SAKATA LA KUUNGUA KWA KIBANDA CHA ASLAY MIHOGO, KAMANDA, DC KINONDONI WATOA TAMKO 'VITU VINGI'...
HTML-код
- Опубликовано: 25 дек 2024
- . Wasimulia moto ulivyoteketeza mgahawa wa Aslay Mihogo
Alfajiri ya Desemba 25, 2024, moto ambao chanzo chake hakijajulikana umeteketeza mgahawa wa mfanyabiashara maarufu, Aslay Mihogo, eneo la Coco Beach, jijini Dar es Salaam.
Mwananchi Digital imefika eneo la tukio ili kufuatilia chanzo cha moto huo, mashuhuda walioshuhudia mkasa huo walieleza kilichotokea.
Aziz Jumanne Mapande, mmoja wa mashuhuda, amesema, "moto ulianza majira ya saa 11 alfajiri, tulianza kuona moshi ukipanda, kisha gesi zikaanza kulipuka, hadi Jeshi la Zimamoto kufika, vibanda vingi vilikuwa tayari vimeteketea."
Fahami Mohamed Seif, amesema: "Ajali ilitokea saa 11 alfajiri na ilitokana na shoti ya umeme. Tulikuwa wawili tumelala ofisini baada ya kuchelewa kurudi nyumbani jana, tulipoona moshi ukitanda na gesi zikianza kulipuka, tulikimbia kuokoa maisha yetu."
Jeshi la Zimamoto lilifanikiwa kudhibiti moto huo kabla haujasambaa zaidi, ingawa banda lote liliteketea.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kinondoni, Mtatiro Kitinkwi, akizungumza na waandishi wa habari, amesema vitu vingi vilivyokuwa katika vibanda hivyo vimeteketea, uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini chanzo cha moto huo.
Pole sanaa jmn
Hii inaitwa system update.... Advertisement ya matajiri budaa.. Ngoja uone sasa mjengo wa maana hapo
😂 we jaman inasikitisha😢😢😢😢
Wivu roho mbaya kwanini krisimasi
Hujuma hzo na wivu