikuwa manabii - YUDA 1:14; 1WAFALME 18:22.
    #UFUNUOWAYOHANA #mashahidiwawili #fredricksimon #ufunuo #mungu #siri #sikuzamwisho

Комментарии • 3